Hiyo nyumba ya milioni 4 inakuwa na ukubwa gani?
Hebu niambie kwanza gharama za paa tu la kawaida kwa maana ya mabati, mbao, misumari na gharama za fundi labda naweza kujua nabishana na nani. Kumbuka mi naulizia paa tu!!
Tukitoka hapo ntakuuliza nyumba itatumia tofali ngapi na bei yake ikoje. Hayo madirisha/milango uniambie ni bei gani. Hapo umetaja tinted nikitafsiri ni aluminium frem na kioo chake... uniambie dirisha moja bei yake na madirisha yako mangapi...
Niishie kwanza hapo nione hilo bulungutu lako la milioni nne linavyoweza kujenga nyumba na wala sio choo
Sikusema M4 nilisema nimejenga kwa 10M, hata hivyo kwa M4 mimi najenga kajumba kakifahari tu sishindwi.
]Nyumba niliyoijenga kwa 10M ambayo nimekwambia ukiiona utasema nimetumia M70 ina vitu vifuatavyo.
.
Madirisha sita ya Aluminium (tinted) kwa 200K kila moja
Milango miwili 200K ni milango haswa
Tofali zilizotumika ni tofali za kuchoma elfu 10 ambalo bei yake moja ni 50 hivyo ilinitoka 500K
.
Bati kwa bei ya kule bati nilitumia bati 60 sawasawa na 780K
Mbao nililipia M1 pamoja na hela ya fundi wa kupaua yani nilienda nikakuta imekwisha funikwa
.
Misumari bei yake ni ya kawaida sana (misumari ya kofia)
Nyumba nimejenga kwa laki sita bei ya fundi hadi anafunga lenta isubirie kupauliwa tu!
Mifuko ya simenti iliyotumika kufungia lenta ni mifuko tisa kwa kila mmoja elfu 10,000 = 90K
.
Nyumba nilijengea tope kisha nikachapia na simenti kabla haijapigwa ripu hivyo sikuwa na ghalama za kutafuta mchanga wa kujengea wala simenti.
Magril ya madirisha kila moja lilinighalimu laki na thelasini kwa magril sita 780K.
.
Fundi wa kufunga magril na wa kufunga mavioo jumla ya fedha nilizowalipa ni 300K
Kilichokuja kuanza kunitafuna ni uwekaji malumalu, simenti ya plasta, rangi, gypsum board mbao za kufungia hayo magypsum zilini gharimu sana.
.
Hatimae kwenye M10 niliyoipangilia nilikamilisha mjengo wa aina yake, usije thubutu kulinganisha hata siku moja gharama za ujenzi za DSM kwamba ndio ziko kote
.
Kwamba M10 yote inaishia kwenye ununuzi wa tofali si ulofa huo, nakupa maajabu mengine nilivuta hadi maji kwa fedha ile ile pamoja na umeme juu na chenchi ikabakia
Note: kuna baadhi ya vitu sijavitaja na vimo ndani ya 10M