Tunaojihisi kuchoka na kitu fulani tufarijiane

Tunaojihisi kuchoka na kitu fulani tufarijiane

Usichoke mamii. Hakuna maisha rahisi.

Tunaendelea kuishi kwa sababu hatujakata tamaa. Na pia tuna wanaotuangalia na kututegemea. Muhimu uhai, uzima na nguvu.

Wazee wetu wangechoka tusingekuwa hapa tulipo saivi.

Screenshot_20220424-221428_WhatsApp.jpg
 
Pole madam, kinachokuchosha ni kutokuwa katika mahusiano yenye furaha na baba watoto. Aidha yamekwisha au bado yapo. Jaribu kufikiri ulikosea au ulikosewa wapi katika hayo mahusiano. Kingine Umri unaenda na watoto unao. Pengine kituo chako Cha kazi kipo kijijini na kila mwanaume unayemuona siye yule wa hadhi yako uliyokuwa unaifikiria ukiwa mwanafunzi.

Kitu kikubwa ambacho baadhi yetu watumishi hatutaki kukiona ni kama tatizo, ni ile miaka saba ya kutopandishwa mishahara au madaraja! Iliua matumaini ya kiuchumi ya mtumishi na ndoto za maisha pamoja na motisha ya kufanya kazi. Vitisho na migogoro na mabosi na watumishi wengine pia uongeza stress.

Umechukua mikopo benki wanakukata marejesho,bodi nao wanakata na unabaki na salio dogo la mshahara. Mzunguko wa kibiashara ni mgumu katika eneo lako na kila ukiangalia hakuna kipya!

Uzuri ni kwamba kazi ya ualimu ina mapumziko makubwa kuliko kazi nyingine nyingi. Kipindi cha likizo safiri na badilisha mazingira na mtazamo wako. Walimu wengi utakuta yupo kituoni miaka sita au saba hajaenda likizo! Kisa? Kuogopa nauli hasa akiwa na familia kubwa.
Yaani haya maisha hayaeleweki eleweki saivi.

Mie mwenyewe hutamani siku moja niamke nipeleke barua ya 24 hrs resignation kazini . Ila kila nikiangalia usawa wa hali ya maisha nakuwa mdogo km piriton. Tuna kazi tunaganga njaa jee tukiziacha. Mifumo hairuhusu [emoji3064]
 
Kikubwa ni kupambana tu mpaka pumzi ya mwisho kwaajili ya watoto wetu! Wao hufurahia tu wanapotuona ndio wanaotupa nguvu ya kupambania maisha usikate tamaa jitie nguvu mtumishi mwenzangu!
Barikiwa sana mama
 
Najua ni muda wa kaz huu,ila tulikuwa na kaz ya kuhakikiwa Ivo imekwisha mapema sana Leo inategemea na kuwahi kwako(tunahakikiwa Kila Leo[emoji849]).

Sasa ni hivi,Kuna muda unajihisi kuchoka na Kila kitu au kitu Fulani.Kwa mfano Mimi nimechoka na

1.Mapenzi(kuwa kwenye mahusiano)
2.Kuongea na watu kwenye simu kuhusu mapenz (hapa ndo nimechoka kabisaa,yaan sitaki)

3.Kufikiri yaan kichwan kimechoka kuwaza hili na lile at least namna ya kupata hela na kulea watoto napata faraja kuwazia Ivo vitu lakini siyo kumfikiria Fulani sijui,kufikiria sijui nn

4.Nimechoka na kaz yangu(ualimu) kuwahi asubuhi kwenda kuitumikia kaz inayonididimiza kiuchumi,I wish hiyo 11 alfajiri ninapoamka kuoga nioge Kwa biashara yangu nitakayotesekea mpaka usiku lakini inanipatia mafanikio.

5.Nimechoka kuishi pia,mechoka sana kiukweli ni vile nina watoto naogopa nikizima watateseka.

Ee Mwenyez Mungu nisaidie,pekeyangu siwez pasipo msaada wako.[emoji120]


Kama tupo wengi katika hili tufarijiane bas
Mkuu yaani mimi ndoo nichoka zaidi yako ila pole tutafika tu mungu yupo pamoja nasi .dunia ina hii ni ngumu inatunyanyasa mpaka akili analock
 
Back
Top Bottom