Kama unakumbukumbu vizuri, Hiki suala Kila Mtanzania alilipinga, Mashirika haya yalijaa Undugu , mtoto wa Boss, mtoto wa Mjomba .
Mashirika yalijaza watu wasokua na weledi, watu mambumbu ,watu walisoma Kwa kufelifeli ila chapchap ili mradi wawahi Baba zao ,wajomba zao kwenye shirika Fulani.
Nakumbuka, HAYATI JPM, aliwahi amuru Shirika Fulani, lifute Ajira zote walokua wameshawapa Ndugu zao, na kuamuru mchakato uanzs upya.
Unaturudisha kulekule ambako tumetoka, kule ambako Rushwa ilitamalaki ili upate Ajira huku ukabila na udini ukiendelea .
TAMISEMI nao ndo Hawa!
Watanzania ni wazi, tuna Kila sababu ya Kumuombea na kumshukuru Hatari JPM
Picha iliopo Sasa nikua, yale yote yalikua wakati wa uongozi wa "Msoga" ,ndio yanarudi Sasa.
Hivi Kweli, Baba, JPM , asingejitutumua , tungekua na Daraja la JPM? SGR, ? JNHEPP, MELI MPYA KADHAA, , NDEGE, ELIMU BURE , UPANUZI WA VIWANJA VYA NDEGE., MADARAJA KILA KONA..
Ukweli ni kwamba Kwa stahili hii, kusingekuwepo na hata Moja, kinachofanyika Sasa, ni watu kua na aibu Kwa khogopa he miradi hii ikifeli, itakuaje? Hatutaonekana tumeshindwa?
Mwenye mradi Mpya alouanzisha Samia Kwa miaka yake miwili hii anijuze, naona kama tunajiendea endea.