Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu alikuja CHADEMA ikiwa na wabunge zaidi ya 50, anaondoka, ikiwa na Mbunge 1

Wananchi ndio wenye maamuzi kama ulivyosema. Ila kwa sasa hata viongozi wa upinzani wapige kelele vipi kama asilimia kubwa ya wananchi wana furaha na amani na mfumo mabadiliko bado hayawezi kuwepo.
Lingine ni upinzani wenye malengo na upinzani imara kwa maslahi ya nchi. Chadema walikua imara sana hadi 2015, walijenga heshma kubwa na uaminifu mkubwa sana kwa watanzania, walihubiri vitu vya msingi vilivyogusa maslahi ya wananchi na wananchi wake ambavyo hakuna chama kilikua kinafanya.
Kitendo cha chadema kukusanya na kuyatetea yale maovu yaliyokua yanafanywa na ccm ndio kilichowafikisha wananchi njia panda kuona heri ccm inayopiga vita ufisadi kuliko chadema inayosafisha mafisadi.

Ukiamua kuwa mpinzani mwenye mafanikio lazima uache vile vibaya watawala wanavyofanya na ufanye vile vile vizuri ambavyo chama tawala hawafanyi

Unakiamini kabisa ulichoandika hapa au ni juhudi tu za kuwashinda wapinzani wako katika mdahalo. Sidhani kama mtu anayefuatilia undani wa siasa za Tanzania kidhati kabisa anaweza kupata mtazamo rahisi kiasi hicho.

CHADEMA wana matatizo na masula makubwa ya kushughulikia. LAKINI si hayo uliyoeleza. Umeandika kirahisi mno.

Na kuhusu CCM, hakuna mpambanaji na ufisadi anayetangulia kuzima nyenzo za uwazi/transparency ndipo aendeshe mapambano hayo. Jiulize kwa nini CCM inang’ang’ania kuendelea kuwa katika mfumo dola? Makundi yote hata yakizozana namna gani yanaishia kuelewana kwenye “ulazima” wa kuhakikisha chama kinabakia kuwa chama dola. Unafahamu kitu kinachoitwa KLEPTOCRACY?

Well dear, stay blessed in whatever you really believe in and working for.
 
Kwaiyo mtaalam wa sheria ameingiza CDM kwenye mtaro na kasepa zake.
 
Hivi ukiwa CCM unakua na matatizo ya mtindio wa ubongo by default?
Mkuu,nimeongea na rafiki zangu wenye hospitali na vituo vya afya pamoja na madaktari tuanze kuwachunguza kwa siri hawa wana CCM ili kujua kulikoni kwa ajili ya kuliokoa taifa na kizazi cha mtindio wa ubongo kijacho.
 
Kwani sasa wananchi ndio wamekuwa na imani na serikali/ccm? 2/3 ya watanzania wamegoma kupiga kura, je hiyo imani inatoka wapi?
Ku"abstain" kitu si kukikataa wala kukikubali!

Hiyo 2/3 inaweza kuwa hakupata nafasi ya kupiga kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo vituo walivyojiandikisha kuwa mbali ama kufanya makosa kwa kufikiria kuwa mgombea wao atashinda hivyo hakuna haja kupiga kura( ingawa yawezekana wengi wao walipatia kufikiria kwao huko na wachache wakakosea). Zipo dhania nyingi kuhudu 2/3! Hivyo siyo sahihi, objectively, kudai hiyo 2/3 wamegoma kupiga kura!
 
"Anayeamini kwamba tar 27 na 28 kulikuwa na uchaguzi inabidi apelekwe mirembe" - Mbowe
Nad
"Anayeamini kwamba tar 27 na 28 kulikuwa na uchaguzi inabidi apelekwe mirembe" - Mbowe
Mimi binafsi naamini kuwa asiyeamini kuwa Oktoba 28 tulikuwa na uchaguzi inabidi siyo tu kwamba apelekwe Mirembe Bali aombewe ili mapepo yanayosumbua kisaikoloji yaondoke
 
Ku"abstain" kitu si kukikataa wala kukikubali!

Hiyo 2/3 inaweza kuwa hakupata nafasi ya kupiga kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo vituo walivyojiandikisha kuwa mbali ama kufanya makosa kwa kufikiria kuwa mgombea wao atashinda hivyo hakuna haja kupiga kura( ingawa yawezekana wengi wao walipatia kufikiria kwao huko na wachache wakakosea). Zipo dhania nyingi kuhudu 2/3! Hivyo siyo sahihi, objectively, kudai hiyo 2/3 wamegoma kupiga kura!
Ni hivi tuko hapa hapa nchini, na watu wanaongea kabisa hawana muda wa kupiga kura kwani matokeo hayaaminiki. Ni kuwa watu wamepoteza imani zoezi zima la uchaguzi. Ingekuwa 1/3 hawakupiga wangalau utetezi wako ungekuwa na mashiko na sio kinyume chake. Kwa maneno marahisi, uchaguzi kwa sasa unafanyika ili watawala kuhalalisha kukaa madarakani kisheria, lakini sio kupata uhalali wa umma kama inavyopaswa kuwa, ndio maana unaona tume ya uchaguzi kuwa biased, watu kupita bila kupingwa, kura za wizi na umwagaji wa damu ili chama tawala kuendelea kukaa madarakani.
 
Wadau,

Nimekaa nikawaza sana.

