Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Tunaomlaumu Tundu Lissu hebu basi tuvae viatu vyake

Mbona tundu alisema kipindi cha kampeni kwamba amewasamehe wote watesi wake ila nikiona twit zake kule Twitter yule bwana bado anakinyongo.
Hicho kinyongo bado ni kidogo sana achinje ng'ombe 1000 atuarike twende tukasherekea , mbona Abood kachija watatu hamsemi?
 
Wasalaam wapendwa!

Kila mara humu mtu ukisoma vizuri comments za kila mada huwezi kupita bila kukutana na neno UNAFKI. Hili neno linasemwa kulingana na sisi wenyewe tulivyo na vitabia vyetu.

Hivi Tundu Lissu kabla haijapigwa risasi akachungulia kaburi na kurudi tuwahi kusikia akiitwa msaliti na nani?

Hebu vaa viatu vyake chukulia kua wewe ni tundu Lissu,u
1. Upigwe risasi 16 saa 7 mchana kweupe na mpaka leo hii wasijulikane waliotenda tukio hilo
2. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu unyimwe gharama za matibabu yako kama mbunge bila sababu yeyote ya msingi
3. Chukulia wewe ndio Tundu Lissu mpaka leo unyimwe nafsi yako ya ubunge na stahiki ziingine
4. Chukulia hii wewe ni Tundu Lissu unaporwa ubunge wako hadharani bila sababu ya msingi
6. Chukulia wewe ndio yeye unapata matatizo watu wanazuiwa hata kukusanyika kukuombea kwa Mola upone
6. Chukulia wewe ni Tundu Lissu unaarifiwa na vyanzo vya ndani ya mfumo kama asemavyo yeye kua ilitolewa amri kua shughuli ilitakiwa imalizike mapema kisha apumzishwe haraka kijijini kwao mapema bila kuagwa, hivi kwa maneno haya upendo utoke wapi?

Tunaomwita Lissu mtumwa wa Mabeberu hebu mfikirieni na yeye kwa vyote aliyofikia nayo. Mbona hatukumwita msaliti kabla? Hivi yeye si binadamu na asinune wala kuchukua ana moyo wa chuma?
Kuna mambo hapa duniani hufanyika ni magumu na kila unapoyaelezea unaweza kuwa unatoa machozi na kulia, Lakini cha ajabu, yakisha kutendeka hayabadiriki tena hata ukivimba na kuvimba Kwa uchungu ukiekezea,

Kuendelea kuyakumbuka ni kujiumiza Kwani huwezi kuyabadirisha, una heri moyo wa kusamehe

Utu hupimwa Kwa uendelevu wa mtu kule aendako na siyo atokako

Ukiniuliza Mimi kuhusu Tundu Lissu Kwa sasa, nitasema, huyu Lissu ni mbaya kuliko anayemsema kuwa ni mbaya!!

Kwa maana ni wangapi ambao wamepatwa na ulemavu wa kusababishiwa lkn Bado walivaa ubinadamu wa kusamehe na kumwinulia Mungu sifa, na unajiuliza, kama ingetokea ndio amekufa siku hiyo, hii lawama angekuwa anaitupa wapi???

Swala lililopo ni kumshukuru Kwanza Mungu Kwa kubaki salama na kwamba Hadi sasa yupo, Swali lake ingelikuwa ni kumu, uliza huyu Mungu aliyeamua abaki, ni lipi anapaswa afanye, na Kwa nini aliamua yeye abaki mbali na kwamba mpango wa maadui zake ilikuwa kwamba afe!!!?

Kama Hana hata hiyo akili, basi yeye ndio mbaya kuliko maadui zake,
 
Labda tuvae viatu vya usaliti kwa nchi yake.

Wakati tunapigania madini alisimama upande wa mabeberu.
Msaliti yoyote wa nchi haachwi, iwe tanzania, urusi, marekani.
Kuna mipaka ukivuka uachwi tena risasi moja tu wanakuondoa, hata kwenye bible mfalme Suleman kuna watu aliwawekea mipaka na kuna watu aliwaondoa.
 
Mbona Billicanas ilivunjwa lakini Mbowe haongei ujinga ujinga kama huyo Tundu Lisu?
Hivi watetezi wa Hayati Jiwe na CCM yenu hamfahamu tofauti ya Mali na Uhai/Utu wa wanadamu wengine(Wasiowasujudia)?Billicanas na uhai wa MTU vinaulinganifu wa maumivu?
Mbaya kuliko vyote ni Roho mbaya zenu kwa kuwaficha Watanzania habari za kuuguliwa na Rais wao Hayati JPM hadi mauti yalipowaumbua.Mkiulizwa Rais yupo wapi mlitujibu shombo,alipofariki mbona hamkutuficha?
Kuhusu Mh.Lissu,mlipomshambulia mlikejeli na kujiapiza kuwa hawezi kupona.Mungu wake akampigania,Madaktari wake wakatenda waliyowezesha Mwamba akapona kwa michango ya wasamaria baada ya kunyimwa stahiki zake za kimatibabu kama Mbunge wa Bunge la JMT.Mkawapa majina waliomtibu na kumhifadhi kuwa ni mabeberu.Mlitaka awashangilie.Amewahenyesha ile October 2020 hadi mkakimbilia NEC/POLICE/TISS na kupora Uchaguzi. Leo mnaomba mpendwe!
 
Msaliti yoyote wa nchi haachwi, iwe tanzania, urusi, marekani.
Kuna mipaka ukivuka uachwi tena risasi moja tu wanakuondoa, hata kwenye bible mfalme Suleman kuna watu aliwawekea mipaka na kuna watu aliwaondoa.
Unapaswa kujua kuwa hakuna kiongozi aliyepigana vita vya kiuchumi akafanikiwa na akabaki salama. Kiburi, dharau ,kujiona , kimewafikisha hapa
 
Sikatai kabisa kwamba TAL alifanyiwa ubaya na uhalifu wa kiwango cha juu.

Lakini alitakiwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwenye hili tukio. Angeweza kulitumia kuvuta hisia za wengi. Nasikitika ameshindwa kulitambua hilo kutokana na machungu ya mikasa iliyompata.

Ana kazi kubwa sana kurudisha imani kwa wananchi wa kawaida walio wengi.
 
Mkuu johnthebaptist:

Unafananishaje UHAI wa MTU na Mali.

Chukua Sekunde chache na ujaribu kutafakari kipi bora kwako au Kwa Familia yako, ROHO au MALI?
Hawa kazi yao ni kuimba mapambio,wanatanguliza matumbo mbele kuliko utu,kwa aliyofanyiwa ni wazi anauchungu sana na kuongea inamsaidia kupata ahueni,
 
Labda tuvae viatu vya usaliti kwa nchi yake.

Wakati tunapigania madini alisimama upande wa mabeberu.
Lissu aliyapigania hayo madini enzi za Mh.Mkapa wakati wa kuvutia wawekezaji.Aliitwa msaliti asiyelitakia Taifa lake mema kwa kupinga uwekezaji.
CCM wakaingia mikataba mibovu na kina Barrick,wakati wa makinikia alikuwa anawakumbusha ubaya wa mikataba mliyowekeana na wazungu inavyoweza kulidhuru Taifa letu,mnamwita msaliti tena?
Kwenye akili timamu hawawezi kuwa CCM.
 
Back
Top Bottom