Tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza wa mwaka 1995, Tanzania haijawahi kushuhudia na kupata mgombea wa upinzani machachari na mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo mbalinbali kitaifa na kimataifa katika nyanja za elimu, siasa, historia, sheria, uchumi nk kama Tundu Lissu (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020...!
Kina Mrema (1995), Lipumba (2000), Freeman Mbowe na Lipumba (2005), Dr Slaa (2010) na Lowassa (2015) walikuwa wagombea Urais wenye sifa zao za kipekee, lakini Tundu Lissu anawazidi wote kwa kuwa na sifa za ziada na kufanya upekee wake uwe maalumu kama nitakavyojaribu kueleza hapa chini...
Naandika thread hii baada ya kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mgombea Urais huyu kwa tiketi ya CHADEMA ya jana tarehe 28/9/2020 akiwa Mugumu - Serengeti mkoa wa Mara....
Ni hotuba ambayo imajaa elimu ya uraia na sheria huku ikifunua UJINGA na UPUMBAVU wa viongozi wengi wa serikali ya CCM ya Magufuli wasiojua sheria, kanuni na taratibu za kusimamia dhamana zao za uongozi kwa ajili ya ustawi wa jamii na amani yetu....
RCO ya Mara, DC na DED wa Serengeti ni mfano mzuri wa viongozi wajinga na wapumbavu. Wapewa dhamana ya uongozi wa mamilioni ya watu, lakini kwa kutojua ama kwa makusudi wao ndiyo wanakuwa wavunjaji wakubwa wa sheria na taratibu....
Ukiacha hili, upekee wa Tundu Lissu ukilinganisha na wagombea wote wa upinzani waliowahi kugombea Urais tangu mwaka 1995 unajitokeza katika maeneo haya;
1. UFAHAMU MKUBWA WA MAMBO:
Huyu bwana amejaliwa kuwa na ufahamu wa hali ya juu wa mambo mengi kuanzia ktk nyanja ya historia, uchumi, jamii, siasa, sheria na utamaduni...
Hii humwongezea ujasiri wa kusimama na kutetea chochote kinachokuja mbele yake na mara zote anakuwa mshindi tu. Hii inatuleta kwenye sifa ya pili...
2. UJASIRI:
Kwa kuwa kajaliwa kuwa na ufahamu mpana wa mambo mbali ya kitaifa na kimataifa karibu katika nyanja zote za maisha, hii imempa hiki kitu kingine yaani - UJASIRI...
Naye sasa anatumia kila njia ku - influence tabia hii ya ujasiri, kutokuwa na hofu ama woga kwa watu wote anaokutana nao. Hapa ndipo hasa ulipo mgogoro wake na watawala. Hili huwatia hofu na woga mkubwa watawala hawa waovu....
Wanajua kuwa watu wakielimishwa, wakatambua WAJIBU na HAKI zao, wataiondoa serikali hii madarakani kufumba tu na kufumbua. Hili linaiogopesha sana CCM na serikali wanayoingoza....
3. NI MSOMAJI SANA WA VITABU HUYU JAMAA:
Ili kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali, sharti utafute maarifa. Sharti usome vitabu na vyanzo vingine mbalimbali vya maarifa...
Huyu ndugu anasoma sana. Simjui na wala sijawahi kukutana naye uso kwa uso karibu. Lakini ninapomtazama kwenye TV akiongea, mtu mdadisi atatumbua hili moja kwa moja...
Ukisikiliza na kutazama hotuba yake ya jana Serengeti utaelewa nikisemacho hapa. Utaelewa kuwa huyu mtu amejaza maarifa kichwani mwake na si matope kama alivyo Polepole ama Cyprian Musiba wa CCM.....
4. NI MGOMBEA PEKEE KATI YA WOTE ALIYETOA UHAI WAKE KWA AJILI YA HAKI ZA WENGI:
Hii ni sifa very exceptional. Huyu bwana amepitia njia ngumu mno hadi kufikia hatua hii aliyonayo hapo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa taifa hili zuri la Tanzania...
Huyu ndugu kwa siku saba achilia mbali miaka miwili na ushee akiuguza majeraha ya risasi kitandani, alikuwa kuzimu. Alionja KIFO na MAUTI lakini kwa sababu anazojua Mungu mwenyewe, alimfufua tena Tundu Lissu. Yuko hai na ndiye huyu ambaye watu wanamuona kama Messiah wao na basically ndivyo ilivyo, ndivyo itakavyokuwa....
5. NI SPEECH GIVER & INFLUENCER MZURI KUPINDUKIA. HUCHOKI KUMSIKILIZA..!!
Wanasiasa wenye kipaji cha namna hii ni wachache mno Tanzania. Huko nje namfahamu mtu mmoja, Martin Luther King Jr, mpigania haki za weusi wa Marekani miaka ile...
Hotuba za Tundu Lissu ni za kushawishi, kuhamasisha, kutia morali na kuwaondolea watu hofu, mashaka na woga....
Watu kama hawa siku zote ni HATARI katika serikali zote za kidikteta zinazogandamiza UHURU na HAKI za kiraia...
Huwindwa kama wanyama pori ili kuwaua kama njia pekee ya kuwaondoa maana HOJA ZAO mara zote hazijibiki na Mara zote ni chungu na zinachoma mithili ya mkuki moyoni...
Mara zote watu wa aina hii hugeuziwa kibao na kuitwa wachochezi, wahamasisha vurugu na wahatarisha amani. Hutungiwa hata sheria kwa ajili yao tu...
Hii yote, kosa lao ni moja tu. Kufumbua macho, akili na ufahamu wa watu wa kutambua WAJIBU na HAKI zao dhidi ya serikali na viongozi wao....!!
Huyu ndugu kwa hakika ni TUNU YA TAIFA hili. Ni machachari and very unique. Nitampa kura yangu mimi na familia na jamaa na rafiki zangu wote....