Mnashida sana nyie, nimeshasema achaneni na tabia za kukariri kila kitu bila kutumia akili zenu, hiyo itawasaidieni kuwa salama.
Hebu rudia kusoma ulichokiandika.
 
Jeiwii mbona mnatazama tu huu uonevu kwa raia wema wa nchi hii,wanaotetea wenzao dhidi ya ukandamizwaji wanaofanyiwa. Tena hawavunji Sheria za nchi ila polisi ndio wanaokiuka katiba na Sheria. Tunawaomba JWTZ mtusaidie raia wa nchi hii. Tumechoka kunyanyaswa ndani ya nchi yetu. Maadui sio lazima watoke nje ya mipaka ya nchi yetu! Tumegundua maadui wabaya zaidi wapo ndani ya mipaka. Kweli Bora wakoloni wazungu warudi kututawala kuliko kutawaliwa na hawa viongozi wanaotunyanyasa na kuharibu nchi kiasi hiki. Ee Mwenyezi Mungu tusaidie.
 
Hii nchi ina watu waajabu sana Jana niliwasikia wakiomba wakamatwe,wapigwe risasi na wakajinadi kwamba hawaogopi mtu na hawataondoka Barabarani.
Kwa ufupi waligoma kuondoka barabarani.

Leo tunaambiwa wamekamatwa kosa halijulikani na wameonewa sana wale mabingwa waliosema hawezi kufanywa lolote kwakuwa wana nguvu!

Siasa za namna hii sizipendi kabisa pamoja na kwamba siwapendi CHADEMA hasa baadhi ya viongozi wao lakini pia sioni CHAMA kinachoweza kutoa suluhisho la matatizo ya wanachi ingawa hakuna ubishi kwamba huwezi kuwaridhisha wanadamu wote.

Suluhu kije CHAMA kipya chenye watu wapya wenye maono na Sera pendwa angalau asilimia 90.
 
Kama ni kweli, basi hakutakuwa na jipya. Tutakuwa tunaendelea kushuhudia uhayawani wa watawala.

Hayo huwa yanatokea wakati waovu na wavunjaji wa sheria na katiba wanapopewa kazi ya kusimamia utiifu wa sheria na katiba.
Tatizo mmegoma kuacha kuwaza Bandari, Sasa Lissu lazima asaidie muisahau bandari kama inachukuliwa kwa utaratibu unaokubalika na wengi ama hapana!

Kalagha bao!
 
Sawa, hawa wakimkamata, hiyo haijibu hoja....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Nimekusikia Muhifadhi uchwara.

Ongezeko la watu ni Ngoro ngoro pekee?

Use common sense.

Just incase... Unataka kuzungumzia uhufadhi njoo ukiwa umekamilika... Yellowstone conservation doesn't work with NCAs.
We can't do things the way Americans does. Hivi Yellow kuna endangered species kama tembo,chui na faru?
 
Mnashida sana nyie, nimeshasema achaneni na tabia za kukariri kila kitu bila kutumia akili zenu, hiyo itawasaidieni kuwa salama.
Hebu rudia kusoma ulichokiandika.
Nilijua tu majibu yako utatukana tu kwasbb you are parochial huna hoja zaidi ya matusi
 
We can't do things the way Americans does. Hivi Yellow kuna endangered species kama tembo,chui na faru?
Yes. na kama hatufanyi kama Americans solution sio kuwahamisha wamasai kwa excuse ya uhufadhi.

Wamasai kwa namna ya pekee wana Co exist na ecology ya NCA, hakuna endangered spp ambae anawindwa kwa namna yeyote na wamasai, tena wao ndio wenye interests na indigenous knowledge ya conservation ya hizo endangered big mammals.

Kuwaondoa Wamasai haisaidii kabisa ku preserve NCA.. ni hisia za wahifadhi uchwara kuliko sayansi.
 
..
 
Nilijua tu majibu yako utatukana tu kwasbb you are parochial huna hoja zaidi ya matusi
So, ukionacho hapo ni matusi? Nimeshaandika, acha tabia ya kujariri utaishia kujipotosha kwenye kila kitu.
Grow up it, zitumie akili usikubali kichwa chako kiwe store ya tafsiri na misemo ya wengine.
 
Ni Vigumu sana kutenganisha hili jeshi la polisi na siasa
 
Utii bila shuruti ni kitu kidogo sana. Hata nyinyi CHADEMA kama mtabahatika kuchukua uongozi wa nchi mtataka maagizo yenu yatekelezwe.

Maasai deserve a better life outside the Ngorongoro area where they are mixed with wild animals. Let us support the Government initiative to re-settle then in Handeni where they will live a decent life like other Tanzanians. Say #NoToPrimitiveSocieties
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…