City Of Lies
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 4,925
- 6,137
Watu wanachukulia poa sana ujenzi hasa huu wa kisasa.Wewe subiri ukifukuzwa kwenu utajua gharama ya ujenzi.Kiwanja 20/40 ni mi 3-6 na inaweza zidi hapo,Fundi wa kupangaa tofali kwa siki moja ni 10k hadi 20k tofali moja ni 800-1200 cement mchanga nondo n.k.unafikiria milioni nane.Are you serious?
mkuu nimesika site yani hivyo vipimo ni avipo ni kwamba urefu ni mita kama 20 na upana ni mita 12,naamini ata wewe ukienda hiyo m7 hutotoa.hilo ni banda sio "nyumba".....au unatumia kigezo kuwa nyumba hujengwa kwa tofali na hapo tofali zimetumika kwa hiyo hilo banda ni nyumba?fikiri tena ninayo taslimu 7m
Tuoneshe mkuu..Nakataa, kwa mikoani hasa Morogoro unajenga Nyumba kwa milion 4 ya tofali za kuchoma na unaweka bati na madirisha na sakafu yako fresh unaishi.
.
Tena ikifika M14 hiyo inakuwa ya kifahari sasa maana itakuwa na tinted, malumalu, na kila kitu!.
.
Nyie mmezoea kupigwa yani hiyo miliom 14 unakuta nyumba haijafika hata usawa wa madirisha imeisha watu tinabakiwa hadi na chenchi nikikuonyesha nyumba niliyojenga kwa M10 haki ya Mungu utasema nimetumia M70
Sikusema M4 nilisema nimejenga kwa 10M, hata hivyo kwa M4 mimi najenga kajumba kakifahari tu sishindwi.Hiyo nyumba ya milioni 4 inakuwa na ukubwa gani?
Hebu niambie kwanza gharama za paa tu la kawaida kwa maana ya mabati, mbao, misumari na gharama za fundi labda naweza kujua nabishana na nani. Kumbuka mi naulizia paa tu!!
Tukitoka hapo ntakuuliza nyumba itatumia tofali ngapi na bei yake ikoje. Hayo madirisha/milango uniambie ni bei gani. Hapo umetaja tinted nikitafsiri ni aluminium frem na kioo chake... uniambie dirisha moja bei yake na madirisha yako mangapi...
Niishie kwanza hapo nione hilo bulungutu lako la milioni nne linavyoweza kujenga nyumba na wala sio choo
Ahsante kwa ufafanuzi. Hapo nimeelewa tunatofautiana sana tunapozungumzia "nyumba ya kifahari" na nyumba ya kawaida. Hapa umezungumzia nyumba ya kawaida tofauti na ulivyosema awali kuwa 14M umejenga nyumba ya kifahari....Sikusema M4 nilisema nimejenga kwa 10M, hata hivyo kwa M4 mimi najenga kajumba kakifahari tu sishindwi.
]Nyumba niliyoijenga kwa 10M ambayo nimekwambia ukiiona utasema nimetumia M70 ina vitu vifuatavyo.
.
Madirisha sita ya Aluminium (tinted) kwa 200K kila moja
Milango miwili 200K ni milango haswa
Tofali zilizotumika ni tofali za kuchoma elfu 10 ambalo bei yake moja ni 50 hivyo ilinitoka 500K
.
Bati kwa bei ya kule bati nilitumia bati 60 sawasawa na 780K
Mbao nililipia M1 pamoja na hela ya fundi wa kupaua yani nilienda nikakuta imekwisha funikwa
.
Misumari bei yake ni ya kawaida sana (misumari ya kofia)
Nyumba nimejenga kwa laki sita bei ya fundi hadi anafunga lenta isubirie kupauliwa tu!
Mifuko ya simenti iliyotumika kufungia lenta ni mifuko tisa kwa kila mmoja elfu 10,000 = 90K
.
Nyumba nilijengea tope kisha nikachapia na simenti kabla haijapigwa ripu hivyo sikuwa na ghalama za kutafuta mchanga wa kujengea wala simenti.
Magril ya madirisha kila moja lilinighalimu laki na thelasini kwa magril sita 780K.
.
