Pre GE2025 Tundu Lissu afukuzwe CHADEMA haraka

Pre GE2025 Tundu Lissu afukuzwe CHADEMA haraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kula pesa ya mbowe kwanza, Lisu bila chadema ataishi bila shida siyo lazima kwenda kokote, Taasisi za kimataifa zinamhitaji sana, Mbowe nje ya Siasa na endapo mmekula pesa zake zote atakuwa mzee baraza vijijini kwani Mbowe ni division zero Darajani, Pesa anayotumia sasa kuununua uenyekiti itokee akosa kuwa mwenyekiti atakuwa kichaa lazima augue sana
LISU sina ubishi na hilo ila Chadema aiache tu aende huko kwenye mashirika ya kimataifa, nadhani atatulia kidogo. Anahitaji kujitazama katoka wapi na anaenda wapi. Nahakika akishinda CHADEMA haitasimama kama wafuasi wake mnavyodhani.
 
Nimeona mchakato huu usipite bila kutoa neno japo dogo kwa kuanzia.
Mkuu Jose, Joseph Ludovick , kwanza asante sana kwa wewe kutia neno, jf ya sasa ina madogo wengi ambao hawakujui wewe ni nani na ulikuwa nani Chadema, wala hawajui roles ulizokuwa una play Chadema ndio maana wanakubeza humu, usiwajali, sisi wa long time tunakufahamu, tunakuheshimu na hatuwezi kupuuzia hoja yako yoyote kwasababu tunajua ulikuwa jikoni, madogo humu hawakujui!. Ila wewe kutaka Lissu afukuzwe Chadema isije kuwa ni muendelezo wa zile hasira za Lissu kutoa siri za ndoa yako Lwakatare Hajawahi Kusimamia Ndoa Yangu
Kwa mambo aliyofanya na kusema mpaka sasa, kuna jambo moja pekee ambalo ni muafaka kwa Tundu Lissu nalo ni Kufukuzwa CHADEMA.
Naomba kuheshimu maoni yako, nakushauri kwa vile wewe ni an inside man, andaa tuu hati ya mashitaka, list down makosa yote ya Lissu na ushahidi wake, mpelekee KM JJ.Mnyika, Chadema itaitisha fasta ile kangaroo court yake ya CC na kumfukuza Lissu fasta, na huo ndio utakuwa mwisho wa Lissu ili Mbowe apite bila kupingwa. Hili likifanyika tutamshauri Lissu akubali tuu yaishe, akubali kufukuzwa arejee zake Ubelgiji au aende Marekani kuungana na familia yake, aiche Chadema salama waendelee na Sultan wao kwa amani.
Kwetu sisi tunaomfahami hasa maisha yake, tunajua kuwa ni Muongo na mjanjamjanja sana. Amedanganya kila kitu. Wakati anajua kila kilichotokea CHADEMA ikiwa ni pamoja na mambo ya kihalifu, Lissu hawezi kujitenga na upuuzi wa CHADEMA.
Hii maana yake na wewe pia unayajua mambo ya kihalifu ya Chadema, kujua uhalifu na kutouripoti ni kosa la jinai!. Mimi kama mwandishi wa habari, baada ya kuujua uhalifu wa Chadema, niliuandikia makala na kuuzungumza humu Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba! wewe baada ya kuujua uhalifu wa Chedema je ulifanya nini kingine chochote zaidi ya ile video yako ya Bukoba Boy kwenye Youtube?.
Naomba kukuuliza, baada ya bandiko lako hili CHADEMA imchunguze Mohamed Mtoi , mara mlengwa alikufa kwa ajali TANZIA - Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali
je ilikuwa ni ajali ya kawaida au kama ile ya Chacha Wangwe?.
Kwa wasiokumbuka, Lissu alishabikia vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa mkuu wa wilaya wa kike na wahuni wa CHADEMA.
Hii sikuwahi kuisikia, unaweza tukumbusha tukio hili?, maana wakati muafaka ndio huu!.
wakati huohuo alisimamia waziri mmoja wa leo (hakuwa waziri wakati ule) kutekwa Nyara na wahuni wa CHADEMA.
Duh...!, kumbe Chadema wanateka nyara?!. Hii ndio nasikia leo, ni waziri gani huyo alitekwa nyara na Chadema leo ni waziri na anawachelea magaidi?.
Lissu amesimamia maamuzi yote ya kuwafukuza na kuwaaibisha waliojaribu kugombea uenyekiti huko nyuma akiwa mwanasheria mkuu wa Chama akifikia kuwatuhumu kwa uhaini dhidi ya chama.
Hii ni kweli , kwa Zitto niliwapa tahadhari ya karma Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
Lissu alihusika kuficha taarifa za wanachama kukituhumu chama kuhusika na ajali ya kada aliyekuwa amejipenyeza Chadema kikachero lakini wakamgundua na kumuwahi.
Kumbe Chadema huwa inahusika na ajali?. Hakuna ubaya ukizitaja tukazijua
Pia tutapenda kumjua huyo kada, aliyejipenyeza kikachero, ambaye aligundulika na aliwahiwa, tunaomba update alishughuliwaje
Je yupo hai au ndio vile tena kama Ben Saanane ?
P
 
