Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Labda tuvae viatu vya usaliti kwa nchi yake.

Wakati tunapigania madini alisimama upande wa mabeberu.
Lisu ni mwanasheria.
Kazi ya sheria ni kumtetea mteja wake.

Kwani serikali haikuwa na mawakili katika hizo kesi??

Hiyo mikataba mibovu ya madini waliyoisaini ni kina nani !?
Ni serikali ya chama gani iliyosaini hiyo mikataba !?
Si serikali ya mbogamboga ndio waliruhusu mawaziri kwenda dubai kusaini mikataba ambayo ina NDA(Non disclosure agreements) ndani yake.

NB: usimlaumu Lisu kwa udhaifu na incompetence za mawakili wa serikali, kama walizidiwa hoja ni uzembe wao wa kutoelewa vizuri kazi yao. Na ilaumu serikali kwa kusaini mikataba mibovu na kuficha kwa wananchi.
 
Hivi chuki zako kwa JPM hadi lini? Unachosha
Ungeiacha ujinga unaweza kujadili vizuri. Kuna mtu amemtaja JPM hapa au una wasiwasi?
Hukumu ziingine Mungu anatoa yeye wala si hakimu wa mahakama ya misitu au wala si jaji Simba
 
Mbona tundu alisema kipindi cha kampeni kwamba amewasamehe wote watesi wake ila nikiona twit zake kule Twitter yule bwana bado anakinyongo...
Hata baada ya kusema hayo baada ya kugombea Uraisi Mataga wakaanzisha mashambulizi mapya

Lissu lazima ajibu mapigo
 
Mbona tundu alisema kipindi cha kampeni kwamba amewasamehe wote watesi wake ila nikiona twit zake kule Twitter yule bwana bado anakinyongo.
Kusamehe haimaanishi kutokuzungumzia.
Kwani umeona Lissu akifungua kesi mahali popote !?
Umeona akidai fidia za matibabu na mishahara yake !?

Kusamehe amesamehe kadiri moyo na nafsi yake vinaruhusu. Sasa kama unamlazimisha awe rafiki yake kabisa hayo ni matatizo yenu.
 
Mbona Billicanas ilivunjwa lakini Mbowe haongei ujinga ujinga kama huyo Tundu Lisu?
Kuvunjwa bills huwezi fananisha na mtu kunusurika kuuawa , mali inatafutwa sio uhai hivyo ni ujinga na upumbavu kulinganisha kubomolewa jengo na uhai wa mtu,tumia akili kidogo basi.
 
Lisu hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Anaropokwa sana,chuki kibao.
Akajifunze kwa Raila Odinga,alimsamehe Moi na yakaisha,huo ndio uanaume,na kuenda kumzika alienda.

Angeweza kujijengea jina sana kama angekaa kimya for now msiba upite.

TZ itajengwa na wananchi wazalendo,kuendelea kumponda Magu haisaidii wala kupunguza chochote.
Ajikite katika kujenga hoja madhubuti na zenye kuleta matokeo chanya kwa jamii.

So anataka kucelebrate mpaka when?
Ok muda ni mwalimu mzuri.
 
Tundu-Lissu-1.jpg

Ilikuwa azikwe fastafasta na ni marufuku kuomboleza

Huenda Waziri Mkuu angetudanganya na kutuambia kuwa Lissu kajishambulia kwa risasi
 
Wasalaam wapendwa!

Kila mara humu mtu ukisoma vizuri comments za kila mada huwezi kupita bila kukutana na neno UNAFKI. Hili neno linasemwa kulingana na sisi wenyewe tulivyo na vitabia vyetu.

Hivi Tundu Lissu kabla haijapigwa risasi akachungulia kaburi na kurudi tuwahi kusikia akiitwa msaliti na nani?

Hebu vaa viatu vyake chukulia kua wewe ni tundu Lissu,
1. Upigwe risasi 16 saa 7 mchana kweupe na mpaka leo hii wasijulikane waliotenda tukio hilo
2. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu unyimwe gharama za matibabu yako kama mbunge bila sababu yeyote ya msingi
3. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu mpaka leo unyimwe nafsi yako ya ubunge na stahiki ziingine
4. Chukulia hii wewe ni Tundu Lissu unaporwa ubunge wako hadharani bila sababu ya msingi
6. Chukulia wewe ndio yeye unapata matatizo watu wanazuiwa hata kukusanyika kukuombea kwa Mola upone
6. Chukulia wewe ni Tundu Lissu unaarifiwa na vyanzo vya ndani ya mfumo kama asemavyo yeye kua ilitolewa amri kua shughuli ilitakiwa imalizike mapema kisha apumzishwe haraka kijijini kwao mapema bila kuagwa, hivi kwa maneno haya upendo utoke wapi?

