Pre GE2025 Tundu Lissu, achana na misimamo misimamo ya kipuuzi, ingia kwenye uchaguzi upiganie wabunge 20 na madiwani

Pre GE2025 Tundu Lissu, achana na misimamo misimamo ya kipuuzi, ingia kwenye uchaguzi upiganie wabunge 20 na madiwani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Neno, kipuuzi tu ndipo ulipoharibu sio misimamo ya kipuuzi. Ila uko sawa kwenye misimamo. Alegeze masharti achague watu makini sana wa kuingia kukohoa bungeni mpaka huku nje panatetemeka hata kama hawatapata Urais nchi itachangamka.
Ni ajabu sana kuona watu mnakimbilia uchaguzi tu bila kujali sheria zinazosimamia uchaguzi wenyewe. Hata kwenye michezo tu sheria zinabadilishwa kila mara kuhakikisha kila anayeshiriki anapa haki. Uchaguzi mkuu wa wabunge na rais huamua hatima ya maisha ya jamii husika (wananchi). Kusipokuwepo na sheria isiyopendelea upande wowote ni rahisi sana kupata viongozi (wawakilishi) wasiojali maslahi ya wananchi na kujiamlia mambo kulingana na utashi na kwa faida yao. Mfano aje hapa mzalendo sana aseme kwa nini rais halipi kodi, kwa nini hawezi kushitakiwa kwa makosa ya kiongozi, nk. Kuleta uwajibikaji lazima tujiwekee sheria na taratibu zinazombana kila mtu bila kujali cheo chake.
 
Unaweza kuongea lugha ya Aina hiyo Kwa mwenyekiti wa ccm?

Tumia lugha mzuri basi
NGOJA APOTEZE MUDA WAKE KWENYE NO REFORM NO ELECTION AONE MATOKEO YAKE, WANAUME TUNAPETA TU
 
NGOJA APOTEZE MUDA WAKE KWENYE NO REFORM NO ELECTION AONE MATOKEO YAKE, WANAUME TUNAPETA TU

Hawez kufanya hiyo kitu
Na ujue watu wengi wa ccm ndio wanampa miongozo hasa wale ambao walikuwa Kwa magufuli

So lisu anajipanga na kuwa na wabunge wengi na atafanikiwa
 
Kumbe mnaiyogopa katiba mpya? Kukubalika kwenu kwanini mnaikataa katiba hiyo?
 
Huyu naye katoka nyumbani kwake kuja kuandika upuuzi huu?

Lissu akomae hapo hapo hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
 
Hekima imenionyesha, nikujulishe hilo, yaani upiganie wabunge 20+ na madiwani wa kutosha ili upate nguvu ya kuweza kusonga mbele na kukijenga chama kwa umaridadi zaidi, kwa msimamo wako huna uwezo wowote wa unaoweza kuzorotesha uchaguzi ujao wa mwezi October, jipange sasa andaa wabunge na madiwani wanaokubalika kwa umma, imarisha matawi, na mashina, unless otherwise chadema itakufia mikononi mwako!
Mjinga mkubwa wewe.utakuwa Abdul wewe.katiba mpya kwanza kabla ya yote
 
Hakuna cha nature kuamua, asipojipanga mapema kuona atashindaje aidha akibakia kwenye msimamo wake wanaume tunapeta tu 😊😊😊
Iwapo kwenye harakati ndogo umeangukia pua wewe na genge lako,vipi zile za kikweli kweli?
 
Hekima imenionyesha, nikujulishe hilo, yaani upiganie wabunge 20+ na madiwani wa kutosha
Una hakika watawapata? Kwanini hawakuwapata 2019? 2020? Kwani hawajawapata 2024? CCM imesema kwakuwa wameshinda 2024 kwa 98% basi na uchaguzi mkuu watashinda kwa kiwango hicho hicho—UNAAMINI HALI ITAKUWA TOFAUTI? KWA VIGEZO VIPI?
 
Chadema ikijipanga vizuri itajipatia viti 20+ bila tatizo lolote, lakini sio arusha, Yapo maeneo ambayo chadema kushinda hakuna mjadala, jimbo moja lipo sumbawanga!
 
