Tunaunga mkono kwa kauli ya RC kurudisha mabasi yote katika stendi ya Magufuli Mbezi

Tunaunga mkono kwa kauli ya RC kurudisha mabasi yote katika stendi ya Magufuli Mbezi

Kama hayawezi kutosha hapo basi kuna Shida ofisi ya RC kuamua jambo bila ya kufanya utafiti.
Kuna shida kwenye siasa , wewe amini hivo uamuzi wa kurudisha mabasi pale ni siasa na trust me utakwama
Johannesburg pamoja na kuwa na stend kubwa ya park station bado kuna vistendi vingi vya mabasi hayo uchochoroni.na maisha yanasonga
 
Utaratibu ni kwamba gari linakaguliwa mwanzo wa safari...Yaani Utembee na gari bovu kuanzia Dar Mbezi hadi Msamvu Moro ndiyo likakaguliwe?
Hivi unafahamu kuwa kuna stend ya Temeke na Mbagala? Kuna ukaguzi wa askari hizo stend?
Kwa mantiki yako mabasi ya Lindi Mtwara Masasi na tunduru hayakaguliwi na ni mabovu.
 
Kuna shida kwenye siasa , wewe amini hivo uamuzi wa kurudisha mabasi pale ni siasa na trust me utakwama
Johannesburg pamoja na kuwa na stend kubwa ya park station bado kuna vistendi vingi vya mabasi hayo uchochoroni.na maisha yanasonga
Kama Magufuli padogo basi wajenge sehemu nyingine ambayo zitaweza kuaccomodate maBUS yote na si solution kuyaweka vichochoroni MITAANI.
 
Hakuna Sehemu yeyote yenye Changamoto ,Kigamboni kuna njia mbili Boti ni 24/7 na Darajani ni 24/7 ,Chamazi Pia ni Mtelezo tena kwa usiku ni Hakuna Foleni ndani ya 1hr ushafika Mbezo Magufuli.

Ukitoka Kigamboni Unapitia Darajani tu unakuja kuibuka Uhasibu ,Unanyoosha Unakuja kuibukia Kijazi Interchange - Unakula Kushoto ukishuka tu MAGUFULI TERMINAL HIYO....Same as Chamazi uwe unatoka Chamazi bamia ,gereji ,maliasili unafika Rangi Tatu hadi Machinjioni Uhasibu -Unakula Kushoto kuitafuta Mandela Road - Kijazi Interchange.
unamaanisha Daladala nazo zinakesha masaa 24?
 
Kama Magufuli padogo basi wajenge sehemu nyingine ambayo zitaweza kuaccomodate maBUS yote na si solution kuyaweka vichochoroni MITAANI.
Stend za mitaani hata majiji makubwa zipo
Stend ya Magufuli haina miaka 10 toka ijengwe leo. Unasema ijengwe nyingine huyo alieyeplan miaka hiyo,hakufikiria kama location ya stend hiyo na ukubwa wake vilikuwa tatizo?
Si bora wangejenga ghorofa pale Ubungo mbona ingetosha
 
Dar kuna Mapori Mengi sana mkuu hayajatumika ,nikiangalia zile stand zao ndogo pale urafiki/shekilango ni vichekesho atleast KIDIA nimeona ana Parking yake sehemu tofauti ndipo anapopaki BUS zake.
 
Nani kakataa stendi isiwe Mbezi?. Stendi iwepo ila mabasi yaruhusiwe kuwa na stendi binafsi za kushushia abiria wa mbali. Kajifunzeni Mwanza wanavyofanya.
Mr Econonist hivi tuna kampuni ngapi za mabasi Tz? Hivi kila kampuni ikiwa na stand yake itakuwaje? Halafu Mr Econonist tujizungunzia mambo ya msongamano au foleni kwenye jiji kama Dar ukilinganisha na mwanzo unadhani changamoto za Mwanza kwenye msongamano ni kama Dar? Mbagala tu kuna changamoto ya msongamano wa watu na vyombo vya usafiri kuliko Mwanza.
 
Shida mmezoea watu kuishi kwa ugumu. Kama basi linaanzia Kigamboni linapitia Mbezi shida ipo wapi?. Yani eneo la watu milioni tano unataka wawe na stendi Moja ya kupandia na kushuka ?. Tuwe serious
Unapojenga au unapopanga zingatia location ya kwenda kwenu..
Huwezi ukaishi chanika halafu ni mwenyeji wa mikoa ya kati ..
Kumbuka abiria anafata basi na sio basi linafata abiria mitaani..
 
Dar kuna Mapori Mengi sana mkuu hayajatumika ,nikiangalia zile stand zao ndogo pale urafiki/shekilango ni vichekesho atleast KIDIA nimeona ana Parking yake sehemu tofauti ndipo anapopaki BUS zake.
Stend ilikuwa Ubungo na design ilitakiwa ifanywe pale pale Ubungo , wangejenga hata two storey building
Haya yanayotokea leo yasingetokea
Kukosea kwenye mipango ya serikali saa nyingine ni mipango maalum ya watu kujipigia pesa za serikali
 
Unapojenga au unapopanga zingatia location ya kwenda kwenu..
Huwezi ukaishi chanika halafu ni mwenyeji wa mikoa ya kati ..
Kumbuka abiria anafata basi na sio basi linafata abiria mitaani..
Mimi nimepangiwa na Serikali kufundisha shule Chanika na ni mwenyeji wa Mwanza. Nifanyaje?
 
Kama ndio ivyo basi stendi irudi KISUTU. Mbezi mbali.
Kazi ni kipimo cha utu
Kama walitaka Dar iwe na stendi moja tu hapo Posta ndipo ilitakiwa ijengwe hapo. Ila kupeleka stendi nje ya mji kwenye kona moja ya mji halafu watu wasafiri km 50 kuifuata ni upuuzi wa kiwango cha lami.
 
Kama ndio ivyo basi stendi irudi KISUTU. Mbezi mbali.
Kazi ni kipimo cha utu
For sure
Hata hao wakoloninkipindi wanapanga dar hawakuweka stend moja
Kisutu iliserve basi za kaskazin, mnazi mmoja ilihudumia basi za kusini, Mbagala basi za Mtwara Masasi na Tunduru
Leo hii kuilazimisha basi za mikoa yote zihamie mbezi ni kama haitawezekana
 
Back
Top Bottom