Nimeona mchakato huu usipite bila kutoa neno japo dogo kwa kuanzia.

Kwa mambo aliyofanya na kusema mpaka sasa, kuna jambo moja pekee ambalo ni muafaka kwa Tundu Lissu nalo ni Kufukuzwa CHADEMA.

Kwetu sisi tunaomfahami hasa maisha yake nje ya media, tunajua kuwa ni Muongo na mjanjamjanja sana. Amedanganya kila kitu. Wakati anajua kila kilichotokea CHADEMA ikiwa ni pamoja na mambo ya kihalifu, Lissu hawezi kujitenga na upuuzi wa CHADEMA.

Kwa wasiokumbuka, Lissu alishabikia vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa mkuu wa wilaya wa kike na wahuni wa CHADEMA. wakati huohuo alisimamia waziri mmoja wa leo (hakuwa waziri wakati ule) kutekwa Nyara na wahuni wa CHADEMA.

Lissu amesimamia maamuzi yote ya kuwafukuza na kuwaaibisha waliojaribu kugombea uenyekiti huko nyuma akiwa mwanasheria mkuu wa Chama akifikia kuwatuhumu kwa uhaini dhidi ya chama.

Ni yeye aliyetetea mafisadi wakubwa walipoanza kufikishwa mahakamani wakati ule na akageuka mtetezi wa mafisadi.

Lissu alihusika kuficha taarifa za wanachama kukituhumu chama kuhusika na ajali ya kada aliyekuwa amejipenyeza Chadema kikachero lakini wakamgundua na kumuwahi.

Naam, Lissu amekuwa katili na asiye na Roho ya utu hata kidogo. Alishangilia kifo cha Mwenyekiti wa CCM kilipotokea.

Binafsi sina maslahi na nani anaweza kuwa mwenyekiti. Mimi natamani Lissu naye sasa apitie kile ambacho yeye mwenyewe aliwapitisha wenziye. Afukuzwe uanachama wa Chadema haraka na bila huruma.
umeandika mambo kijumla jumla mno..... mengine ni ya kufikirika hayana ushahidi
 
Kama wewe sio mchagga Pole sanaaa. Wachaga tumewazidi mbali sanaaa kwa akili na kikoba chetu hamtakaa kukiongoza. Anzisheni cha kwenu nyumbu nyie.
Ulichowazidi Wachaga wengine ni upumbavu na hilo si lakupongezwa.
 
Ahahahahaha! Eti Lissu ana watu wengi, KUMBAVU! Alivyopigwa risasi walifanya nini hao watu wengi? Siku ile baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 alipokuwa anakimbia airport ili aende Ubeleji mbona alikuwa peke yake na Maafisa wa Ubalozi wa EU tu? Hao watu wengi alionao walikuwa wapi? KUMBAVU!!!
Mkuu watu wengi wakikusapoti ndo huwezi kufa au kupigwa, Magufuri kipenzi cheti / Cha wengi alikufa na nani?
 
Wewe kama Nani?
Kama mtu ninayemfahamu maisha yake ya Udanganyifu. Lissu siyo dikteta uchwara bali ni dikteta kamili. Wote waliowahi kuwa karibu naye kiuongozi wanalifahamu hili. Sidhani kama wana Chadema sasa wanataka kutawaliwa na Mr.Haambiliki. pili Lissu hana Any policy accomplishment wala hana maono yoyote wala msimamo wa kisera. Malalamiko tena ya kinafiki hayawezi kuongoza chama. Kama anadanganya kwenye mambo yanayofahamika itakuwaje kwa yasiyofahamika?
 