Mjinga mkubwa wewe.utakuwa Abdul wewe.katiba mpya kwanza kabla ya yote
WORK FORCE YA KWENDA KUIPIGANIA BUNGENI IPO WAPI? / HATUWEZI SEMA TUNAPITISHA KATIBA YA WARIOBA KWANI NAYO IMESHAKUWA OUT DATED, TANZANIA INAHITAJI KATIBA MPYA, BASI MSINGI WAKE NI LAZIMA UANZIE BUNGENI SASA BUNGENI UNA AKINA NANI? / TUSAMEHE MWENYE UCHAGUZI WAKE 2020, TUANZE UPYA, TUAMUE UPYA, YAPO AMBAYO NI MAGENI TUMEJIFUNZA TOKA KWA MAJIRANI ZETU, TUNATAKIWA KUYAWEKA KATIKA KATIBA MPYA!
 
Katiba mpya ni fedha, ni suala la Kitaifa, sio swala la kamati ya watu 10-20, ni mchakato na mchakato huu ni lazima uanze upya hatuwezi kufufua viporo, tunataka kazi ianze na itimilike moja kwa moja, Rais wetu alishatolea maelezo huko kitambo sitaki kuyarudia.
 
Lissu et al shikirieni hapo hapo..wameshaanza kupagawa..

Njooni na MIKAKATI ya NGUVU inayotekelezeka, bila ya kusahau huu wa kwenda KUWASILIBIA kwa wenye dunia..kusanyeni tu evideces za kutosha...NA SANDUKU LA KURA LIHESHIMIWE
 
Hekima imenionyesha, nikujulishe hilo, yaani upiganie wabunge 20+ na madiwani wa kutosha ili upate nguvu ya kuweza kusonga mbele na kukijenga chama kwa umaridadi zaidi, kwa msimamo wako huna uwezo wowote wa unaoweza kuzorotesha uchaguzi ujao wa mwezi October, jipange sasa andaa wabunge na madiwani wanaokubalika kwa umma, imarisha matawi, na mashina, unless otherwise chadema itakufia mikononi mwako!
Wakikata majina yote ya wagombea kama alivyofanya Magufuli na Samia serikali za mitaa je?
 
Hekima imenionyesha, nikujulishe hilo, yaani upiganie wabunge 20+ na madiwani wa kutosha ili upate nguvu ya kuweza kusonga mbele na kukijenga chama kwa umaridadi zaidi, kwa msimamo wako huna uwezo wowote wa unaoweza kuzorotesha uchaguzi ujao wa mwezi October, jipange sasa andaa wabunge na madiwani wanaokubalika kwa umma, imarisha matawi, na mashina, unless otherwise chadema itakufia mikononi mwako!
Hakuna haja ya kushiriki uchaguzi usiokuwa huru na wa haki.
 
Subutu yake mimi ni mbobevu, nashauri kwa wema kabisa.
Unless anatafuta ruzuku, mimi sioni ni kwanini Chadema waingie kwenye uchaguzi. Magufuli alifungua ukurusa mpya kabisa kwenye siasa za Tanzania i.e. rais aliyepo madarakani hapaswi kufanya uchaguzi bali kutumia dola kuingiza watu anaotaka.
 
Suala la katiba liko mikononi mwa CCM na unaona kabisa hawana huo mwelekeo Chadema haina uwezo wa kulazimisha.
Suala la katiba siyo la CCM bali lilitakiwa liwe la wananchi japo wananchi bado wamelala. Watakuja kugutuka siku mambo yameshaharibika.
 
Hekima imenionyesha, nikujulishe hilo, yaani upiganie wabunge 20+ na madiwani wa kutosha ili upate nguvu ya kuweza kusonga mbele na kukijenga chama kwa umaridadi zaidi, kwa msimamo wako huna uwezo wowote wa unaoweza kuzorotesha uchaguzi ujao wa mwezi October, jipange sasa andaa wabunge na madiwani wanaokubalika kwa umma, imarisha matawi, na mashina, unless otherwise chadema itakufia mikononi mwako!
GNoPC1CXoAAzWwG.jpeg
 
Back
Top Bottom