Tundu Lissu aache kumsema vibaya Hayati Magufuli

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Ni muhimu sana tena sana kwa Tundu Lissu kuepuka kumsema vibaya Hayati John Magufuli katika mikutano yake.

Ikumbukwe kuwa, pamoja na mapungufu machache aliyokuwa nayo kama ilivyo kwa binadamu yeyote, Hayati Magufuli ana watu wengi sana wanaomkubali mpaka sasa.

Anakubalika sana kuliko hata walio hai.

Nawasilisha.
 
Acha asemwe Ili wengine wajifunze
Sawa, lakini ikumbukwe kuwa, TAL ni mwanasiasa kwa hiyo anahitaji watu.

Watu hao anaowahitaji TAL kama mtaji wa kisiasa ndio wanaomkubali sana JPM anayesemwa vibaya hadharani. Kwa hiyo, kumsema vibaya JPM ni kupunguza wafuasi wengi sana wa Siasa, lakini pia kumsema vibaya JPM haisaidii chochote kile.
 
Upo sahihi ila chukulia mfano wewe ndiye TAL na maswahibu uliyopitia huenda ungemponda huyo mtu zaidi ya yeye anavyomuongelea
 
Umenishangaza sana uliposema JPM alikuwa na mapungufu machache!
N. B, Tanzania yote ingegeuzwa vingunguti.
Chawa wake na wakatili wenzake watamkumbuka sana!
 
Upo sahihi ila chukulia mfano wewe ndiye TAL na maswahibu uliyopitia huenda ungemponda huyo mtu zaidi ya yeye anavyomuongelea
Ni kweli, ni ngumu sana kusamehe mtu aliyekufanyia mabaya, lakini kwa mustakabali wa siasa, ni vema kuwa na ngozi ngumu ya kusamehe ili mambo mengine yaendelee.
 
Ingekuwa wale wanaohusishwa na pyu pyu pyu pyu wanatoka Serikalini ningewafukuza kazi, na kuwapeleka mahakamani, na kunyongwa.

Bahati mbaya hawakutoka huko, kwani wanaotoka huko 'huwa hawakosagi'....yaani umkute mtu katili na AK amkose hivi hivi tu? Eboo!

Akimaliza kuonyesha majerahaha atarudi Ulaya kukaza vyuma na skruu....abakie huko asijetumalizia ma Vii eiti
 
Mtume Muhammad ana wafuasi mabilioni duniani, na kuna binadamu wengi wanamsemea mabaya. Japo hawajawahi kumsikia...

Yesu Kristo ana wafuasi mabilioni duniani na kuna binadamu wengi wanamsema vibaya japo hawajawahi kumjua...

Sembuse Magufuli?

Tusipangiane maisha.

Au nasema uongo ndugu zangu?

Basi hili nalo ukalitazame
 
We
We ni sawa tu na hao marehemu unaongea upupu. Katishie wafu siyo walio hai. Hao wanaomshabikia mfu km wewe wote ni wafu mpigieni tena kura huko mlipo
 
Magufuli hakubaliki na watu wengi kama unavyotaka kutuaminisha. Ushahidi ni namna alivyopora uchaguzi 2019 na 2020. Anayekubalika hawezi kuwa na hofu kiasi kile. Kwa nini alijiprintia fomu moja ya Mgombea urais?

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Nyie mnaofungua nyuzi za kumhusu huyu mwovu ndiyo mnakaribisha mijadala ya kumsema vibaya kama wewe ulivyofanya
 
Acha ujinga ungekuwa ni wewe umetendewa alivyotendewa Lissu ungemsifia huyo Magufuli? Tumia akili
 
Mnatumia nguvu nyingi sana kumtetea, sasa wewe acha amseme vibaya(of course kwa mabaya yake) ndipo tuone huko kukubalika kwake.
Viongozi waliopo ndipo wanapojifunza kuwa ukitenda mabaya daima utakumbukwa kwa mabaya yako hata baada ya kufa, unyama aliowafanyia Watanzania unapaswa kutungiwa kitabu kabisa ili iwe fundisho kwa uzao ujao wa viongozi.
Ukipanda bangi usitegemee kuvuna mahindi, Jiwe anavuna alichopanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…