Tundu hakuwa msaliti, alitakiwa ajibiwe kwa hoja sio kwa mtutu. Alipwe pesa zake

Mkuu leo mchana tulikua na huo mjadala! Mtu anaanza kumlaumu tu Lissu namuuliza hivi unajua Lissu kaanza hizi harakati za madini lini? Hana jibu! Namuuliza wewe binafsi Lissu amewahi kukukosea nini mpaka unamchukia? Hana jibu!

Nilichokuja kugundua watu wengi wanaomchukia Lissu Wana uwezo mdogo sana kichwani kureason..(Mtanisamehe kwa hili)
Nikweli wengi gorofani hamna kitu
 
Lengo la serikali halikua hiyo pesa, lengo kuu ilikua kuwaludisha Acacia barabarani,

Na ilifanikiwa, maana mikataba iliangaliwa upya hadi ikazaliwa Twiga,

So ukisema serikali ilidanganya watu hautokua sahihi.

..huwezi ku-negotiate kwa kuwa na madai ya uongo, au yasiyo make sense.

..serikali ilikuwa inasema mambo mengi ya uongo ktk vyombo vya habari ili kuwapumbaza wananchi.

..lakini naamini ktk majadiliano ndiko mbivu na mbichi zilipojulikana.

..na ukiangalia mkataba ambao serikali imesaini na barrick ni kitu tofauti kabisa na madai waliyokuwa wanawatangazia wananchi.

..hata kampuni ya Twiga imeanzishwa kwasababu ya mabadiliko ya sheria yaliyofanyika wakati wa JK na siyo vurugu alizokuwa akifanya Jpm.

..tatizo la Jpm ni kwamba hata akisema ukweli lazima adanganye; kufanya jambo la heri lazima atumie shari. Na hicho ndicho kilichotokea ktk " mgogoro " wetu na acacia.

NB:

..acacia ni kampuni iliyoanzishwa na barrick. Lakini serikali ilikuwa inajenga taswira kwamba barrick ni wasafi na acacia ni wachafu.
 
Mungu anasema maono ya lissu yapo na wamtakiao mabaya watashudia utukufu wa Mungu juu yake iwe mvua au jua ,wamekufa au WAKO hai, jiulize
1. Kapigwa risasi zaidi ya risasi za kumuua mnyama yeyote Dunian ila yupo, na anadunda pamoja na surgery kibao ambazo wenda zinavunja record, katika ulimwengu wa tiba ,25
2. Amenyimwa pesa ya matibabu, ya kujikim ila Ndo bado leo kavaa suti kali na imemkaa mwilini sawasawa,
3. Mkasema enzi za mwendazake haludi nchini, ebo ,mwanaume kaja mchana kweupe, kavuka vikwazo vyote vya nec, nakuanza kimbiza mwizi Kimia kimia bila huruma,
Lissu sio tumuonavyo huyu ni mshindi, alisema mchungaji mmoja,

Subilin wakati ,mda ,dakika muone utukufu wa Mungu ulivyo wa ajabu, ipo siku yaja
4.Aliyetaka kumuua katoweka yeye, Mungu mkubwa.
 
Baadhi ya Watanzania wenzetu wana matatizo sana. Wanapenda kushadadia mambo bila kufanya tafakuri.

Kama mtu anasema mtapata hasara mkivunja mkataba fulani ndio apigwe risasi?

Mtu akisema tutumie akili kudili na masuala ya kisheria ndio apigwe masasi?

Serikali hii hii inatakiwa kumlipa Lissu stahiki zake. Ndio hii hii serikali iliyo mfanyia kitu mbaya.
Kiufupi hakuna Mtanzania aliyepigania haki za mikataba ya madini kumzidi Tundu Lissu toka Tanganyika ipate uhuru toka kwa Mkoloni Mwingereza.

Kama uzalendo ungekuwa unapimwa kwa kutetea haki za madini kwa wazawa basi Tundu Lissu angekuwa ndiye Mzalendo Namba 1. Msidanganywe na propaganda za Magufuri na Kabudi.