Huu ujinga bakia nao huko unaposhinda ghetto kwa mbowe ukivuta bangi, humjui wala kumfahamu lisu na kama ungemjua usingemsingizia hayo yote ya kijinga uliyoyaandika kisa njaa zako umekula pesa za mbowe na kuja na ujinga eti lisu afukuzwe? Kusema madudu ya mbowe udhaifu mapungufu ya mbowe kuna ubaya gani? Hiki ni kipindi cha kampeni unataka kumpangia Lisu cha kusema ? Kisa eti atafukuzwa akisema madhambi ya mbowe? Chadema itaoza ikiendelea kuwa na watu wajinga kama wewe
Ndugu yangu, kuna watu huishi gizani wakati wote. Wewe ni mmoja wao. Kumbuka njama anazozitumia Lissu sasa ndo mbinu hizohizo imekuwa ikizitumia CHADEMA kama chama inapopambana na CCM ama mambo mengine. Ni uongo na hadaa. Lissu hajamsema Mbowe lolote, amejisema yeye zaidi kuliko alivyomsema Mbowe. Maana kila anacholalamikia yeye mwenyewe amekifanya tena amekilinda tena amekisimamia. Lissu hakuna namna anaweza kuuzwa kwetu kama mwana mabadiliko. Ni mtu mpuuzi sana mwenye ego kubwa asiyejali maisha ya wengine. Baada ya kuwaharibu wengine, zamu yake naye imefika. Itimie haraka
 
Mbowe anaendesha chama kienyeji idara ya pesa yupo mwenyewe katibu mkuu wala kiongozi yeyote hasogei kitengo cha pesa za chama, hata kuwe na ufisadi viongozi wengine hawatahusika, hakuna mtu mwenye Akili Timamu atamwelewa mleta mada na ana Bahati kala pesa za mbowe mapema, na asingekuwa kala mbowe asingemlipa baada ya kusoma majibu yetu humu
Muulizeni Lissu alikuwa wapi miaka yote haya yakitokea. Mnajitoa akili kana kwamba Lissu siyo sehemu ya uongozi wa juu wa CHADEMA? Anahusika na kila tuhuma anazotoa sasa kwa unafiki. Yeye ndiye aliukumbatia mfumo anaoulalamikia sasa. Tena akitumia kuaminika kwake kama Mwanasheria kuwanyamazisha na kuwaaminisha watu uongo. Kama anasema Mbowe amekula ruzuku, wamekula pamoja. Kama ni kufukuza wapinzani wa Mbowe ndani ya Chama, ni yeye alikuwa anasuka na kusimamia mipango hiyo na yuko on record. Hakuna mtu aliyesimamia ufisadi ndani ya Chadema kuliko Lissu.
 
Nimeona mchakato huu usipite bila kutoa neno japo dogo kwa kuanzia.

Kwa mambo aliyofanya na kusema mpaka sasa, kuna jambo moja pekee ambalo ni muafaka kwa Tundu Lissu nalo ni Kufukuzwa CHADEMA.

Kwetu sisi tunaomfahami hasa maisha yake nje ya media, tunajua kuwa ni Muongo na mjanjamjanja sana. Amedanganya kila kitu. Wakati anajua kila kilichotokea CHADEMA ikiwa ni pamoja na mambo ya kihalifu, Lissu hawezi kujitenga na upuuzi wa CHADEMA.

Kwa wasiokumbuka, Lissu alishabikia vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa mkuu wa wilaya wa kike na wahuni wa CHADEMA. wakati huohuo alisimamia waziri mmoja wa leo (hakuwa waziri wakati ule) kutekwa Nyara na wahuni wa CHADEMA.

Lissu amesimamia maamuzi yote ya kuwafukuza na kuwaaibisha waliojaribu kugombea uenyekiti huko nyuma akiwa mwanasheria mkuu wa Chama akifikia kuwatuhumu kwa uhaini dhidi ya chama.

Ni yeye aliyetetea mafisadi wakubwa walipoanza kufikishwa mahakamani wakati ule na akageuka mtetezi wa mafisadi.