Nimeanza kuhisi kuwa it's very possible Bwana Lissu akawa ni mtu aliyetumwa kuja kuua upinzani hasa CHADEMA.

Nimetafakari kauli zake na misimamo yake, ni dhahiri kabisa mtu yule lengo lake sio kujenga upinzani Bali kubomoa

Sasa hivi yeye mwenyewe ameondoka amerudi Ulaya na nina uhakika hatorudi Tena kwa miaka hii ya karibuni

Amegoma CHADEMA kuchukua viti maalum, sawa ila Alitakiwa kujua kwa siasa za tanzania ya Sasa hivi kukosa platform ya kuongea ni kosa kubwa sana hasa kwa chama kama Chadema.

Yan hapo kitakuwa kimekufa kabisa. JPM sio JK ambaye alikuwa anaweza kuwaita Ikulu na kuongea; mzee Magu hayupo hivyo.

Ukijaribu kuwaza kiundani utagundua kabisa lengo la Tundu Lissu ni CHADEMA ifutwe, then yeye na familia yake atakuwa zake Ulaya.

Huwezi kubishana na Serikali hasa serikali za Kiafrika.

Mimi kwa maoni yangu naona kabisa kuwa bwana Lissu ni pandikizi ambalo lengo lake ni kuja kuizika CHADEMA.
 
Dini na siasa, bora Nini?

Gwajima: Unanichanganya, nipe miaka mitano nitafakari jibu la kukupatia.

Sijui kama nimetembea kwenye mada.
 
You must be wrong... Wahenga Walipata Kusema “Hauwezi Kujisaidia Kariakoo Mchana kweupe Ukatoka Unapiga Miruzi Mikono Mfukoni Huku Ukijiaminisha Watu Hawakuoni. We're naked brother "Dunia ya Sasa ni Kijiji" Zoezi tulilolimaliza dunia ilituona tukiwa "Uchi" Stop Joking "TAL" was for the purpose na hakuwa anatania.

Ameshaondoka tuongee tu ya kwetu kwani sio Threat Kwa muda huu Mfupi. Nadhani madhara ya kujisaidia K'koo mchana Kweupe tutayaona mda si Mrefu, Tujipe muda "Tunaenda Kubinywa"..Daaah!!!!
 
Mackanackyyy,

Unajiona mjanja Sana au sio?

Vyama vyote vya upinzani lazima viwe na platform ya kuongea au kuonekana

Magu alisema hakuna siasa kwa miaka mitano iliyopita mlifanya nn?
 
CHADEMA ikifa wewe unapungukiwa na nini na wakati mmeshinda ubunge kwa 100% na ndiyo ilikuwa lengo lenu?
Hizo ndio akili kama za lisu
Anataka watu wagome, waandamane, wakati huo yy amekaa ubalozini anakula hewa safi

Na yeye Lissu Ana akili kama zako kuwa CHADEMA ikifa yeye hapati hasara yoyote
 
Mbona kama anawasumbua sana huyu lissu? Bado hamuamini kama kaondoka? Kuweni na amani jamani wana Lumumba,,
 
You must be wrong... Wahenga Walipata Kusema “Hauwezi Kujisaidia Kariakoo Mchana kweupe Ukatoka Unapiga Miruzi Mikono Mfukoni Huku Ukijiaminisha Watu Hawakuoni. We're naked brother "Dunia ya Sasa ni Kijiji" Zoezi tulilolimaliza dunia ilituona tukiwa "Uchi" Stop Joking "TAL" was for the purpose na hakuwa anatania. Ameshaondoka tuongee tu ya kwetu kwani sio Threat Kwa muda huu Mfupi. Nadhani madhara ya kujisaidia K'koo mchana Kweupe tutayaona mda si Mrefu, Tujipe muda "Tunaenda Kubinywa"..Daaah!!!!

JPM alikataa chama chochote kufanya siasa kwa miaka mitano je hiyo dunia ilisema nini? Au ilifanya nn?

Wakina Mbowe walikuwa jela, je hiyo dunia ilikuja kuwatoa?
 
JPM alikataa chama chochote kufanya siasa kwa miaka mitano je hiyo dunia ilisema nn? Au ilifanya nn?

Wakina Mbowe walikuwa jela, je hiyo dunia ilikuja kuwatoa?
Muulize hili: CCM ilishinda viti vingapi kiuhalisia? Jee Jandoni hawajakoromewa kuhusu unafiki? Hawajasonywa na kukoromewa msithubutu kamwe?. Mahasira na tahadhari kibao za nini?
 
Hivi posho za buku 7 bado zipo kweli?
Kaka jaribu kuwaza kwa kina, utaungama na mimi tu

Mwanasiasa ambae hataki chama chake kisikike lengo lake ni nn?

Me nilitegemea angeruhusu wabunge vyuma waende bungeni kule ndio sehem ya kupaza sauti

Sasa kwa kujitoa kwa kila kitu hizo siasa anaenda kufanyia ulaya?
 
Kwanza ungejiuliza kwanini ccm waliiba kura na kutengeneza kura feki
Kaka jaribu kuwaza kwa kina, utaungama na mm tu

Mwanasiasa ambae hataki chama chake kisikike lengo lake ni nn?

Me nilitegemea angeruhusu wabunge vyuma waende bungeni kule ndio sehem ya kupaza sauti

Sasa kwa kujitoa kwa kila kitu hizo siasa anaenda kufanyia ulaya?
 
Back
Top Bottom