Watu wa CCM kila Mbunge wa Singida Mashariki Mheshimiwa (anastahili kuitwa Mheshimiwa)Tundu Lissu anapotoa hoja zake za kisiasa kwa kutumia taaluma yake ya kisheria, humponda sana kwamba uwezo wake ni mdogo kwenye kuchambua hoja za kisiasa kisheria.
Lakini inawezekana ni kweli kwamba Lissu (kwa mtazamo wa wana CCM) uwezo wake kisiasa na kisheria ni mdogo sana. Lakini ni Lissu ambaye kila wakati anakuwa upande sahihi dhidi ya wanasiasa na wanasheria wanaotumiwa na CCM katika kuendesha mambo mbali mbali ya kisheria na kisiasa serikalini. Mambo mengi yanayokanushwa na "wabobezi" wanaotegemewa na CCM dhidi ya hoja za Lissu, huja kuonekana baadaye kwamba Lissu alikuwa sahihi.
Wakati Lissu anahangaika dhidi ya sheria Mbovu na wawekezaji "uchwara" kwenye sekta ya madini, wabobezi wa Sheria na siasa toka CCM walimwita Lissu kuwa ni mtu anayetisha wawekezaji. Leo hii wawekezaji waliowaita wenyewe, wakaingia nao mikataba, wakawapa migodi, CCM wanawaita wezi!!
Kwa ivo inawezekana kwa mitazamo hasi ya Ki-CCM Lissu si mwanasiasa bora wala si mwanasheria mbobezi, lakini kuna ukweli unaobakia kwamba Lissu ni Mwanasheria na mwanasiasa mwenye ujasiri wa kipekee kwenye kusimamia sheria na kupigania maslahi ya nchi yetu Tanzania.
Kunguru wa Lumumba msidhani kila sehemu ni jalala la kupatia mizoga!!