Atakayebisha hili anaweza hata akamkataa mama yake aliyemzaa. Tafuta hata mapendekezo ya Tume ya Bomani, Time ya Mruma au Tume ya Lawrence Masha. Wote recommendations zao ni zile zile ambazo Lissu amwweka kwenye Tafiti zake au machapisho yake
 
..YES.

..acacia waliishtaki serikali ya Tz.

..kesi ilisitishwa baada ya barrick kununua hisa za minority share holders wa acacia.

..na madai ya usd 191 billion ya serikali dhidi ya acacia nayo yameyeyuka.

..TUMETAPELIWA.

Tumepigwa pakubwa
 
..huwezi ku-negotiate kwa kuwa na madai ya uongo, au yasiyo make sense.

..serikali ilikuwa inasema mambo mengi ya uongo ktk vyombo vya habari ili kuwapumbaza wananchi.

..lakini naamini ktk majadiliano ndiko mbivu na mbichi zilipojulikana.

..na ukiangalia mkataba ambao serikali imesaini na barrick ni kitu tofauti kabisa na madai waliyokuwa wanawatangazia wananchi.

..hata kampuni ya Twiga imeanzishwa kwasababu ya mabadiliko ya sheria yaliyofanyika wakati wa JK na siyo vurugu alizokuwa akifanya Jpm.

..tatizo la Jpm ni kwamba hata akisema ukweli lazima adanganye; kufanya jambo la heri lazima atumie shari. Na hicho ndicho kilichotokea ktk " mgogoro " wetu na acacia.

NB:

..acacia ni kampuni iliyoanzishwa na barrick. Lakini serikali ilikuwa inajenga taswira kwamba barrick ni wasafi na acacia ni wachafu.
Mkuu naomba ushahidi ni kipindi gani katika utawala wa JK alianza mazungumzo ambayo baadae yakaja kuzaa Twiga

Simdharau JK, amefanya kazi kubwa sana kwenye utawala wake.
 
Magufuli alikuwa anajuwa kiwango cha ujinga wa Watanzania walio wengi na ndiyo ukawa mtaji wake kwa propaganda za UWONGO. Wasomi na wajuzi wa mambo akawanyamazisha kwa sheria mbaya za mtandao, takwimu na sheria ya habari. Amedanganya na ikawa ndiyo hulka yetu na mpaka alipokufa tukadanganywa kwa siku 7 kuwa yupo anachapa kazi.

Barrick amerudi kama Twiga Corporation na tukapewa 16 ya second class shares (No voting ppwers), tukaahidiwa 50/50 ya economic benefits (wajinga wanadhani economic benefits =Commercial profits).

Bado Mahakama zetu hazitakuwa na jurisdiction kwenye business dispute (lazima twende London), smelter ya makinikia hakuna. Na kimkataba wa 1998 makinikia yanayokadiriwa kuwa na 0.7 Kg kwa 20ft container ni mali yao, ya kwetu ni Gold na Silver tu ambayo wanailipia. Ile USD 190 Bilion aka noah moja kwa Mtanzania imebaki ndoto za mwendawazimu na Goodwill ya USD 300 Million inamezwa ma madai ya kodi ambazo hatukuwafidia.

Hapo ndipo unamkumbuka Tundu Lissu, kuliko kumpiga risasi walipaswa wamuinguze kwenye Negotiation Team ya Prof Kabudi ili atuongoze tuwabane
 
Mkuu naomba ushahidi ni kipindi gani katika utawala wa JK alianza mazungumzo ambayo baadae yakaja kuzaa Twiga

Simdharau JK, amefanya kazi kubwa sana kwenye utawala wake.

..shares za serikali ktk kampuni ya Twiga sheria yake iliandikwa wakati wa JK.

..kama utakumbuka JK naye aliunda tume ya madini na bunge lilifanyia marekebisho sheria ya madini.
 
Mkuu leo mchana tulikua na huo mjadala! Mtu anaanza kumlaumu tu Lissu namuuliza hivi unajua Lissu kaanza hizi harakati za madini lini? Hana jibu! Namuuliza wewe binafsi Lissu amewahi kukukosea nini mpaka unamchukia? Hana jibu!

