Hilo zuio awamu zingine lilikuwepo.
Wangapi wapo jela kwa kubambikwa,mama yake kabendera Nani alimuuwa,bensaanane je,rejea chaguzi feki za marudio na serikali za mitaa umewahi ona wapi uhuni ule,vipi viongozi wa dini awakushughulikiwa kakobe kabla ya kuunga juhudi Hakuwa mtz baada ya kuunga juhudi amekuwa mtz, vipi kuhusu zuio la bunge live Hali uzinduzi wa vyoo Ni live, kupigwa ban kwa magazeti, vipi kuhusu usiri wa matumizi ya Kodi zetu, vipi kuhusu usiri juu ya mikataba inayotafuna Kodi zetu, vipi kuzulumiwa kwa wakulima, kuliwa kwa rambirambi, vipi kuzuia pesa za maendeleo majimbo ya upinzani,vipi kuhusu wasiojulikana amewahi kemea?,vipi kamata kamata ya wapinzani Hadi mikutano ya ndani Tena ya wanawake hofu ya nini,vipi kupigwa risasi kwa Lisu Tena sehemu nyeti. Jibu haya kwa uchache mengine yanakuja.
1. Huko nyuma mazuio yalikuwepo lkn sheria hazikufuatwa. Serikali ya JPM imeamua kutekeleza sheria hiyo ili ilete maendeleo yaliyokusudiwa.
2. Waliopo jela kwa kubambikwa kama wapo ni makosa. Sheria zipo you can prove beyond doubt that someone has been wrongly held in custody. Then follow the legal procedures to set him/her free, then demand compensation.
3. Mama yake Kabendera unaweza ukataja aliyemuua kama unamjua. Nenda polisi ukawasaidie kurahisisha upelelezi.
4. Ben Saanane aliuawa kwa mipango ya akina Mbowe. Labda wewe tu ndo hujui au unajua lkn unaendeleza madai ya chadema kuinyooshea vidole serikali wkt ukweli mnaujua. Hayo mambo ya kujiteka na kuuana ni mambo ya kawaida ndani ya chadema. Chacha Wangwe nani alimuua?
5. Wapinzani wakishindwa uchaguzi wanauita uchaguzi feki. Wakishinda unakuwa uchaguzi safi. Hizo ni akili za wendawazimu.
6. Mambo ya viongozi wa dini kushughulikiwa, hizo ni hoja hafifu za Lisu. Nawe umemezeshwa sumu hivyo hivyo. Unapaswa kufanya utafiti kujua ukweli. No research, no right to speak.
7. Bunge live. Ni nchi gani uliona bunge lao linakuwa live kila siku mwanzo hadi mwisho. Unapata wapi muda wa kuangalia bunge live? Utafanya kazi saa ngapi? Matukio ya uzinduzi hayapo kila siku. Na yanapokuwepo ni ya muda mfupi. Malalamiko yako ktk hili hayana logic. Hizi ni kati ya agenda za kijinga za CHADEMA.
8. Kupigwa ban magazeti. Hizi hoja mufilisi. Usalama wa Taifa kwanza, magazeti badae.
9. Usiri wa kodi zenu. Hapa ndo naona wewe ni bendera fuata upepo. Unamezeshwa maneno mazima mazima na wewe huna uwezo wa kupambanua pumba na mchele. Hujui kazi ya kodi? Siri gani ulitaka kujua na ukanyimwa? Kodi kazi zake ni kutoa huduma kwa wananchi. Huduma hazitolewi? Acha kudandia madai ya kipuuzi ya watu waliofilisika kisiasa. Akili za kuambiwa na wewe weka zako.
10. Madai yako Mengine yaliyobaki. Madai yote uliyoorodhesha ni ya upotoshaji tu. Hayana logic yoyote. Ni madai ya kutapatapa tu ya akina Lisu na wenzake, na wewe unadandia tu kuimba nyimbo hizo hizo. Kama wewe unaongea kwa haki mbona hutaji utafunaji wa ruzuku ya chadema, mbona husemi juu ya CHADEMA kupiga risasi AQUILINA, mbona husemi juu ya Lisu kushiriki kumteka mwandishi wa habari huko Bagamoyo, mbona husemi juu ya CHADEMA kumwagia tindikali kijana huko Nzega Lisu akishiriki kuratibu uovu huo, mbona husemi juu ya dereva wa Lisu kufichwa baada ya Lisu kupigwa risasi, mbona husemi juu ya askari polisi kuuawa huko Kibiti, mbona husemi juu ya sababu za kukimbia chadema akina Prof Balegu, Safari, Zitto Kabwe, wabunge kibao, nk. Usionyeshe kidole kimoja kwa mwenzako wakati vidole vitano vimekuangalia wewe.