Tunavyosema mkataba una dosari muelewe, oneni ufafanuzi wa CCM hapa na ndio wamesema wanaelimisha watu

CCM yenyewe inajimaliza yenyewe sasa. Ipo mikononi mwa watu wasotaka hata kuisikia ikitamkwa maisha yao yote. Leo CCM uwakabidhi kina Jussa unategemea nini?
 
Why don't GTs like me and others think that, you Mr. Pascal Mayalla is actually a really mburula at the same time mburumatata whom you sometimes (not always) bring on the table uncomprehensible materials?
Duh...!.
Duh...!.
Naheshimu mawazo yako
P
 
Pascal mzee wangu unatatizo sehemu, km sio ulevi basi ni uzee.
Tangu lini makubaliano mabovu yakaleta mkataba mzuri?
Mbona mnajitoa ufahamu kiasi hiki?
Huyu jamaa sio mzee, labda kuna mahali amepata kabahasha, anatafuta uteuzi au uchawa tu.
 
Huyo atakuwa Mjema. Hivi Maza alimuokota wapi huyo Mwanamama. Bora ya Nape na for 4 ya ya point 29.
 
Mkuu Pascal, katika IGA kuna ahadi on both parties ya kutimiza mambo fulani in the future. Ahadi hizo ni executory consideration. Na zisipotimizwa kuna legal consequences.

Amandla...
 
as many as it takes!, kila project ina HGA yake, to start with ni HGA moja ya berth 1-7, wakipewa kitu kingine chochote, kina HGA yake.
P
Ok umejibu vizuri..IGA haitaji wala ku limit idadi za HGA. Maana yake HGA ni kwamba HGA zinaweza kuwa nyingi with different time intervals. Unaweza kuwa na project ya 25 years, ukiwa mwaka wa 20 ukaingia nyingine ya 15 years..ukiwa mwaka 30 ukaingia nyimgine ya 20..etc.. endlessly. So IGA haina ukomo.
 
Mkuu Pascal, katika IGA kuna ahadi on both parties ya kutimiza mambo fulani in the future. Ahadi hizo ni executory consideration. Na zisipotimizwa kuna legal consequences.

Amandla...
Nakubaliana na wewe, ila lets get to the drawing board ya hii IGA, Watanzania waelimishwe IGA ni nini na ni ya kazi gani,
IGA ni barua ya posa kwa DPW kuiposa Bandari yetu!.

Mambo yalianza zamani mwezi February 2022 wakati wa Expo Dubai, kijana shababi Mwarabu wa Dubai, kamuona binti Bandari ya Dar es Salaam, kampenda. Akamwalika Mzazi wa binti kutembelea Dubai wakati wa Expo Dubai, ndipo kijana shababi DPW akatangaza nia ya kumposa binti Bandari Dare Salaama. Nia njema, MoU kati ya Bandari na DPW ikasainiwa Dubai huku mzazi akishuhudia, MoU hiyo ni kumruhusu shababi DPW kuleta barua ya posa.

October 2022 shababi DPW katua nchini na mshenga wake kuleta barua ya posa, IGA.

Mzazi wa binti ni Mama Samia, akamruhusu mjomba mtu Prof. Mbarawa kuipokea barua hiyo ya posa, Mbarawa akaanguka saini yake barua ya posa ikapokelewa ile October 2022.

Mzazi wa binti Bandari, mamie mwali akaipeleka barua hiyo ya posa kwenye kikao cha wanafamia, kuomba ridhaa ya wanafamilia kuridhia barua ya posa ikubaliwe binti Bandari aposwe na Mwarabu wa Dubai. Kikao cha familia, kikaridhia, ndio kile kikao cha Bunge kuridhia IGA.

Baada ya posa kukubaliwa sasa ndio anapangiwa mahari. At this stage IGA ni makubaliano tuu ya kukubali kupokea barua ya posa lakini mahari haijapangwa, haijalipwa!.

Tunaweza kuikata hii IGA na hakuna any legal implications!. Ila baada ya kukubalina mahari, HGA, na shababi DPW akakubali, that is a contract, ikitokea tuka ghairi, hawa jamaa watatushitaki for a legitimate expectations.
IGA ni makubaliano tuu, hauna any legal consequences, HGA ndio mkataba rasmi wenye legal implications.
P
 
You are absolutely right, ila kila HGA itakuwa na ukomo wake.
P
 
Yes CCM wanasema kweli, na huu ndio uelimishaji umma wenyewe kuhusu hii IGA. IGA sio mkataba, ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA bado, utakuwa ni mkataba mzuri.
P
Makubaliano yetu ni kwamba, utanipa nyumba zako nizitumie bure. Kama itatatokea una nyumba nyingine hautaruhusiwa kumpangisha yeyote, utatakiwa uniulize mimi kwanza kama na hiyo nitaihitaji nitumie bure.
Makubaliano yetu ni kwamba hakutakuwa na ukomo wa lini makubaliano yetu yata expire, pia hakuna kiwango cha hela ambacho wewe utapokea.
Hivi, unaweza ukaenda nyumbani kwako na Makubaliano ya aina hii kweli? Halafu ukaanza kuiambia familia yako kuwa mali zenu zimepata muwekezaji?
Mstari wa Makubaliano na Mkataba unachorwa wapi? Si ni signature tu ya kuyatambua hayo makubaliano.
Swali ni je, hayo makubaliano yenyewe jinsi yalivyo yana hadhi ya kubebwa na mtu mwenye akiki timamu kwamba anaenda kuyajadili na kuyafikiria? Just be fair.
 
Wanaotetea kwamba mkataba bado hayo ni makubaliano tu ni Wajinga, eleweni kwamba HGA ndio hutokana na IGA. Kama IGA mbovu kwa vyovyote vile HGA ni lazima iwe Mbovu tu. Kikubwa futeni kabisa hili dude.
 
Nakuuliza tena kwa namna nyingine; Familia inajadili POSA au MAHALI?
 
Acha porojo mzee, HGA zitakazotungwa zitabebwa na IGA hasa kutakapotokea disputes, ndo maana IGA ina legaly binding clauses, pia IGA ni mkataba wa milele na hicho unachosema ukomo wa HGA ni changa la macho, bahasha nono zimewafanya watu kuweka nchi rehani.
 
Unakosea tena Pascal. Hayo unayoita makubaliano ni MoU ambayo kweli sio commitment. Unataka kutuambia kuwa hakutakuwa na legal consequeces kama tutaamua kumpa kampuni nyingine kuendeleza maeneo yaliyoainishwa katika Appendix 1 kuwa yataendelezwa na DPW? HGAs ni mikataba ya utekelezaji ya yale yaliyoainishwa katika IGA. Majukumu ya serikali ya JMT kwa DPW ( na vilevile ya DPW kwa serikali ya JMT)yameainishwa kwenye IGA. Mambo kama ajira, kodi, access kwa ardhi n.k. yote yamo kwenye IGA na HGA yeyote ni lazima iendane nayo.
Mbona Pascal unataka kuwachuuza wenzako? Hayo mambo ya posa hayaendani na hili suala.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…