Uchaguzi 2020 Tundu A.M. Lissu: Mgombea Urais wa upinzani machachari zaidi kuwahi kutokea katika chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi kurudi 1992

Lissu amewabananisha kwenye kona ya kitanda hadi imefika hatua wanaccm na mavitambi yenu mnavamia vyombo vichafu vya wapiga kura na kulazimisha kuviosha ili mpigiwe kura [emoji1787]
Baada ya oktoba utaelewwa
 
Huyu TAL ndiye presidential material katika uchaguzi huu kulioko mgombea yeyote. Namuombea kwa Mwenyezi Mungu amuondolee mazonge yote katika njia yake ya kuelekea Ikulu
 
Ogopa sana spana za huyu mtu anayeitwa Tundu Lissu zimewaingia CCM hadi imefikia hatua mgombea wa CCM na polepole na meza kuu wanawapigia wananchi magoti na kuwaomba kura 🤣

Dogo hiyo ni sanaa tuu, Maeneo ya Njombe unapoomba kitu kwa uaminifu na anaeombwa ni vigumu kukunyima ni kuomba kwa kupiga magoti. Uliza watu wa Njombe humu wakujuze. Wanasiasa Sanaa.
 
Mwanasiasa mmoja hata awe mzuri kiasi gani, hawezi kuleta mabadiliko katika li nchi kubwa kama Tanzania.

Wanatakiwa wawepo kina Lissu wengi na karibu kila sehemu ili anayotamka kubadilika yatokee.

Tuendako atapotea kwa kuwa atapoteza jukwaa baada ya uchaguzi na platforms za kuzungumzia zitakua chache sana.

Kwa generation ya elected leaders wa CCM watakao kuja bungeni patawaka moto.

Angekuwa na impact kubwa sana kama angechagua topics mbili au tatu na akasimamia hizo hizo kama alivyokuwa Dr. Slaa kuhusu Ufisadi. Vinginevyo akiwa generality politician atashindwa kusimamia anachokitaka kupandikiza kwa Watanzania.

..uzuri wa TL ni kwamba anapozungumzia suala lolote lile anakuwa amelichimba mpaka historia yake.

..kwa mfano, jana alikuwa anazungumza na wananchi wa Serengeti, basi alianza na historia ya hifadhi hiyo, akaja mpaka kuzungumzia tafiti mbalimbali zilizofanyika kuhusu uhifadhi, na baadhi ya njia mbadala zinazopendekezwa kuhusu masuala ya uhifadhi.

..sasa uzuri ni kwamba alifanya yote hayo akitumia lugha rahisi inayoeleweka na wananchi wa kawaida. Na pia TL huwa na mazungumzo na wananchi, tofauti na wanasiasa wanaohutubia wananchi.

..Hiki ni kipaji ambacho nimegundua wanasiasa wengi hapa Tanzania hawanacho. Kingine kinachombeba Tundu Lissu ni REKODI yake ya miaka mingi kutetea wananchi wanyonge.
 
Kuna kitu ambacho lazima ukifahamu vizuri, Law is politics. kwa hiyo manasheria mzuri ni rahisi sana kuwa mwanasiasa mzuri.

Jee umewahi kujiuliza kwa nini asilimia karibu 90 ya politicians ni ama Lawyers ama waliochukua Humanities na wala sio Scientists ?

Lakini kwa kutatua tatizo Scientists ni wazuri sana kuliko Lawyers au waliochuku Humanities. Lakini pia wapo ambao wana vipaji vya kutatatua matatatizo. Lakini wengi wao wana lack ability to coherently organise people (leadership).

Kwa kuwa Political (election) campaigns zina endelea , tuta pata muda wa kutosha kuvumbua vipaji vingi sana katika siasa.
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
Kwa kutumia MAHERA inawezekana
 
Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995, Tanzania haijawahi kushuhudia na kupata mgombea wa upinzani machachari na mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo mbalinbali kitaifa na kimataifa katika nyanja za elimu, siasa, historia, sheria, uchumi nk kama Tundu Lissu (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020...!

Kina Mrema (1995), Lipumba (2000), Freeman Mbowe na Lipumba (2005), Dr Slaa (2010) na Lowassa (2015) walikuwa wagombea Urais wenye sifa zao za kipekee, lakini Tundu Lissu anawazidi wote kwa kuwa na sifa za ziada na kufanya upekee wake uwe maalumu kama nitakavyojaribu kueleza hapa chini...

