Nimewasikia wananchi wa eneo moja huko mufindi kama sikosei kwenye mkutano wa ndugu Tundu Lisu kuwa hawana barabara pamoja na maji na wamesema wanaomba akichaghuliwa awatengenezee hivyo vitu.
Nikajiuliza kwa nini hao watu hawahitaji maendeleo ya watu wao wametaka maendeleo ya vitu?
Majibu ya Tundu lisu ni kwamba, hata yeye anashangaa kwa nini mpaka sasa hawana barabara na maji, na kwamaba mpaka huko alipotokea mpaka kufika pale jana yake ametembea kwenye njia ya vumbi mpaka alipofika kwenye mkutano akawa amechoka sana hadi kutaka kuahilisha mkutano.
Swali langu kwa Tundu Lissu.
Kama yeye na pesa aliyo nayo, na magari aliyotumia bado amepata maumivu kwa kupita barabara ya vumbi, je anakubali maendeleo ya vitu ni moja ya kurahisisha maendeleo ya watu?
Anaweza kufahamu kuwa kuna watu pia wanahitaji usafiri wa ndege kuwapeleka sehemu husika na pengine kunusuru maisha yao tofauti na wangetumia barabara wasingepona kutokana na umbali?
Je, unaweza kuwa na mapesa mengi na magari mazuri lakini ili ufike kwako ni lazima ukanyage tope kwa kusukuma gari yako na ukifika kwako huna hata umeme unatumia kibatari na gari yako inakuwa chafu mda wote na ndani mwako vumbi kibao kutokana na barabara ya vumbi ambayo magari yakipita vumbi yote inajaa ndani mwako.
Je, utafurahi na maisha hayo ya uchafu kila siku ila una pesa?
Je, Tundu lisu akiingia madarakani atatekereza maombi ya hao wananchi ya barabara na maji waliyo omba au atataka awajaze pesa iii wawe na furaha kwanza?