Fundi wa kufunga magril na wa kufunga mavioo jumla ya fedha nilizowalipa ni 300K
Kilichokuja kuanza kunitafuna ni uwekaji malumalu, simenti ya plasta, rangi, gypsum board mbao za kufungia hayo magypsum zilini gharimu sana.
.
Hatimae kwenye M10 niliyoipangilia nilikamilisha mjengo wa aina yake, usije thubutu kulinganisha hata siku moja gharama za ujenzi za DSM kwamba ndio ziko kote
.
Kwamba M10 yote inaishia kwenye ununuzi wa tofali si ulofa huo, nakupa maajabu mengine nilivuta hadi maji kwa fedha ile ile pamoja na umeme juu na chenchi ikabakia
Note: kuna baadhi ya vitu sijavitaja na vimo ndani ya 10M
Mkuu mmezoea kugalalizwa huku mnakokuita mjini, kiwanja changu kina square meter 360 nilikinunua kwa bei ya kawaida sana enzi za Jakaya Nyumba iko mtaa wa Rombo Morogoro ni mjini kabisa na wala si kijijini.Ahsante kwa ufafanuzi. Hapo nimeelewa tunatofautiana sana tunapozungumzia "nyumba ya kifahari" na nyumba ya kawaida. Hapa umezungumzia nyumba ya kawaida tofauti na ulivyosema awali kuwa 14M umejenga nyumba ya kifahari....
BTW huyu anayeuza hii nyumba anauza na kiwanja pia.... we umejenga ukiwa na kiwanja tayari... Nyumba ya madirisha sita.... itakuwa nyumba ya vyumba vingapi vya kulala? Vipi kuhusu sebule, dinning, stoo na choo vyote vilikamilika??
Siwezi kubishana na wewe mkuu kwa maana ya gharama ya ujenzi kwa Dar na Moro ni tofauti. Mathalan kiwanja kwa Dar kwa bei ya chini sana unazungumzia 5M... Sasa katika 14M umebakiwa na 9M... Tufanye nyumba itachukua tofali 2500... kwa gharama za hapa tayari ni 2.5M... Mchanga, nondo, kokoto kwa ajili ya msingi, nguzo, lenta na balcony unazungumzia sio chini ya 1M, Mabati tufanye unachukua ya bei ya chini kabisa... mabati 60 unazungumzia 1M nyingine, mbao za kupaua fanya tena 1M,... Madirisha sita (Umenishangaza kusema nyumba ya room 3 za kulala, sebule, jiko na choo ikawa na madirisha 6 pekee) hapa unazungumzia 1.5M, Frem za milango na milango yake... si chini ya 2M... Hapa sijazungumzia kabisa gharama za ufundi, wala sijaweka mambo ya tiles, gypsum, gharama ya shimo la choo, mabomba, wiring, plasta, rangi.....Mkuu mmezoea kugalalizwa huku mnakokuita mjini, kiwanja changu kina square meter 360 nilikinunua kwa bei ya kawaida sana enzi za Jakaya Nyumba iko mtaa wa Rombo Morogoro ni mjini kabisa na wala si kijijini.
.
Ina vyumba vitatu vya kulala, dinning hall, choo ambacho ni bafu humohumo, na jiko na vilikamilika ndio maana nilisema malumalu na magypsum yalinitafuna sana pesa la sivyo ningejenga kwa bei ya chini zaidi
Mwanzoni nilijua nitatumia tofali za kuchoma kama elfu 6-7 matokeo yake zikaongezeka na kufikia elfu 10, na ujenzi wa Morogoro tope liko hapohapo unachimbua tu, nyumba ikishakamilika pale ulipojengea tope unapachapia na simenti kabla hujapiga full plasta ili iwe imara na kumbuka tofali za kuchoma zina dumu mno hazina expire date kama tofali za simenti.
.
Ndiyo nyumba anayoishi mama yangu mzazi kwa mbele akaongeza frem za maduka ambazo alitumia matofali ya simenti hizi gharama alitoa yeye mimi bahili mno😂😂😂
.
