Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Wasalaam wapendwa!

Kila mara humu mtu ukisoma vizuri comments za kila mada huwezi kupita bila kukutana na neno UNAFKI. Hili neno linasemwa kulingana na sisi wenyewe tulivyo na vitabia vyetu.

Hivi Tundu Lissu kabla haijapigwa risasi akachungulia kaburi na kurudi tuwahi kusikia akiitwa msaliti na nani?

Hebu vaa viatu vyake chukulia kua wewe ni tundu Lissu,
1. Upigwe risasi 16 saa 7 mchana kweupe na mpaka leo hii wasijulikane waliotenda tukio hilo
2. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu unyimwe gharama za matibabu yako kama mbunge bila sababu yeyote ya msingi
3. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu mpaka leo unyimwe nafsi yako ya ubunge na stahiki ziingine
4. Chukulia hii wewe ni Tundu Lissu unaporwa ubunge wako hadharani bila sababu ya msingi
6. Chukulia wewe ndio yeye unapata matatizo watu wanazuiwa hata kukusanyika kukuombea kwa Mola upone
6. Chukulia wewe ni Tundu Lissu unaarifiwa na vyanzo vya ndani ya mfumo kama asemavyo yeye kua ilitolewa amri kua shughuli ilitakiwa imalizike mapema kisha apumzishwe haraka kijijini kwao mapema bila kuagwa, hivi kwa maneno haya upendo utoke wapi?

Tunaomwita Lissu mtumwa wa Mabeberu hebu mfikirieni na yeye kwa vyote aliyofikia nayo. Mbona hatukumwita msaliti kabla? Hivi yeye si binadamu na asinune wala kuchukua ana moyo wa chuma?
 
Tundu Lissu alikuwa majeruhi tukakatazwa kufanya Ibada za kumuombea na watu wote waliotaka kufanya hivyo walisakwa kama Majangili.

Jiwe kaumwa bila Sisi kujua na hatuku muombea pia. Jiwe amefariki tunaanza kuhamasishana Mshikamano mara Tumuombee.

Hivi kipi bora, KUOMBEA MAJERUHI au MAITI?

MUNGU ni fundi na Malipo ni hapa hapa Duniani.
 
mkuu hivi viatu kwa upande wangu naogopa hata kuvivaa kwa maana naweza kutoa adhabu kali kuliko ya sodoma na gomola,
haya yalimtokea mwanasiasa msomi wa sharia na maarufu, je ni wabongo wangapi waliokaa kama kondoo hawajui haki zao na hawajitanbui, vimewatokea mara ngapi wakafa na ma presha na magonjwa ya kisukari kwa kudhurumiwa haki zao? Mwacheni Lissu Amalize hasira zake msimpangie kaumizwa.
 
Tundu Lissu alikuwa majeruhi tukakatazwa kufanya Ibada za Kumuombea na watu wote waliotaka kufanya hivyo walisakwa kama Majangili.

Jiwe kaumwa bila Sisi kujua na hatuku muombea pia. Jiwe amefariki tunaanza kuhamasishana Mshikamano mara Tumuombee.

Hivi kipi bora, KUOMBEA MAJERUHI au MAITI?

MUNGU ni fundi na Malipo ni hapa hapa Duniani.
Hatari sn huyu mtu alikuwa hatari sn
 
Back
Top Bottom