Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Huwa uko smart, Ila wewe ni mdini flani, Yani ikifika dini yako haijaguswa huwa unajitoa ufahamu. Acha udini mkuu, Raisi angekuwa mkristo ungeweza anapendelea Imani yake
 
Changamoto ni hiyo balance. Imagine wewe ndio rais unawaambiaje wasaidizi wako, nileteeni watu watano wa dini A na watano wa dini B?
Ni rahisi tu, unawaambia nileteeni watu 500 wenye vigezo na unawaagiza wawape maksi kutoksna na vigezo vya vetting—Kisha bada ya hapo unapick watu 20 kutoka miongoni mwao wewe mwenyewe kwa misingi ya haki bila kulalia kundi moja.
Sasa wakileta watu 500 kisha list yao ikawa ya kibaguzi, ubaanza kutimua kazi haohao wanaofanya upuuzi huo
 
Wewe unataka kuyumbisha taifa.

Pita kule nenda zako shetani.

Sijawahi kuona manufaa yoyote kwangu kutokana na kiongozi wa dini yangu kuteuliwa...

Zaidi zaidi naona familia yake iki enjoy zaidi
Halafu kuchagua mtu kisa dini yake kwani ni nafasi za ma shekhe,askofu, nchungaji au baba paroko. Watu watumiao udini, au ukanda kupata Jambo ni hatari kwa mstakabali wa umoja wakitaifa
 
Waraka wako cc ni kwa Waislamu watupu!
Ndo ujue sisi wengine tunatetea principle.

Rais akiwa Muislamu na akafanya teuzi za kibaguzi tutasema

Na raisi asipokuwa muislamu na akafanya teuzi za kibaguzi tutasema pia

Issue siyo nani ni rais au Waziri mkuu, ISHU HAPA ni UTEUZI umemarginalize waislamu na wanawake. Kwa hiyo tuna haki ya msingi kabisa ya kuhoji, Je katika makundi hayo mawili kuna watu wachache mno wenye sifa za kuhudumu katika hizo nafasi hadi ionekabe kuwa watu wa dini moja ba jinsia moja ndo wanaotosha?
 
Sasa ulitaka amteue babu Tale?
 
Mkuu ww udini unakusumbua hilo kwanza ukili tu.....Hii nchi hakuna mtu anachaguliwa kwa udini wake bali kwa uwezo wake.Sikatai wakristo wanakua wengi husikii watu wanalalamika kua waziri mkuu na Rais na katibu mkuu ni waislam na hivo ni vyeo vikubwa sana mbona wakristo hawalalamiki au kuna mkristo kalalamika kua kwa nn Rais katoka zanzibar na ni muislam.Mimi ndo hua nasema uislam hua unaharibiwa na watu km nyinyi maana ww ubinafsi unakusumbua sana na udini.
 
uzi mreefu lakin hoja dhaifu! ulipoongelea kugawana keki ya taifa nikaishia hapo. kwani mtu anachaguliwa akale keki ya taifa au akachape kazi? na hiyo kazi inafaidisha kidini au watanzania kwa ujumla wao! kwa tanzania kuna virus hutafanikiwa kirahis kuipandikiza. jadiri cv ndugu.
 
Mkuu katiba inasema nchi yetu haina dini,pia hata katika sensa hatuulizi dini wala kabila .Unakotaka kutupeleka siko. Mimi ni mkiristo lakini hakuna ninachofaidi kamamimi binafsi kutokana na kuwa eti viongozi wengi ni wakiristo,barabara ninazopita hazisemi zimejengwa na mkristo na kila mtu anajipitia,shule,madaraja,vyuo ,flyover vyote havisemi ni mkristo kajenga kwa hiyo muislamu asipite.Zanzibar karibu asilimia 99% ya viongozi ni waislamu je muislamu wa kawaida yeye binafsi anaufaika nini na kuwa viongozi ni waislamu,kule Zanzibar kuna wakristu hatujawahi kuwasikia wakilalamika kuwa viongozi wote ni waislamu kwa hiyo wanaofaidi keki ya taifa ni waislamu, sisi tunataka maendeleo kwa wote hata awekwe mpangani muhimu ni maendeleo, ukitaka hivyo hamia Zanzibar ukafaidi huo Uislamu.
 
Sifa zina vipimo, je ukipita list nzima ukakuta katika top 50, 90% wote ni wa dini fulani utafanyaje?

Leo hii ukichukua watu wote wenye PHD hapa Tanzania, nina uhakika kutakuwa na over-representation ya makabila flani hivi, kwa hiyo sio bahati mbaya kwamba kwenye michujo wanapenya sana, wako wengi kwa vigezo sio wingi wa watu tu.
 

Katiba imeliweka vizuri sana suala la kutopendelea watu wa dini moja ila nashangaa teuzi nyingi huwa zinalalia watu wa dini moja, Ndiyo maana nataka uchunguzi ufanyike ili tujue kuwa hizi Mamlaka za Vetting na uteuzi hakuna motive ya udini katika hizi teuzi.
Hsiwezekani Always waislamu wawe wachache tena wachache kwelikweli kwenye kila yeuzi inayoinvolve watu wengi
 
Usipojali demographia ya nchi, unaweza kuteua makatibu wakuu wote wahaya, halafu ukajiaminisha kuwa maadamu wana vigezo basi hakuna tatizo—Tatizo lipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…