Ikabidi Wafanyakazi Tufunguke kwa Askari namna Tulivotukanwa na Kutishiwa hatulipwi Mishahara yetu, yule Askari akaamuru Bosi apigiwe simu, hivo akapigiwa simu(Bosi wa Kiume ambae ni Mume wa yule Mama) na Kwa Bahati nzuri Supervisor alifanya akili akarekodi Voice ya Mazungumzo baina ya Askari na Mwajiri Wetu.m hivo ushahidi wa Voice Tunao ambapo Yule Askari aliamuru Siku inayofata (29-January-2022) saa 2 asubuhi Bosi akutane na Wafanyakazi wote kusolve hili tatizo na Atulipe Mishahara Yetu lasivo tukishindwa Kuelewana Turipoti kituo cha Polisi ili Tuelekezwe wapi tutapata Msaada.
Ikabidi Tuwajulishe na Wenzetu ambao waliingia shift ya Mchana yaliojiri usiku huo ili wote Tukutane asubuhi.
Siku ya Pili tulifika Kazini asubuhi tukimsubiria Bosi kabla ya Muda wa kazi Kufika (Mgahawa unafunguliwa saa 6 Mchana),
Yeye na Mkewe waliwasili saa 5, Wakatuita Tuongee na sisi tukatii, Tulikua 15, Bosi wa Kiume akaomba Supervisor ajitokeze na alivojitokeza tu Gafla yule Bosi akamtukana Matusi na Kumsukuma. Sisi wote tukainuka na Kuondoka kwani tuliona Hamna Usalama.
Baada ya dakika Chache Likaja Defender likataka kumchukua Supervisor Pekee ila akajitetea ana madai yake ya Mshahara pamoja na Sisi wengine hivo Wote tukapanda kwenye Gari kasoro watu 3 walibaki waliona Sio Dalili nzuri.
Hilo ndo kosa Tuliofanya, baada kufika Polisi Tukaeleza Madai yetu ya Mishahara, yule Mama akadai sisi tuna wiki mojamoja Kazini hivo hawez kutulipa kitu ambacho ni Uongo!
Pia Ilivofika Saa 12 Jioni Mkuu wa Kituo akasema Tupo chini ya Ulinzi tusubiri Kupelekwa Lockup, na yy pamoja na Askari wake waliondoka Na Bosi zetu Wakidai wanaenda Kufanya Uchunguzi, ila ukweli ni kwamba walialikwa Mgahawani na Kupewa Dinner ya Nguvu (Wenzetu waliobaki Kazini walitutonya)
Polisi waliporejea Kituoni saa 3 Usiku tuliruhusiwa Kurudi nyumbani kwa Sharti kwamba iwe Siri kwamba Hatukulazwa Lockup hata Wenzetu waliobaki Kazini tusiwaambie Siri hii.
Hatimae wakaamriwa Watulipe Mishahara Yetu na wao wakasema Watatulipa siku ya Jumanne hapo Kituoni.