Naandika thread hii baada ya kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mgombea Urais huyu kwa tiketi ya CHADEMA ya jana tarehe 28/9/2020 akiwa Mugumu - Serengeti mkoa wa Mara....

Ni hotuba ambayo imajaa elimu ya uraia na sheria huku ikifunua UJINGA na UPUMBAVU wa viongozi wengi wa serikali ya CCM ya Magufuli wasiojua sheria, kanuni na taratibu za kusimamia dhamana zao za uongozi kwa ajili ya ustawi wa jamii na amani yetu....

RCO ya Mara, DC na DED wa Serengeti ni mfano mzuri wa viongozi wajinga na wapumbavu. Wapewa dhamana ya uongozi wa mamilioni ya watu, lakini kwa kutojua ama kwa makusudi wao ndiyo wanakuwa wavunjaji wakubwa wa sheria na taratibu....

Ukiacha hili, upekee wa Tundu Lissu ukilinganisha na wagombea wote wa upinzani waliowahi kugombea Urais tangu mwaka 1995 unajitokeza katika maeneo haya;

1. UFAHAMU MKUBWA WA MAMBO:

Huyu bwana amejaliwa kuwa na ufahamu wa hali ya juu wa mambo mengi kuanzia ktk nyanja ya historia, uchumi, jamii, siasa, sheria na utamaduni...

Hii humwongezea ujasiri wa kusimama na kutetea chochote kinachokuja mbele yake na mara zote anakuwa mshindi tu. Hii inatuleta kwenye sifa ya pili...

2. UJASIRI:

Kwa kuwa kajaliwa kuwa na ufahamu mpana wa mambo mbali ya kitaifa na kimataifa karibu katika nyanja zote za maisha, hii imempa hiki kitu kingine yaani - UJASIRI...

Naye sasa anatumia kila njia ku - influence tabia hii ya ujasiri, kutokuwa na hofu ama woga kwa watu wote anaokutana nao. Hapa ndipo hasa ulipo mgogoro wake na watawala. Hili huwatia hofu na woga mkubwa watawala hawa waovu....

Wanajua kuwa watu wakielimishwa, wakatambua WAJIBU na HAKI zao, wataiondoa serikali hii madarakani kufumba tu na kufumbua. Hili linaiogopesha sana CCM na serikali wanayoingoza....

3. NI MSOMAJI SANA WA VITABU HUYU JAMAA:

Ili kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali, sharti utafute maarifa. Sharti usome vitabu na vyanzo vingine mbalimbali vya maarifa...

Huyu ndugu anasoma sana. Simjui na wala sijawahi kukutana naye uso kwa uso karibu. Lakini ninapomtazama kwenye TV akiongea, mtu mdadisi atatumbua hili moja kwa moja...

Ukisikiliza na kutazama hotuba yake ya jana Serengeti utaelewa nikisemacho hapa. Utaelewa kuwa huyu mtu amejaza maarifa kichwani mwake na si matope kama alivyo Polepole ama Cyprian Musiba wa CCM.....

4. NI MGOMBEA PEKEE KATI YA WOTE ALIYETOA UHAI WAKE KWA AJILI YA HAKI ZA WENGI:

Hii ni sifa very exceptional. Huyu bwana amepitia njia ngumu mno hadi kufikia hatua hii aliyonayo hapo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa taifa hili zuri la Tanzania...

Huyu ndugu kwa siku saba achilia mbali miaka miwili na ushee akiuguza majeraha ya risasi kitandani, alikuwa kuzimu. Alionja KIFO na MAUTI lakini kwa sababu anazojua Mungu mwenyewe, alimfufua tena Tundu Lissu. Yuko hai na ndiye huyu ambaye watu wanamuona kama Messiah wao na basically ndivyo ilivyo, ndivyo itakavyokuwa....

5. NI SPEECH GIVER & INFLUENCER MZURI KUPINDUKIA. HUCHOKI KUMSIKILIZA..!!

Wanasiasa wenye kipaji cha namna hii ni wachache mno Tanzania. Huko nje namfahamu mtu mmoja, Martin Luther King Jr, mpigania haki za weusi wa Marekani miaka ile...

Hotuba za Tundu Lissu ni za kushawishi, kuhamasisha, kutia morali na kuwaondolea watu hofu, mashaka na woga....