Tunaomwita Lissu mtumwa wa Mabeberu hebu mfikirieni na yeye kwa vyote aliyofikia nayo. Mbona hatukumwita msaliti kabla? Hivi yeye si binadamu na asinune wala kuchukua ana moyo wa chuma?
Kipindi Cha mzee wa msoga lissu hakuwai itwa msaliti

Ila kipindi Cha dikteta uchwara akaanza itwa usaliti

Lissu hakuwai badilika tangu enzi za mchonga hadi za dikteta uchwara

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
2
Tundu Lissu hafai kuwa Rais wa JMT. Mimi siyo CCM wala CHADEMA, yaani sina chama. Lakini sina trust na Lisu kabisa kwa usalama wa Taifa letu.
Ungevaa wewe viatu vyake nadhani sahizi ungekuwa ushakufa kwa kwa furaha maana kama hadi sasa unashindwa kuona ni jinsi gani tundu lisu anajaribu kupunguza maumivu ya moyo wake kwa kuachiwa kilema kwa kosa tu la kisema udhaifu wa kiongozi, hakustahili adhabu kubwa kiasi kile mbona kikwete aliweza kwenda naye hadi akamuacha salama, kwani kaanza kuongea wakati wa mgufuli pekee?
 
Jino kwa jino adi kieleweke, yaani ni mwendo wa kuwapiga spana adi mnyooke kisawa sawa ***** zenu....,,,eti leo na nyinyi mnajifanya mna roho??
 
Wasalaam wapendwa!

Kila mara humu mtu ukisoma vizuri comments za kila mada huwezi kupita bila kukutana na neno UNAFKI. Hili neno linasemwa kulingana na sisi wenyewe tulivyo na vitabia vyetu.

Hivi Tundu Lissu kabla haijapigwa risasi akachungulia kaburi na kurudi tuwahi kusikia akiitwa msaliti na nani?

Hebu vaa viatu vyake chukulia kua wewe ni tundu Lissu,
1. Upigwe risasi 16 saa 7 mchana kweupe na mpaka leo hii wasijulikane waliotenda tukio hilo
2. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu unyimwe gharama za matibabu yako kama mbunge bila sababu yeyote ya msingi
3. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu mpaka leo unyimwe nafsi yako ya ubunge na stahiki ziingine
4. Chukulia hii wewe ni Tundu Lissu unaporwa ubunge wako hadharani bila sababu ya msingi
6. Chukulia wewe ndio yeye unapata matatizo watu wanazuiwa hata kukusanyika kukuombea kwa Mola upone
6. Chukulia wewe ni Tundu Lissu unaarifiwa na vyanzo vya ndani ya mfumo kama asemavyo yeye kua ilitolewa amri kua shughuli ilitakiwa imalizike mapema kisha apumzishwe haraka kijijini kwao mapema bila kuagwa, hivi kwa maneno haya upendo utoke wapi?

Tunaomwita Lissu mtumwa wa Mabeberu hebu mfikirieni na yeye kwa vyote aliyofikia nayo. Mbona hatukumwita msaliti kabla? Hivi yeye si binadamu na asinune wala kuchukua ana moyo wa chuma?
Aliyepanga kummaliza tundu lissu bado yuko mtaani....sio jpm, huyu sababu alikua mpinzani wake basi ni rahisi kumdondoshea jumba bovu..ila mbaya wake bado yuko mtaani.
 
Huo ukibaraka mmempa baada ya kupigwa risasi. Kabla ya hapo hata wewe ulimsifu
 
Aliyepanga kummaliza tundu lissu bado yuko mtaani....sio jpm, huyu sababu alikua mpinzani wake basi ni rahisi kumdondoshea jumba bovu..ila mbaya wake bado yuko mtaani.
Kwanini yupo mtaani mpaka sasa? Yeye ni jini haonekani?
 
Mbona Billicanas ilivunjwa lakini Mbowe haongei ujinga ujinga kama huyo Tundu Lisu?
Hizi ndio akili za MATAGA.

Kwa hiyo wewe unaona mali na uhai vina thamani sawa !?

Au unataka yeyote aliyeonewa akae kimya tuu kwa kuwa mtu kafa !?
Serikali hii hii iliyoshiriki kutoa maamuzi ya hovyo wakati mtu akiwa mahututi na kumdhulumu stahiki zake mara baada ya kugundua amevuka bonde la uvuli wa mauti leo hii mnataka anyamaze !?
Kwa mazuri yapi !?

Msipangie watu namna ya kuomboleza, kila mtu ana namna yake. Na sio lazima shujaa wako awe shujaa wake.
IMG_20210320_145257.jpg
 
Back
Top Bottom