Tetesi: Tunashukuru kwa Serikali kumalizana kabisa na Mkulima wa ndege

mboni hivyo hasira za nn tena wakati deni limelipwa kupitia ofisi kuu
 
Leta hiyo source ya taarifa yako,pay sheet ya malipo ikiwa na mhuri wa mahakamani. Otherwise hii taarifa yako Niya kupuuza maana haina hoja nzito ya kujitosheleza yeyote zaidi ya Mapambio tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umepata ngapi kwani?
Hata kama ni kweli tumelipa, Immmma, Tundu Lisu& Co. hawakujui na wala hawatakupa hata shilingi, wenzako hela ya uwakili wameingiziwa kwenye akaunti na Muzungu wewe takataka unabakia kupiga mihayo ya ushabiki hapa JF.

Low IQ individual!
 
Ndiyo ubaya wa kurithi ofisi ambayo imejaa uchafu na ya hovyo. Ukirithi ofisi yale mazuri au mabaya ni ya kwako. Pole sana Mhe. Rais wa Awamu ya Tano. Umelipa au utalipa deni ambalo siyo la kwako.
 
That Is obvious, huoni wanaongea tu Mkulima ameshindwa lkn hawasemi ameshindwaje😀
 
Ndiyo ubaya wa kurithi ofisi ambayo imejaa uchafu na ya hovyo. Ukirithi ofisi yale mazuri au mabaya ni ya kwako. Pole sana Mhe. Rais wa Awamu ya Tano. Umelipa au utalipa deni ambalo siyo la kwako.
kwa kweli ,
 
Boss MURUSI Acha Uongo wako, Tutawezaje kumalizana nae kabisa halafu tumpe pesa ya ziada ya kumzuia asiongee na media??? Au asiongelee Kesi yetu na yake???? Kama tumemalizana nae kabisa, huu uoga wa yeye kuliongelea unatoka wapi??? Huyu Mkulima anatia hasira, wangapi wanaidai Jamhuri aka Serikali na hatujakamata mali za Nchi kupitia Mahakama??? !!!


 
Musiba alisema mzungu ni fix,halafu serikali inapiga magoti kumpoza mzungu asibwabwaje huku JF na kwengineko!
Nalog off
 
Hizi speculations zitaendelea kama serikali yetu haitaweka hadharani kilichojiri huko Canada. Sijaona mbwembwe kama tulizoletewa wakati wa kesi ya kule SA, inawezekana ni kweli tumelizwa. Canada wenzetu sheria iko juu ya mtu yeyote tofauti na hapa kwetu Africa.
 
Dawa ya deni ni kulipa sio kuzima simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halina mjadala pasipo kithibitisho? Au ni sababu ndio habari unayoipenda, as if ni makosa ya magu kumdhulumu huyo mzungu, haters mbona mtateseka sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu ,Mazingira tu ya Tukio lenyewe ni Ushahidi tosha wa kilicho wadilishwa hapa。Tulipo mshinda SA tulitangaza hadharani kwa mbwembwe za kutosha.Huko Canada kulikoni kimya ,zaidi tumeambiwa tu Ndege yetu imeachiwa lakini kilicho tokea mpaka iachiwe hakiwekwi wazi ni kwa nini hatujui.

Tuna Haki ya kupata Habari Sahihi na kwa Wakati Mkuu kama Wananchi wa Tanzania ,Kodi zinazo tumika kufanya Nchi hii iwe hivi ilivyo ni za Wananchi hivyo zinafwaa zihojiwe..

Serikali makini haigopi kuhojiwa ,tujibuni tu kwa Hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…