Watu kama hawa siku zote ni HATARI katika serikali zote za kidikteta zinazogandamiza UHURU na HAKI za kiraia...

Huwindwa kama wanyama pori ili kuwaua kama njia pekee ya kuwaondoa maana HOJA ZAO mara zote hazijibiki na Mara zote ni chungu na zinachoma mithili ya mkuki moyoni...

Mara zote watu wa aina hii hugeuziwa kibao na kuitwa wachochezi, wahamasisha vurugu na wahatarisha amani. Hutungiwa hata sheria kwa ajili yao tu...

Hii yote, kosa lao ni moja tu. Kufumbua macho, akili na ufahamu wa watu wa kutambua WAJIBU na HAKI zao dhidi ya serikali na viongozi wao....!!

Huyu ndugu kwa hakika ni TUNU YA TAIFA hili. Ni machachari and very unique. Nitampa kura yangu mimi na familia na jamaa na rafiki zangu wote....
Ukweli mtupu .
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
Nyomi lile mnang'oka...mkiiba kura Lissu anauwezo wa kuhamasisha watu waingie road..polisi watavua magwanda tutawachapa nyie Mataga na makalio yenu makubwa kama Bashite
 
Umeandika uchambuzi mzuri sana; binafsi nimejikuta napata hamu kumuona Lissu akiendelea kuwa mgombea Urais hata 2025 and beyond if possible, ni mwalimu, mshauri, mtetezi, na sifa nyingine nyingi tu.

Ni matumaini yangu atashinda this year, then ataendekea kuwa Rais mpaka 2030, muda wake wa vipindi viwili utakapokwisha.
 
Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995, Tanzania haijawahi kushuhudia na kupata mgombea wa upinzani machachari na mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo mbalinbali kitaifa na kimataifa katika nyanja za elimu, siasa, historia, sheria, uchumi nk kama Tundu Lissu (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020...!

Kina Mrema (1995), Lipumba (2000), Freeman Mbowe na Lipumba (2005), Dr Slaa (2010) na Lowassa (2015) walikuwa wagombea Urais wenye sifa zao za kipekee, lakini Tundu Lissu anawazidi wote kwa kuwa na sifa za ziada na kufanya upekee wake uwe maalumu kama nitakavyojaribu kueleza hapa chini...

Naandika thread hii baada ya kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mgombea Urais huyu kwa tiketi ya CHADEMA ya jana tarehe 28/9/2020 akiwa Mugumu - Serengeti mkoa wa Mara....

Ni hotuba ambayo imajaa elimu ya uraia na sheria huku ikifunua UJINGA na UPUMBAVU wa viongozi wengi wa serikali ya CCM ya Magufuli wasiojua sheria, kanuni na taratibu za kusimamia dhamana zao za uongozi kwa ajili ya ustawi wa jamii na amani yetu....

RCO ya Mara, DC na DED wa Serengeti ni mfano mzuri wa viongozi wajinga na wapumbavu. Wapewa dhamana ya uongozi wa mamilioni ya watu, lakini kwa kutojua ama kwa makusudi wao ndiyo wanakuwa wavunjaji wakubwa wa sheria na taratibu....

Ukiacha hili, upekee wa Tundu Lissu ukilinganisha na wagombea wote wa upinzani waliowahi kugombea Urais tangu mwaka 1995 unajitokeza katika maeneo haya;

1. UFAHAMU MKUBWA WA MAMBO:

Huyu bwana amejaliwa kuwa na ufahamu wa hali ya juu wa mambo mengi kuanzia ktk nyanja ya historia, uchumi, jamii, siasa, sheria na utamaduni...

Hii humwongezea ujasiri wa kusimama na kutetea chochote kinachokuja mbele yake na mara zote anakuwa mshindi tu. Hii inatuleta kwenye sifa ya pili...

2. UJASIRI:

Kwa kuwa kajaliwa kuwa na ufahamu mpana wa mambo mbali ya kitaifa na kimataifa karibu katika nyanja zote za maisha, hii imempa hiki kitu kingine yaani - UJASIRI...

Naye sasa anatumia kila njia ku - influence tabia hii ya ujasiri, kutokuwa na hofu ama woga kwa watu wote anaokutana nao. Hapa ndipo hasa ulipo mgogoro wake na watawala. Hili huwatia hofu na woga mkubwa watawala hawa waovu....