Lissu alihusika kuficha taarifa za wanachama kukituhumu chama kuhusika na ajali ya kada aliyekuwa amejipenyeza Chadema kikachero lakini wakamgundua na kumuwahi.

Naam, Lissu amekuwa katili na asiye na Roho ya utu hata kidogo. Alishangilia kifo cha Mwenyekiti wa CCM kilipotokea.

Binafsi sina maslahi na nani anaweza kuwa mwenyekiti. Mimi natamani Lissu naye sasa apitie kile ambacho yeye mwenyewe aliwapitisha wenziye. Afukuzwe uanachama wa Chadema haraka na bila huruma.
CCM mbona mnamwogopa sana Mbowe na Lissu.
 
Kama mtu ninayemfahamu maisha yake ya Udanganyifu. Lissu siyo dikteta uchwara bali ni dikteta kamili. Wote waliowahi kuwa karibu naye kiuongozi wanalifahamu hili. Sidhani kama wana Chadema sasa wanataka kutawaliwa na Mr.Haambiliki. pili Lissu hana Any policy accomplishment wala hana maono yoyote wala msimamo wa kisera. Malalamiko tena ya kinafiki hayawezi kuongoza chama. Kama anadanganya kwenye mambo yanayofahamika itakuwaje kwa yasiyofahamika?
Naomba kukuuliza kitu, Jos, kama target ya Chadema ni kushika dola, Lissu ndie the one and only mwenye uwezo huo, huoni kumchafua Lissu kwa maovu yake ndani ya Chadema, pia unakichafua chama na unamchafua Mbowe?. Kati ya wewe na bosi wako Rwaka, nani anaijua Chadema zaidi?. Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!
Mbona yeye kanyamaza, wewe kumsagia Lissu kunguni unapata nini?.
P
 
Mkuu Jose, @Joseph Ludovick , kwanza asante sana kwa wewe kutia neno, jf ya sasa ina madogo wengi ambao hawakujui wewe ni nani na ulikuwa nani Chadema, wala hawajui roles ulizokuwa una play Chadema ndio maana wanakubeza humu, usiwajali, sisi wa long time tunakufahamu, tunakuheshimu na hatuwezi kupuuzia hoja yako yoyote kwasababu tunajua ulikuwa jikoni, madogo humu hawakujui!. Ila wewe kutaka Lissu afukuzwe Chadema isije kuwa ni muendelezo wa zile hasira za Lissu kutoa siri za ndoa yako
Mkuu paschal mayalla kwa kuchukua muda wa kutosha na kusoma andiko langu kwa karibu na kufollow up. Nakufahamu kwa umakini mkubwa. Lakini nimeshangazwa tukio ulilorejea kwamba linaweza kuwa sababu za mimi kuwa na hasira na Lissu. Mimi nina HASIRA kubwa na Lissu lakini haitokani na hicho kisa chake cha uongo kama kawaida yake. Nimeshangaa umenukuu andiko ambalo nilikanusha madai yake lakini uka affirm kana kwamba alichosema kilikuwa kweli.

