Siwezi kukutajia vyakula moja Kwa moja ila unabidi ujitahidi kusoma aina ya vyakula
Mlo wako unatakiwa uwe na virutubisho vyote na kutokana na uchumi wetu watanzania hatuwekeani limit maana utaacha kula ugali unaoupata , ila chakula chako kisikose matunda na mboga mboga - na unatakiwa unywe maji lita 2-3 kwa mtu mzima ila iwe hasubuhi na mchana tunahepuka kwenda chooni kila mara Kwa kunywa maji mda wa usiku
Unatakiwa ule mda maalum,Mda wa kula pia uzingatie hautakiwi kula kila wakati au unapojihisi njaa tu ndio hapo hapo ulee, pia hepuka vyakula vya kukaanga mfano chips, maandazi nk
Nyakati za usiku hautakiwi ule na hapo hapo ukalale hapana- unatakiwa baada ya kula uwe active masaa 2 mpaka 3 ndio ukalale
Kwa kuanza mazoezi unaweza kuanza kutembea dk 30 mpaka 60- yaani lisaa limoja kama hautoweza kukimbia hautakiwi kujichosha sanaa utapunguza mwili kidogo kidogo
Mazoezi hasubuhi na jioni unabidi ulazimishe upate mda wa kufanya mazoezi usikose kufanya mazoezi