Wanajua kuwa watu wakielimishwa, wakatambua WAJIBU na HAKI zao, wataiondoa serikali hii madarakani kufumba tu na kufumbua. Hili linaiogopesha sana CCM na serikali wanayoingoza....

3. NI MSOMAJI SANA WA VITABU HUYU JAMAA:

Ili kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali, sharti utafute maarifa. Sharti usome vitabu na vyanzo vingine mbalimbali vya maarifa...

Huyu ndugu anasoma sana. Simjui na wala sijawahi kukutana naye uso kwa uso karibu. Lakini ninapomtazama kwenye TV akiongea, mtu mdadisi atatumbua hili moja kwa moja...

Ukisikiliza na kutazama hotuba yake ya jana Serengeti utaelewa nikisemacho hapa. Utaelewa kuwa huyu mtu amejaza maarifa kichwani mwake na si matope kama alivyo Polepole ama Cyprian Musiba wa CCM.....

4. NI MGOMBEA PEKEE KATI YA WOTE ALIYETOA UHAI WAKE KWA AJILI YA HAKI ZA WENGI:

Hii ni sifa very exceptional. Huyu bwana amepitia njia ngumu mno hadi kufikia hatua hii aliyonayo hapo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa taifa hili zuri la Tanzania...

Huyu ndugu kwa siku saba achilia mbali miaka miwili na ushee akiuguza majeraha ya risasi kitandani, alikuwa kuzimu. Alionja KIFO na MAUTI lakini kwa sababu anazojua Mungu mwenyewe, alimfufua tena Tundu Lissu. Yuko hai na ndiye huyu ambaye watu wanamuona kama Messiah wao na basically ndivyo ilivyo, ndivyo itakavyokuwa....

5. NI SPEECH GIVER & INFLUENCER MZURI KUPINDUKIA. HUCHOKI KUMSIKILIZA..!!

Wanasiasa wenye kipaji cha namna hii ni wachache mno Tanzania. Huko nje namfahamu mtu mmoja, Martin Luther King Jr, mpigania haki za weusi wa Marekani miaka ile...

Hotuba za Tundu Lissu ni za kushawishi, kuhamasisha, kutia morali na kuwaondolea watu hofu, mashaka na woga....

Watu kama hawa siku zote ni HATARI katika serikali zote za kidikteta zinazogandamiza UHURU na HAKI za kiraia...

Huwindwa kama wanyama pori ili kuwaua kama njia pekee ya kuwaondoa maana HOJA ZAO mara zote hazijibiki na Mara zote ni chungu na zinachoma mithili ya mkuki moyoni...

Mara zote watu wa aina hii hugeuziwa kibao na kuitwa wachochezi, wahamasisha vurugu na wahatarisha amani. Hutungiwa hata sheria kwa ajili yao tu...

Hii yote, kosa lao ni moja tu. Kufumbua macho, akili na ufahamu wa watu wa kutambua WAJIBU na HAKI zao dhidi ya serikali na viongozi wao....!!

Huyu ndugu kwa hakika ni TUNU YA TAIFA hili. Ni machachari and very unique. Nitampa kura yangu mimi na familia na jamaa na rafiki zangu wote....
Hana lolote, zaidi ya matusi na jazba. Baada ya slaa kuondoka, chama saccos kwisha kabisa. Mnapoteza muda kuzunguka nchi nzima, huku mkijua hamuwezi shinda.
 
Mwanasiasa mmoja hata awe mzuri kiasi gani, hawezi kuleta mabadiliko katika li nchi kubwa kama Tanzania.

Wanatakiwa wawepo kina Lissu wengi na karibu kila sehemu ili anayotamka kubadilika yatokee.

Tuendako atapotea kwa kuwa atapoteza jukwaa baada ya uchaguzi na platforms za kuzungumzia zitakua chache sana.

Kwa generation ya elected leaders wa CCM watakao kuja bungeni patawaka moto.

Angekuwa na impact kubwa sana kama angechagua topics mbili au tatu na akasimamia hizo hizo kama alivyokuwa Dr. Slaa kuhusu Ufisadi. Vinginevyo akiwa generality politician atashindwa kusimamia anachokitaka kupandikiza kwa Watanzania.
Kwani kina Martin Luther walikuwepo wangapi?