Naomba kuheshimu maoni yako, nakushauri kwa vile wewe ni an inside man, andaa tuu hati ya mashitaka, list down makosa yote ya Lissu na ushahidi wake, mpelekee KM JJ.Mnyika, Chadema itaitisha fasta ile kangaroo court yake ya CC na kumfukuza Lissu fasta, na huo ndio utakuwa mwisho wa Lissu ili Mbowe apite bila kupingwa. Hili likifanyika tutamshauri Lissu akubali tuu yaishe, akubali kufukuzwa arejee zake Ubelgiji au aende Marekani kuungana na familia yake, aiche Chadema salama waendelee na Sultan wao kwa amani.
Maoni yako hapa yanasikitisha. Kwanza hauamini kama CHADEMA inaweza kufanya maamuzi yake, ukiita Kamati kuu a cangaroo court, lakini pia ukionyesha kuwa against Mbowe. Hii inakupeleka moja kwa moja kuwa surrogate wa Lissu. Kama nimekosea nisahihishe mkuu wangu. Akifukuzwa sasa mtasema wamemfukuza maana wameogopa atashindwa ichaguzi. Ngoja ashindwe kwanza ndiyo sasa aliwe kichwa.
Hii maana yake na wewe pia unayajua mambo ya kihalifu ya Chadema, kujua uhalifu na kutouripoti ni kosa la jinai!. Mimi kama mwandishi wa habari, baada ya kuujua uhalifu wa Chadema, niliuandikia makala na kuuzungumza humu Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba! wewe baada ya kuujua uhalifu wa Chedema je ulifanya nini kingine chochote zaidi ya ile video yako ya Bukoba Boy kwenye Youtube?.
Naomba kukuuliza, baada ya bandiko lako hili CHADEMA imchunguze Mohamed Mtoi , mara mlengwa alikufa kwa ajali TANZIA - Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali
je ilikuwa ni ajali ya kawaida au kama ile ya Chacha Wangwe?.
Ndg yangu umepatwa na nini? Unakiri kuna video ya Bukoba boy halafu bado unadai niripoti uhalifu? Au na wewe ni kati ya wengi walioaminishwa na Lissu kuwa video ile haikuwa halisi wala kweli? Video ile haikuwa inafichua uhalifu? Hiyo ni moja tu. Yako mengine mengi niliyoripoti kifichoni na hadharani. Hata hapa JF nilishaandika mengi mno ya uhalifu huo. Tatizo watu wa aina ya Lissu walikuwa wakiyapinga nanyi mkiwaamini. Ulitaka nifanyeje zaidi.
Umesema wewe ni mwanaHabari. Nini kilikuzuia kufanya mahojiano na mimi kwa muda wote huo wakati ukijua nimehusishwa kwenye masuala haya ninayokuwa nayasema kila mara? Au nawe ni kati ya Genge la wale waandishi wanaoamini kwamba Chadema inasingiziwa kwa kila kitu? Nimekwishasema na naendelea kusema kila nikipata nafasi na ninapoona inafaa. Waandishi wa Habari wengi wakiwa machawa wa wanasiasa wa pande zote hawako interested na ukweli bali matumbo yao. Ni kujisumbua kuwategemea kwamba watatoa habari zenye maslahi ya umma.
Juu ya kifo cha Mtoi waulize Mbowe na Lissu ndiyo wanaweza kujua majibu.
Duh...!, kumbe Chadema wanateka nyara?!. Hii ndio nasikia leo, ni waziri gani huyo alitekwa nyara na Chadema leo ni waziri na anawachelea magaidi?.
Aidha nimestushwa kwamba haujui kuwa CHADEMA ya Lissu na Mbowe huwa wanateka watu..inashangaza sana kwa sababu matukio ya utekaji Chadema yapo muda mrefu. Hii inakuonyesha wewe ni mtu gani na upo upande gani. Wewe ndiye haukujua utekaji Nyara wa aliyekuwa msaidizi wa Dr.Slaa? Akafungiwa siku kadhaa na kufanyiwa matendo ya udhalilishaji wa utu? Haijui wewe kisa cha kutekwa na CHADEMA mtu anaitwa Joseph Yona na amekuwa akisema yeye mwenyewe na akina Lissu wakidiscredit account yake kwa faida ya uuaji wao? Haujui wewe aliyoandika Dr.Slaa kwenye kitabu chake cha Nyuma ya Pazia?......umenishtua mkuu. Kama ni chuki kwa uliyemwita "Sultani" basi imekupofusha na kama ni mapenzi kwa "mkombozi" nayo yamekupofusha vilevile.
Umeongelea "Karma" na umekubali kuwa nawe uliwaambia, naamini unakubali kuwa na Lissu ni mmoja wao. Sasa wataka kuibishia Karma? Wacha iwale. Wacha Lissu naye aonje kile aliwafanyia wenzake, namely KUFUKUZWA kwenye Chama.
 
Nimeona mchakato huu usipite bila kutoa neno japo dogo kwa kuanzia.

Kwa mambo aliyofanya na kusema mpaka sasa, kuna jambo moja pekee ambalo ni muafaka kwa Tundu Lissu nalo ni Kufukuzwa CHADEMA.

Kwetu sisi tunaomfahami hasa maisha yake nje ya media, tunajua kuwa ni Muongo na mjanjamjanja sana. Amedanganya kila kitu. Wakati anajua kila kilichotokea CHADEMA ikiwa ni pamoja na mambo ya kihalifu, Lissu hawezi kujitenga na upuuzi wa CHADEMA.

