Uchaguzi 2020 Tunaojiandaa kumpa tena kura Rais Magufuli tukutane hapa

Ulishajiuliza hata siku moja ni kwa nini Magufuli anawaogopa wapinzani na hataki kabisa kuingia nao kwenye uchaguzi huru?.
 
Sawa,naona mipango ya kupata kura zote kwa kutumia wakurugenzi,tume nk umekamilika
 
Sasa bwashee kura zote,inamaana na mgombea wa upinzani atamchagua JIWE??
 
Kuna chama ukiwa humo hutakiwa kutumia akili kabisa kufikiri, hata kwa makalio unaweza kutumia kufikiri!
 
Kanywe supu kwenye hiyo buku7 ya Jana ndio uje hapa.
 
Magufuli atashinda vizuri mno tena kwa kura nyingi zaidi ya zile za 2015.
 
MKUU WA MKOA WA MANYARA KATANGAZA KUWA KWENYE MKOA WAKE HAKUTOFANYIKA UCHAGUZI JE LABDA HIZO NDIO MBINU ZA KUPATA KURA MAGU?



NA KAMA MNYETI KAANZA JUA NA MIKOA MINGINE ITAFATA MAANA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MANYARA NDIO ULIKUA MKOA WA KWANZA MKUU WAKE WA MKOA KUTOA MAELEKEZO YA KUWAKATA WAGOMBEA WA UPINZANI NA NASKIA WASIMAMIZ WAKAAMBIWA WAKIWAPITISHA WATAENDA NAO MAJUMBANI MWAO

KWA HIZI MBINU CCM ITAPATA KURA ZOOTE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je wajua kuwa hata wew kwa tume hii waweza pata kura zote regardless una huu upupu kichwani kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida hawa waleta hizi mada huwa hawawezi kuzitetea.. Wakishaweka wanapotea, na sababu ya kushindwa kuzitetea ni kw vile sio mabandiko yao bali wanaandikiwa... Ni sehemu ya praise team iliyo empty upstairs

Jr[emoji769]
 
Kwa mjibu wa Mwl Nyerere, Upumbavu nao ni kipaji
 
Hata ingekua ni mimi ndio rais, kama tume ya uchaguzi ni yangu, na vyombo vya ulinzi ni vyangu ningekua naamua tu nipate asilimia ngapi ya kura zinazopigwa, hata asilimia 100 naweza kupata

Na wenye uchu wa madaraka ndio mara nyingi hufanya hivyo.Wanawabana wenzao ili waendelee kutawala wao tu bila kupingwa,sasa jiulize wanang'ang'ania madarakani kwa nini kama wao sio wezi na walafi wa mali za umma??
 
Hahaha hata akimfukuza Makonda bado hatoshinda, wananchi wanamtaka Baraba!

Angemuita mwenyekiti wa ccm taifa amuulize kwanini chama kimeshindwa kuisimamia serikali, akishindwa kujieleza amtumbue adharani.
 
Kuna mfululizo wa post kama hizi zitakuja hapa kwa mfuatano wa bandika bandua kwa ID tofauti tofauti lakini mode of writing ikiwa inafanana...

Jr[emoji769]
Angalia hoja na kuichambua acha mapovu!
 
Atapata kura zote au anatamani apate kura zote? Aweke tume huru ya uchaguzi kisha tuone hizo kura zote.
Mmebaki kulalamika tu kwenye mitandao hakuna hoja za maana!
 
Kura za Dr Magufuli kwa mwaka huu wa uchaguzi hazitahesabika uhakika ni kwamba atapata 98% za kura zote.asante kwa kushiriki wapinzani.
 
Kwa kawaida hawa waleta hizi mada huwa hawawezi kuzitetea.. Wakishaweka wanapotea, na sababu ya kushindwa kuzitetea ni kw vile sio mabandiko yao bali wanaandikiwa... Ni sehemu ya praise team iliyo empty upstairs

Jr[emoji769]
Mkuu hiyo nimeandika mwenyewe, mimi sio mshabiki. Hebu jaribu kusoma hoja za wapinzani wa jamii forum kwenye huu uzi. Ukizisoma utaelewa nilicho kuwa nakisema kuwa akili zao zimejaa negativity, ndimi zao ni kama za simba, wanatoa maneno machafu yasio na sera ndani yake. Maneno kama hayo wewe unazani yanaweza hata kumponya mtu kweli? Zaidi zaidi ni kumkatisha tamaa. Wapinzani wajifunze kutafakari kabla ya kutoa meneno yao, hiyo ndiyo hekima mkuu. Badirikeni ndugu zangu, mtu aliye elimika anatambuliwa kwa kile anachokitoa kichwani mwake, anatambulika kwa Tabia yake.

Mkitaka mwe wapinzani wazuri jaribuni kujifunza kwa wapinzani wa mataifa yaliyo endelea kama Marekani. Hivi leo tukisema tuandikie vizazi vijavyo maneno ya mpinzani mmoja wapo kwenye vitabu, tutaandika ya naani? Ukiangalia clip za kina Martin Luther, unajifunza nini mkuu, tatizo hamtaki kujifunza jinsi ya kufanya siasa, mnaenda kwa mihemko. Mnachagua viongozi kwa mihemko, mwaka 2015, mnakumbuka mlicho tufanya? Tatizo hamwelewi mnakokwenda wala hamjui mnachotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…