Nyie magamba siku zote mna hoja za ajabu ajabu sana...

Unazungumzia kizazi kipya cha wabunge wa CCM bungeni kuja na hoja motomoto, chini ya bunge hili la Ndugai?! wewe kweli hujielewi.

Topic mbili au tatu kwa Lissu za nini? yule akili kubwa, anabeba topic nyingi na zote anazichambua wasikilizaji wake tunamuelewa vizuri kabisa na hamu ya kumsikiliza haiishi, wewe na kichwa chako cha lumumba beba hiyo moja uende nayo popote utakako.
 
Jipe muda kuelewa na kutofautisha utawala wa kimajimbo na wa kikabila. Utawala wa majimbo haina maana kuwarudisha watu katika maeneo asili ya makabila yao bali ni kuwapa wananchi katika maeneo yao wanayoishi fursa na nguvu zaidi ya kufanya maamuzi juu utawala,rasilimali na kodi katika maeneo wanayoishi bila kujali kabila la mtu.
Mkuu nitafurahi kama tutakuwa na uchambuzi bila ushabiki ili kila mmoja wetu atajirike na mwenzake, na sio vinginevyo. Sisi watu wa mjini tumekwisha piga kura myoyoni kwetu itakapo fika tarehe 28th, October tutatumbukiza kura tuu, kwa hiyo michango ituelimishe.

Mimi ninajitahidi sana ninapokuwa na muda kufuatilia kwa undani kinacho endelea na philosophy ya Mwanasiasa. Lissu anaweza kuelezea jambo kwa upana bila philosophy yake, kitu ambacho kwa kufananisha, Dr. Slaa alikuwa mzuri sana.
Mfano: Suala la majimbo kuna maeneo ambayo jamii haina intergration kubwa hilo swala watalikubali kirahisi, lakini sehemu yeyote ambayo jamii imekuwa na intergration ya juu na mikoa na jamii nyingine, suala la majimbo linakuwa mtihani.

Mfano, suala la majimbo mkoa wa kilimanjaro itabidi ufanye kazi ya ziada wananchi walikubali, japo utekelezaji uko tofauti na wanavyo dhani, na sababu ni jamii ya Kilimanjaro imetawanyika sana karibu nchi nzima na wakirudi Kilimanjaro hawatotosha.

Nitakupa mfano mwingine wa mawasiliano ambao watu wengi ambao hawajui umuhimu wa kuconnect message yako kwa walengwa wana shangaa sana Magafuli anavyo fanya kampeni zake.

Kwa muono wa kawaida Magufuli ni mshamba: Lakini sisi binadamu tuna taabu sana.
Mfano kwetu Upareni, ukichonga kiswahili na kikanyooka wazee watakwambia huyu ni Mnyika na mswahili. Maana yake halisi ni mtoka mbali kwa hiyo wanatakiwa kujihadhari na wewe. kiswahili kikikupa taabu kidogo, yaani hakikunyooka, wao ni rahisi kukuamini. Mwenye kunyoosha kiswahili anaitwa Mswahili- maana kamili ni mtu wa kuchukulia tahadhari nae.

Tusishangae Magufuli ambae sisi tuna muona mshamba, kwa watu wa mikoani inawezekana wanamuani zaidi kwa kuwa wanamuona ni mshamba mwenzao kwa kusindwa kunyoosha kiswahili, kwa hiyo wanaona hawadanganyi.

kila Mwanasiasa lazima achomeke uongo japo kidogo anapotaka kunogesha ujumbe anao uwakilisha.
 
Hakuna tatizo watu kuchagua watu kwa vigezo vya Mswahili,mnyika au mshamba.Hiyo ndio demokrasia na wakati mwingine ina gharama chungu sana ukiwa na taifa lenye wajinga wengi,jambo la muhimu ni uwanja sawa wa kisiasa wenye kutoa fursa ya uchaguzi huru na wa haki na ionekane hivyo.
Mkuu nitafurahi kama tutakuwa na uchambuzi bila ushabiki ili kila mmoja wetu atajirike na mwenzake, na sio vinginevyo. Sisi watu wa mjini tumekwisha piga kura myoyoni kwetu itakapo fika tarehe 28th, October tutatumbukiza kura tuu, kwa hiyo michango ituelimishe.