Kwa wasiokumbuka, Lissu alishabikia vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa mkuu wa wilaya wa kike na wahuni wa CHADEMA. wakati huohuo alisimamia waziri mmoja wa leo (hakuwa waziri wakati ule) kutekwa Nyara na wahuni wa CHADEMA.

Lissu amesimamia maamuzi yote ya kuwafukuza na kuwaaibisha waliojaribu kugombea uenyekiti huko nyuma akiwa mwanasheria mkuu wa Chama akifikia kuwatuhumu kwa uhaini dhidi ya chama.

Ni yeye aliyetetea mafisadi wakubwa walipoanza kufikishwa mahakamani wakati ule na akageuka mtetezi wa mafisadi.

Lissu alihusika kuficha taarifa za wanachama kukituhumu chama kuhusika na ajali ya kada aliyekuwa amejipenyeza Chadema kikachero lakini wakamgundua na kumuwahi.

Naam, Lissu amekuwa katili na asiye na Roho ya utu hata kidogo. Alishangilia kifo cha Mwenyekiti wa CCM kilipotokea.

Binafsi sina maslahi na nani anaweza kuwa mwenyekiti. Mimi natamani Lissu naye sasa apitie kile ambacho yeye mwenyewe aliwapitisha wenziye. Afukuzwe uanachama wa Chadema haraka na bila huruma.
Mkuu, siku nyingi sana kiongozi.

Karibu tena JF.
 
Akifukuzwa watasema Mbowe kaogopa sanduku la kura, huyu aachwe apate kura 7 zake kwanza akili imkae sawa.
 
Naomba kukuuliza kitu, Jos, kama target ya Chadema ni kushika dola, Lissu ndie the one and only mwenye uwezo huo, huoni kumchafua Lissu kwa maovu yake ndani ya Chadema, pia unakichafua chama na unamchafua Mbowe?. Kati ya wewe na bosi wako Rwaka, nani anaijua Chadema zaidi?. Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!
Mbona yeye kanyamaza, wewe kumsagia Lissu kunguni unapata nini?.
P
Nianze kusahihisha makosa kwenye bandiko lako hili.
1. Umejiongoza vibaya kudhani Lissu is the only one. Imani hii ni sawa na wanaoona Mbowe is the only one kuwa mwenyekiti.
2. Simchafui Lissu kwa lolote bali nasema alivyo na kuonyesha kuwa sasa anatumia uongo kutaka kushika madaraka ya Chama.
3. Mimi simtetei Mbowe wala Chadema kwa lolote. Ninaposema Lissu ameshiriki kila kitu anachopinga sasa huko siyo kumtetea Mbowe. Wala siyo kuichafua Chadema
4. Ulihemkwa kusema hatma ya CHADEMA iko mikononi mwa Lwaka. Alishaondoka Chadema na bado inadunda. Taasisi ni kubwa kuliko mtu yeyote. Mimi mwenyewe niko kimya. Sijasema lolote damaging kwa CHADEMA ama to that effect. Nyie waandishi kwa miaka 11 mmegoma kunihoji wala kunipa platform. Nyie waandishi kwangu mimi ni sehemu ya maadui wa umma. Kama Lwaka amekaa kimya ni maamuzi yake na mimi kukaa kimya ni maamuzi yangu. Siku nikiamua kuongea nitaongea. Haya ni rasharasha tu.
5. Swali la mimi na Lwaka nani anaijua vizuri Chadema halina jibu la moja kwa moja. Katika taasisi kuna level za taarifa siyo kila mtu anaweza kuaccess kila kitu. Wakati kwa kawaida kiongozi wa juu anategemewa kuwa na taarifa nyingi, lakini inawezekana kuna taarifa yeye hana ila juniors wanazo. Mfano kuna wakati Viongozi wa Chadema walikuwa hawapokei taarifa kutoka kwa Lwaka bali kwa wasaidizi wake.........
MImi simsagii Lissu Kunguni. Nimeamua kutoa mchango wangu kusaidia umma wamjue yukoje ili wafanye maamuzi kwa ufahamu (informed decision). Huyu ni mtu Katili asiye na ubinadamu kwa kipimo chochote kile. Leo eti anajilizaliza anaonewa. Kama wanaweza wamuonee tu. Akome
 
Back
Top Bottom