Suala la China kukopesha fedha nyingi Sri Lanka kwa mikopo mibaya isiyolipika ni fact, na limesemwa na watu wengi.
BBC haikusababisha China kuikopesha Sri Lnka hela nyingi kwa mikopo isiyolipika.
Na hicho ndicho alichojibu mwanasiasa huyo wa Sri Lanka, kwamba wanasiasa wa Sri Lanka wamefanya maamuzi mabaya, hilo halikwepeki.
Huko nje hata kama kuna mbinu za ku undermine Sri Lanka, hiyo ni fact ya dunia tu, ni geopolitics.
Kinachotakiwa ni Sri Lanka kuwa na wanasiasa wanaojua kuitetea nchi yao, na si kuacha nchi yao inateketea kiuchumi huku wao wakivimbisha matumbo yao, halafu wakifurushwa, walalamike kuna mabeberu huko nje.
Yani, ni kama vile unajua huu uwanja una miba na mbigiri nyingi, halafu unao uamuzi wa kuvaa viatu, halafu unakataa kuvaa viatu. Halafu ukichomwa na miba, unalalamika uwanja una miba mingi.
Uwanja kuwa na miba ni fact, wewe umejilinda vipi na hiyo miba? Kwa nini miba ikuchome wewe na si jirani yako?