Mimi ninajitahidi sana ninapokuwa na muda kufuatilia kwa undani kinacho endelea na philosophy ya Mwanasiasa. Lissu anaweza kuelezea jambo kwa upana bila philosophy yake, kitu ambacho kwa kufananisha, Dr. Slaa alikuwa mzuri sana.
Mfano: Suala la majimbo kuna maeneo ambayo jamii haina intergration kubwa hilo swala watalikubali kirahisi, lakini sehemu yeyote ambayo jamii imekuwa na intergration ya juu na mikoa na jamii nyingine, suala la majimbo linakuwa mtihani.

Mfano, suala la majimbo mkoa wa kilimanjaro itabidi ufanye kazi ya ziada wananchi walikubali, japo utekelezaji uko tofauti na wanavyo dhani, na sababu ni jamii ya Kilimanjaro imetawanyika sana karibu nchi nzima na wakirudi Kilimanjaro hawatotosha.

Nitakupa mfano mwingine wa mawasiliano ambao watu wengi ambao hawajui umuhimu wa kuconnect message yako kwa walengwa wana shangaa sana Magafuli anavyo fanya kampeni zake.

Kwa muono wa kawaida Magufuli ni mshamba: Lakini sisi binadamu tuna taabu sana.
Mfano kwetu Upareni, ukichonga kiswahili na kikanyooka wazee watakwambia huyu ni Mnyika na mswahili. Maana yake halisi ni mtoka mbali kwa hiyo wanatakiwa kujihadhari na wewe. kiswahili kikikupa taabu kidogo, yaani hakikunyooka, wao ni rahisi kukuamini. Mwenye kunyoosha kiswahili anaitwa Mswahili- maana kamili ni mtu wa kuchukulia tahadhari nae.

Tusishangae Magufuli ambae sisi tuna muona mshamba, kwa watu wa mikoani inawezekana wanamuani zaidi kwa kuwa wanamuona ni mshamba mwenzao kwa kusindwa kunyoosha kiswahili, kwa hiyo wanaona hawadanganyi.

kila Mwanasiasa lazima achomeke uongo japo kidogo anapotaka kunogesha ujumbe anao uwakilisha.
 
Mwanasiasa mmoja hata awe mzuri kiasi gani, hawezi kuleta mabadiliko katika li nchi kubwa kama Tanzania.

Wanatakiwa wawepo kina Lissu wengi na karibu kila sehemu ili anayotamka kubadilika yatokee.

Tuendako atapotea kwa kuwa atapoteza jukwaa baada ya uchaguzi na platforms za kuzungumzia zitakua chache sana.

Kwa generation ya elected leaders wa CCM watakao kuja bungeni patawaka moto.

Angekuwa na impact kubwa sana kama angechagua topics mbili au tatu na akasimamia hizo hizo kama alivyokuwa Dr. Slaa kuhusu Ufisadi. Vinginevyo akiwa generality politician atashindwa kusimamia anachokitaka kupandikiza kwa Watanzania.

1. Wewe unasema ishu ya kuchagua "topic" mbili ama tatu tu ili aende nazo kwa wananchi kuombea kura, au siyo?...

Mimi nakuambia hivi, "topic" hizo tatu ni nyingi mno na zinaingia katika agenda kuu ya UHURU, HAKI na MAENDELEO YA WATU...

Ndiyo sasa kusema kuwa, Tundu Lissu anasimamia na amebeba agenda (siyo topic) moja tu ambayo ni UHURU, HAKI na MAENDELEO YA WATU...

2. Ni kweli, mtu mmoja hata akiwa mzuri kiasi gani hataweza kuleta mabadiliko ya uzuri katika jamii yoyote bali mpaka wawepo kadhaa kama yeye...

Ndicho kinachofanyika sasa. Anafundisha, hamasisha, kutia morali na kuelekeza ili watu wajue na kutambua WAJIBU na HAKI zao za kiraia...

Hiki ndicho kunachopingwa na kujaribu kuzuiwa na watawala kwa hila na kwa nguvu zote....!!
 
Ongezea na hii: ....mgombea urais aliyekuja na nuksi ya kuambulia wabunge 4 tu kwa chama chake na kupata kura kiduchu kuwahi kutokea single digit 7% ya kura za urais!
Mahaba
 
Sasa huu ni ushabiki wa kisiasa unaokupelekea kuukataa ukweli.
 
Back
Top Bottom