Ushauri wa bure mkuu asprin unaweza kujenga nyumba kwa 20M hapa DSM ikaonekana ni ya M150 ukiamua yani unajitoa haswaa na naweza kukusaidia ukiwa mfungua pochi tu unaibiwa, kama ni tofali za huku lazima ziwe za Cement unafyatua wewe mwenyewe sio lazima mashine ubao tu unapunguza gharama na kufanya hivi si umasikini
Umehesabu hadi kiwanja?M14 si najenga na nahamia
Hiyo nyumba ya milioni 4 inakuwa na ukubwa gani?
Hebu niambie kwanza gharama za paa tu la kawaida kwa maana ya mabati, mbao, misumari na gharama za fundi labda naweza kujua nabishana na nani. Kumbuka mi naulizia paa tu!!
Tukitoka hapo ntakuuliza nyumba itatumia tofali ngapi na bei yake ikoje. Hayo madirisha/milango uniambie ni bei gani. Hapo umetaja tinted nikitafsiri ni aluminium frem na kioo chake... uniambie dirisha moja bei yake na madirisha yako mangapi...
Niishie kwanza hapo nione hilo bulungutu lako la milioni nne linavyoweza kujenga nyumba na wala sio choo
Hata mimi nawashangaa sana hawa jamaa aseeHata mimi nilishangaa, eti 4M ujenge nyumba ikamilike sababu bidhaa za viwandani, kama bati, cement, misumari, n.k. havina uhusiano na vijijini au mjini. Tena huko vijijini ndiyo bei inapanda zaidi. Juzi juzi tu kuna ndugu yangu kamaliza kupaua nyumba yake ya kawaida gharama za kupaua around 15M (5M Mbao, 5M bati, 3M Fundi, 2M misumari na mengineyo). Tuache utani ujenzi ni gharama!!
Lol kitunda, Yani majirani zako wakurya tu, hapana kwakwwli
Lol kitunda, Yani majirani zako wakurya tu, hapana kwakwwli
Mkuu hizo bati 60 kwa shilingi 780,000 gauge ngapi?Sikusema M4 nilisema nimejenga kwa 10M, hata hivyo kwa M4 mimi najenga kajumba kakifahari tu sishindwi.
]Nyumba niliyoijenga kwa 10M ambayo nimekwambia ukiiona utasema nimetumia M70 ina vitu vifuatavyo.
.
Madirisha sita ya Aluminium (tinted) kwa 200K kila moja
Milango miwili 200K ni milango haswa
Tofali zilizotumika ni tofali za kuchoma elfu 10 ambalo bei yake moja ni 50 hivyo ilinitoka 500K
.
Bati kwa bei ya kule bati nilitumia bati 60 sawasawa na 780K
Mbao nililipia M1 pamoja na hela ya fundi wa kupaua yani nilienda nikakuta imekwisha funikwa
.
Misumari bei yake ni ya kawaida sana (misumari ya kofia)
Nyumba nimejenga kwa laki sita bei ya fundi hadi anafunga lenta isubirie kupauliwa tu!
Mifuko ya simenti iliyotumika kufungia lenta ni mifuko tisa kwa kila mmoja elfu 10,000 = 90K
.
Nyumba nilijengea tope kisha nikachapia na simenti kabla haijapigwa ripu hivyo sikuwa na ghalama za kutafuta mchanga wa kujengea wala simenti.
Magril ya madirisha kila moja lilinighalimu laki na thelasini kwa magril sita 780K.
.
Fundi wa kufunga magril na wa kufunga mavioo jumla ya fedha nilizowalipa ni 300K
Kilichokuja kuanza kunitafuna ni uwekaji malumalu, simenti ya plasta, rangi, gypsum board mbao za kufungia hayo magypsum zilini gharimu sana.
.
Hatimae kwenye M10 niliyoipangilia nilikamilisha mjengo wa aina yake, usije thubutu kulinganisha hata siku moja gharama za ujenzi za DSM kwamba ndio ziko kote
.
Kwamba M10 yote inaishia kwenye ununuzi wa tofali si ulofa huo, nakupa maajabu mengine nilivuta hadi maji kwa fedha ile ile pamoja na umeme juu na chenchi ikabakia
Note: kuna baadhi ya vitu sijavitaja na vimo ndani ya 10M
Hata chumba kimoja hujengiM14 si najenga na nahamia