Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Wananchi ndio wenye maamuzi kama ulivyosema. Ila kwa sasa hata viongozi wa upinzani wapige kelele vipi kama asilimia kubwa ya wananchi wana furaha na amani na mfumo mabadiliko bado hayawezi kuwepo.
Lingine ni upinzani wenye malengo na upinzani imara kwa maslahi ya nchi. Chadema walikua imara sana hadi 2015, walijenga heshma kubwa na uaminifu mkubwa sana kwa watanzania, walihubiri vitu vya msingi vilivyogusa maslahi ya wananchi na wananchi wake ambavyo hakuna chama kilikua kinafanya.
Kitendo cha chadema kukusanya na kuyatetea yale maovu yaliyokua yanafanywa na ccm ndio kilichowafikisha wananchi njia panda kuona heri ccm inayopiga vita ufisadi kuliko chadema inayosafisha mafisadi.
Ukiamua kuwa mpinzani mwenye mafanikio lazima uache vile vibaya watawala wanavyofanya na ufanye vile vile vizuri ambavyo chama tawala hawafanyi
Unakiamini kabisa ulichoandika hapa au ni juhudi tu za kuwashinda wapinzani wako katika mdahalo. Sidhani kama mtu anayefuatilia undani wa siasa za Tanzania kidhati kabisa anaweza kupata mtazamo rahisi kiasi hicho.
CHADEMA wana matatizo na masula makubwa ya kushughulikia. LAKINI si hayo uliyoeleza. Umeandika kirahisi mno.
Na kuhusu CCM, hakuna mpambanaji na ufisadi anayetangulia kuzima nyenzo za uwazi/transparency ndipo aendeshe mapambano hayo. Jiulize kwa nini CCM inang’ang’ania kuendelea kuwa katika mfumo dola? Makundi yote hata yakizozana namna gani yanaishia kuelewana kwenye “ulazima” wa kuhakikisha chama kinabakia kuwa chama dola. Unafahamu kitu kinachoitwa KLEPTOCRACY?
Well dear, stay blessed in whatever you really believe in and working for.