Kifo cha Magufuli kilileta hasara gani, labda kwa lile kundi lenu la watu wasiojulikana, maana huenda miradi yenu ilikuwa haijakamilika. Alichokuwa anakifanya Magufuli dhidi ya wapinzani ni kiburi cha ulevi wa madaraka sio zaidi ya hapo. Mama Samia hatoi nafasi kwa upinzani kama hisani, bali huo ndio uhalisia na ndio katiba isemavyo. Mzungu gani anamridhisha huyo mama Samia? Kuna wazungu gani wanahangaika na siasa za nchi masikini boss?
Umma upi wa watanzania, ule umma uliokuwa unawekewa maneno mdomoni kuwa unamkubali Magufuli, lakini ilipofika wakati wa uchaguzi ikabidi apore uchaguzi ili mtazamo halisi wa watanzania usifahamike?! Ukweli wa uchaguzi ule hata mama Samia anaujua, na vile hana ulimbukeni wa madaraka inabidi afuate uhalisia, na sio ule ushamba wa yule limbukeni. Unajisifu unakubalika, kisha inafika siku ya uchaguzi unapora uchaguzi.
Magufuli atakuwa ana impact gani baada ya kufa, wakati hata alipokuwa hai alikuwa anatumia vitisho na vikundi vya kumpamba ili ionekane anakubalika? Angeheshimu uchaguzi maana ule ndio ulikuwa kipimo halisi cha kukubalika kwake na chama chake. Sasa anapora uchaguzi halafu we sukuma gang unasema anakubalika, sijui legacy na upuuzi gani. Uza ubongo huo mzee maana unakaa nao kwa hasara.