Nilichokuja kugundua watu wengi wanaomchukia Lissu Wana uwezo mdogo sana kichwani kureason..(Mtanisamehe kwa hili)
Wakati mwingine unajiuliza, uhuru tulioutaka sana kutoka kwa wakoloni ulikuwa wa kazi gani? Kama mwaka 1920 watu walishindwa kutoa maoni au kuwa na mawazo yanayokinzana na watawala, na leo 2020 bado ni makosa kuwa tofauti na watawala, uhuru wetu ulikuwa wa kazi gani?

Tuko huru au tumebadilisha wakoloni?
 
Nilitaka ushahidi mkuu, ila poa nimekuelewa

Ila pamoja na kazi kubwa aliyoifanya JK, hatupaswi kuudharau mchango wa JPM hata kama tunamchukia,

Kuhusu mapitio ya sheria kipindi kile nakumbuka ilihusu zaidi Gas mkuu.
 
Nahisi sisi Watanzania ni special edition hapa duniani, namna yetu ya kufikiri, kuchanganua na kureact iko tofauti sana na binadamu wengine hapa chini ya Jua!
 
Nilitaka ushahidi mkuu, ila poa nimekuelewa

Ila pamoja na kazi kubwa aliyoifanya JK, hatupaswi kuudharau mchango wa JPM hata kama tunamchukia,

Kuhusu mapitio ya sheria kipindi kile nakumbuka ilihusu zaidi Gas mkuu.

..Jpm amefanya alivyoweza.

..ila alikosea pakubwa kumgeuza adui, Mtz aliyepigania rasilimali zetu wakati yeye Jpm akiwa hana ujasiri wa kupigania rasilimali hizo.

..natufuta namna ya kuhalalisha hukumu ya KIFO dhidi ya Lissu kutokana na aliyoyasema wakati wa mgogoro na acacia lakini nimeshindwa.
 
Mkuu leo mchana tulikua na huo mjadala! Mtu anaanza kumlaumu tu Lissu namuuliza hivi unajua Lissu kaanza hizi harakati za madini lini? Hana jibu! Namuuliza wewe binafsi Lissu amewahi kukukosea nini mpaka unamchukia? Hana jibu!

Nilichokuja kugundua watu wengi wanaomchukia Lissu Wana uwezo mdogo sana kichwani kureason..(Mtanisamehe kwa hili)
Uko sawa mkuu. Shauri yao watakaoona umewakosea. Huna haja ya kuwabembeleza
 
Mwendazake aliwafitinisha sana Watanzania na watu waliokuwa wanawatoa matongotongo,Lissu alikuwa anatoa Elimu watanzania wajitambue ila kwa sababu ya roho mbaya za mwana propaganda ambae alipandikiza kwa wapumbavu akili za kimasikini kwa kuwaita WANYONGE,wakamuona msaliti,wakati ndiye mtetezi wao wa kweli,halafu majizi yakawa ndiyo watetezi.
Ili kuwaibia ilibidi wahakikishe kila mtoa elimu anadidimizwa,Taifa lumepitia wakati mgumu sana
 
Kiufupi hakuna Mtanzania aliyepigania haki za mikataba ya madini kumzidi Tundu Lissu toka Tanganyika ipate uhuru toka kwa Mkoloni Mwingereza.

Kama uzalendo ungekuwa unapimwa kwa kutetea haki za madini kwa wazawa basi Tundu Lissu angekuwa ndiye Mzalendo Namba 1. Msidanganywe na propaganda za Magufuri na Kabudi.

Atakayebisha hili anaweza hata akamkataa mama yake aliyemzaa. Tafuta hata mapendekezo ya Tume ya Bomani, Time ya Mruma au Tume ya Lawrence Masha. Wote recommendations zao ni zile zile ambazo Lissu amwweka kwenye Tafiti zake au machapisho yake
Good and well said.
 
Back
Top Bottom