Tunaposema "Mungu Wabariki Wazungu" muwe mnaelewa tunachomaanisha

Emancipate Yourself from Mental Slavery....

Anyway kama unapenda kujisomea tafuta story au angalia hata movie au google kuhusu trojan horses....

At best watu wanatafuta quid pro qou lakini when push comes to shove ni numero uno...
Mental Slavery ni ngumu sana kuisha.
Kwa uthibitisho mdogo ni namna wale waliopewa nafasi serikalini kwa niaba yetu wanavyojipigia pesa hadi mama anatamani kulia. Kama pesa yote inyotolewa kwa ajili ya maendelea ingetumika hata kwa asilimia 75 misaada hii tusingeihitaji. Bado tuna akili za kitumwa tukiwa tumevaa suti.
 
Kwa Ile mihela ya jana no wonder wamachinga wa masoko yote ya mjini na wale wa vijijin waliitana wakakubaliana kila mtu apite mtaani kunadi bidhaa zake
Ili yule mgeni aje atoe hizo ela alafu watajua wanalindanaje
Soma tena ulichoandika
 
Jiwe lazima alaaniwe kwa kutuingiza kwenye hasara kubwa kwenye biashara ya ndege na bwawa la umeme na sgr
 
Chadema haihusiki na ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani
 
No free lunch wakupe wewe Nani upewe bure

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja kwanza , hapa sijakuelewa , nimeweka ya CAG ili kuonyesha uvumilivu wa Wazungu kwa uchafu wetu , yaani pamoja na kwamba ndani yetu wamo panya buku lakini wao hawachoki kutupa chakula .
 
Dah!

Mkuu 'Yoda', nilijua utakuja tu. Mimi nilijizuia mara ya kwanza nilipoona mchango wako wa mwanzo kabisa katika mada hii kuku'quote'. Sasa tupo hapa pamoja.

Hiyo mifano uliyotoa hapo juu ni mizuri sana, ila hitimisho lake haliko sawa.

Hao matajiri "wanajipenda", lakini siyo sahihi kusema kwa vitendo vyao hivyo "wanasambaza upendo wao kwa jamii."

Ngoja hili niliachie hapa.
 
Hakuna hata moja la msingi hapa
1. Sijasema katika andiko lile kwamba yaliyokuwepo 1961 ndiyo tunatakiwa kubaki nayo sisi, tusibadilike kama dunia inavyobadilika. Kubadilika hakuna maana ya kujikabidhi kwa yeyote duniani akuendeshee maisha yako

2. Nilitaka Tanzania isijifiche vichakani kwa kuogopa kuwaudhi hao wanaotununua sasa hivi. Sisi ni taifa na tunao uamzi tunaoona unafaa kutokana na tunachoona kinafaa kwa msimamo wa nchi yetu, siyo kwa mshinikizo wa mataifa mengine.
Hilo swala la uvamizi ni mjadala mwingine ambao pia sikubaliani nawe; wewe unauita uvamizi, mimi ninautambua kama kujihami kwa wanaopigiwa hesabu kwa usalama wao.
Upofu wa akili unaanzia hapo, na kushindwa kujua kuwa dunia inabadilika, siyo kama unavyodhani wewe.

3. Kama unafikiri "Cold War" ilikwisha na sasa tujikabidhi kwa hao wanaojiona wana haki ya kuitawala dunia tena kwa misingi yao, utashangaa sana kama huoni kwamba vita mpya imezuka tena. Bado hutambui kwamba kelele zote hizi za kutuweka mifukoni mwa hao wakubwa ni sehemu ya vita hiyo?

Kwa taarifa yako: Ujamaa haukushindwa, upo leo na utakuwepo siku zote, kote duniani.
 
Hapo ulipo malizia, tupo pamoja. Hivyo tuendelee kuwashukuru wazungu, maana hatuna namna.
EeeenHeeeee!
Kuwashukuru wazungu ni hapo tutakapojitambua sisi wenyewe kuwa nasi ni binaadam wenye akili na utashi, na tunaweza kabisa kuishi maisha yetu bila ya kujiuza ili tupendwe.

Tuchukue hiyo misaada inayotolewa, iwe ni kwa kupendwa au vipi, lakini tuwe na akili ya kuitumia hiyo misaada kujijengea heshima yetu wenyewe.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…