Acha upotoshaji! Watanzania tulio wengi tunataka maendeleo ya vitu yaende sambamba na maendeleo ya watu! Hakuna mfanyakazi atakayekubali kunyimwa haki zake za msingi mfano kupandishwa daraja kwa wakati, kisa eti unajenga barabara au kununua ndege!
Mbona wakati wa JK hizo barabara, madaraja, nk vyote hivyo vilijengwa kila kona ya nchi! Lakini bado ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu, haki za wafanyakazi na makundi mengine katika jamii ziliheshimiwa?
Iweje huyu mtu wenu aone barabara na ndege ni vitu vya muhimu sana kuliko haki za wengine? Mbona hatujawahi kumsikia akijipunguzia mshahara na posho zake?
Hata Rais angekua ni Lissu au Hashimu Rungwe, bado hizo barabara zingejengwa tu. Hilo ni moja ya jukumu la serikali yoyote ile duniani. Na kodi tunazolipa na mikopo ya ndani na nje ya nchi, hufanikisha zoezi hilo.