Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Mkuu wadau humu wamechangia na kukujibu vizuri sana na kuna hoja nzito zimeiburiwa kutokana na uzi wako lakini umeshindw kuzijibu..naomba upitie vzuri michango ya wakuu humu.ina hoja na maswali mazito sema wameondika katika hali fikirishi.....kama bado hutaelewa,itabidi watu waanze kuandika magazeti ili kukuelewesha
 
Nafasi zote za teuzi za rais huwa hazifiki watu 3000.
Sasa waislamu Graduates, wenye sifa na vigezo wanazidi nafasi zote hizo nilizozitaja.

Sasa ukiniambia eti hakuna waislamu wa kutosha kuteuliwa mpaka ipelekee teuzi zifanyikazo zilalie kwa sana kwa watu wa dini moja kila wakati ni hoja ambayo haina ukweli wowote.

Sasa ukiteua makatibu wakuu 20, unataka kuniabia nchi hii hakuna waislamu 8, 9, 10, 12 wenye vigezo vya kuwa makatibu wakuu?
 
hii mada ingekuwa na hoja endapo mtoa mada angetuambia Wakristo ni asilimia ngapi ya wananchi wote na Waislam ni asilimia ngapi
maana huwezi kutaka uwe na 50% ya teuzi zote huku kwenye population upo kwa 25%
 

Hizi teuzi zimefanyika kwenye kipindi cha Easter ndiyo maana zimewa-favor ndugu zetu wakristo ngoja afanye teuzi katika kipindi cha Ramadhani utaona nao waislamu watakavyopewa shavu.
 
hii mada ingekuwa na hoja endapo mtoa mada angetuambia Wakristo ni asilimia ngapi ya wananchi wote na Waislam ni asilimia ngapi
maana huwezi kutaka uwe na 50% ya teuzi zote huku kwenye population upo kwa 25%
Waislamu waliomba sensa ya mwaka 2012 iwe na kipengele cha dini ya mtu, Kanisa na Serikali vikapinga.

Kimsingi Waislamu walitaka mfano wa mambo hayahaya ninayokemea ya viashiria vya ubaguzi kwenye teuzi vikome, maana data zinaonyesha representation yao kwenye nafasi za teuzi ni kiduchu sana kitu ambacho kinahitaji utafiti wa kitawala, kwa nini Myslims siku zote ni wachache kwenye teuzi, Je kuna udini behind?, Je hawapo wa kutosha wenye vigezo?, ni kwa namna gani vetting inafanyika?—Vyote hivyo lazima vifanyike ili tuzidi kupata nchi iliyofair zaidi!
 
Hii hoja kwamba waislamu hawajasoma ni hoja iliyopitwa na wakati, wapo mamia ya waislamu wenye PhDs na maelfu ya wenye digrii za kawaida
Naungana na wewe.Binafsi sipendi kukosoa dini za wengine as long as humanity unazingatiwa..sipendi kutawala na kuwa juu ya imani za wengine...kuwa dini fulani kusitujengee uadui.umeona katika ngazi mbalimbali kuna wawakilishi wa dini mbalimbali..inatosha KWA namna na sula hiyo ndg yangu.narudia tena kuna hoja zimeiburiwa humu je ujaziona mkuu?
 
hii mada ingekuwa na hoja endapo mtoa mada angetuambia Wakristo ni asilimia ngapi ya wananchi wote na Waislam ni asilimia ngapi
maana huwezi kutaka uwe na 50% ya teuzi zote huku kwenye population upo kwa 25%
Mambo ya udini kwenye teuzi yamepitwa na wakati, tujenge nchi yetu kwa maslahi ya watanzania wote.
 
Missile of the Nation Dini ikichanganyika na siasa katika nchi isiyokuwa ya kidini ni sawa uchanganye maji na mafuta. Wanadini wote ni sawa katika Tanzania hii, kuna leo na kesho labda leo unavyo ona wakristo wengi katika teuzi huenda kesho waislamu wakawa wengi kwenye teuzi, kwani kuna hata wakristo hawasapoti wakristo wenzi wao na kuna waislamu hawasapoti waislamu wenzi wao, hivyo haya ni mambo ya mpito tu.
 
Naunga mkono hoja....mfumo wa dunia uliopo sasa hauleti uwiano wa kijamii kisiasa na hata kiuchumi hivyo ni vigumu sana kuweka uwiano hata linapokuja kwenye swala la kidini....nyerere alijitahidi sana kubalansi haya mambo na aliibua hoja nzito sana kutetea uamuzi wake
 
Si vizuri ubaguzi kuupoza kwa lugha za kidiplomasia au kuufumbia macho kwa jicho la mshikamano.

Dawa ya ubaguzi ni kuuondoa, ili tuwe na taifa lenye fairness na haki kwa wote.

Ngoja nikuulize swali, leo hii rais akateua Wazanzibar watupu kwenye ukatibu mkuu, utaona tatizo au utaona ni sawa tu!?
 
Kaka naona tunashindwa kuelewana..na mda wa kujibu umeisha kumbuka ni mida ya kazi hii....ila natamani sana kubadilisha mawazo yako kwa kuwa ni hatari KWA ustawi wa nchi yetu hivyo itabidi niandike gazeti
 
Naona wewe ndugu yangu una shida, Dunia yote ktk nchi zote zinatumia system kama ya Tanzania na sio ya 1:1
Nenda hata ZnZ, Kenya, Uganda, Nigeria, Chad, CAR n.kn.k
Na ukienda USA au UK weupe watakuwa wengi kuliko Rangi yangu au yako na sio 1:1:1:1
 
Mimi kwangu awe Muislamu,Mkristo, Hindu e.t.c ninachopenda kuona ni
1.Katiba kuheshimiwa
2.HAKI isiwe jambo la hisani ya Kiongozi
3. Taasisi imara zisizoingiliwa na mhimili wowote kimaamuzi.

Kubwa zaidi watu waishe kwa furaha.
 
Hiyo ratio ni based on assumption katika nini?
 
Akifuata vigezo hakuna shida kwani watakuwa wanachukua maendeleo ya bara au resource zaidi ya hiyo ratio ya 96:4
 
Hoja ni kwamba, waislam wapo wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…