Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Kwamba kila Rais atakaye ingia madarakani nyumbani kwao inapelekwa miradi mikubwa bila kufanya utafiti wa kutosha wa mahitaji kwa fedha za walipa kodi hawa masikini.
Matokeo ni kuwa wanapo ondoka madarakani inageuka kama ile ya nyumbani kwa Mobutu maana ilikuwa kukurupuka.
Tumeona speed ya Chato kuibadili katika miaka mitano. Kuna vitu vilifanywa ambavyo sasa imegundulika ni matumizi mabaya ya rasilimali kwa ukubwa usio stahili.
Mfano Airport, Referral Hospital hadi majengo makubwa kama mabenki yasiyo stahili na mbuga za wanyama zisizo hadhi. Leo vyote vinakufa.
Sasa leo tumeanza na Kizimkazi! Miradi mingi inapelekwa kwa fedha zetu (tena za Bara kwa maeneo yanayostahili SMZ) nje ya budget kuu huku shughuli hizo zikichagizwa na mbwembwe nyingi za wasanii.
Hatubweki kama mbwa kuhusu maendeleo hayo bali ni utamaduni mbaya, maendeleo ni mipango na kupanga ni kuchagua, wehu ni pale unapochagua kununua Suti toka Piccadilly badala ya kununua godolo la kulalia kwanza.