Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Mgombea Uenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amefunguka kupitia Twitter space jinsi alivyokusanya ushahidi wa kutosha kuhusu rushwa ya pesa za Abdul na mama yake kwa viongozi wa Chadema.

Ameeleza kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha CHADEMA aliyempatia ushahidi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo na aliyemsaidia kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya kamati kuu ya Chama cha CHADEMA kwa sasa ni Marehemu. Hata hivyo Lissu alikataa kumtaja Mjumbe huyo akidai kwamba haitasaidia kitu chochote.

Na alipoulizwa iwapo kifo cha Mzee Ali Kibao kinahusiana na tuhuma za pesa za Abdul aliomba asilizungumzie Hilo kwa sasa.

Mifumo iliyoshindwa Burkina Faso, Ivory Coast, Tunisia, Misri, Mali..

Ni Mifumo ya nini? Android?
Unakebehi mfumo ukiwa nyuma ya keyboard,jitokeze upambane nao uone moto 😀😝
 
20241226_132152.jpg
 
Umeshaambiwa kuna uwezekano kwamba kulikuwa na mfumo ndani ya mfumo - pande mbili zenye nguvu zinazosigana kwenye mfumo uleule mmoja.

Jamaa anadai kwamba ndipo ukatokea mwanya wa kusukumiana kete mbovu kwa ushirikiano wa adui wa nje anayetambulika na ule mfumo ndani ya mfumo. Sijui inaeleweka hapo?

Unaposema JPM angejua nani aliyekuwa mastermind wa kumpoteza BS8 kwa sababu ya nguvu na intelligence aliyokuwa nayo, usisahau pia kwamba kuondoka kwake mara kwa mara kumehusishwa na njama zilezile za yeye mwenyewe kuondolewa (na akina nani hao?!). Please, think!!!
Ukinangalia situation ya BS8 hao akina nanii hakuwa na conflict ofinterest na wao, kwanza as long as hao kina nanii walikuwa na mgogoro na JPM kwao huyo BS8 ilikuwa ni karata dume kabisa kusaidia kwenye mashambulizi dhidi ya JPM
 
Lissu na Mbowe siwapendi lkn katika kutofautiana wao katika kipindi hiki natumia fursa kubaini yale ambayo nilikuwa nikiwaeleza ndg zangu wasukuma watu hawa ni hatari lkn mmoja ni hatari zaidi.

Nadiriki kusema Mungu amlaze mahali pema peponi Magufuli wetu hasa wazalendo mtu huyu alibalagazwa sana kabla na baada ya maisha yake hapa duniani
 



Tumia akili ...kwa sasa serikali ipo mikononi mwa watu walio mchukia jpm swali je mbona si mbowe wala ccm ya samia wanataka uchunguzi ufanyike kuhusu hicho kifo .....wewe hata samia umjui ni nani! Samia ana chuki kubwa sana na JPM ndiyo maana wamezuia kabisa jina lake kutajwa swali je kama jpm aliusika na kuua hao watukwa nini samia asinge sisitiza uchunguzi ili kumzihilisha kuwa jpm ni muovu tofauti na mbinu wanazo tumia sasa za kuzuia jina lake kutajwa
Kila zama na kitabu chake, ya wakati huu wa Samia yajadiliwe kwa wakati huu. Hapa tunazungumzia wakati huo wa JPM kwanini alishutumiwa yeye direct na akakaa kimya? Kila mtu alisikia vitisho vyake wazi wazi na kudhihirisha uhusika wake pasi na shaka.

Hayo ya Samia kumchukia au kutomchukia mimi sijui. Unapoona issue inatokea na wenye mamlaka wanalaumiwa/kushutumiwa ila wanakaa kimya fikiri nje box.
 
Mkuu, hoja yako inaeleweka vizuri sana. Lakini unaipa asilimia ngapi ya uhakika - 100%? Kama si 100% basi jua kwamba upo uwezekano wa hoja mbadala.

Ukisema uchunguzi haukufanyika, utakuwa unaongea bila ushahidi wowote kwa sababu mimi na wewe hatujui kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia - labda kama na wewe unajua siri zote za serikali.

Sidhani kama uko sahihi unaposema hakuna uchunguzi wowote uliofanyika, kwamba hakuna hata mtu mmoja aliyehojiwa. Hatuna uhakika 100% kuhusu hilo.

Kama kuna ukweli wa nadharia ya uwepo wa mfumo ndani ya mfumo, si ajabu matukio mengi haya-make sense kwa mwonekano wa juujuu.
Kwenye masuala yanayoteka hisia za mamilioni ya raia hasa mauaji na kupotea kwa wanasiasa au watu maarufu hizo case huwa hazipoi kirahisi. Pangekuwa na uchunguzi au kufikishwa mahakamani hata kwa sisimizi mmoja lazima vyombo vya habari vingetoa taarifa.
 
Bninapata picha kuwa na inaoneka maraisi wa ccm waliotangulia Bm, jk, walimuweka Mbowe kwenye circle zao

Sasa alipokuja kichwa ngumu magu akamtoa na kumtolea nje, akajalibu kumdhoofisha ili asijaribu kumkaribia

Jpm Akiamini kwa siasa zake za udikteta
Udikteta ni nini?
hamuhitaji mbowe anajitosheleza

Alipokuja mama abdul imebidi amrejeshe kwenye circles zake

Mama ameenda zaidi ya watanulizi wake amemwaga fungu la uhakika

Abdul ni masterminder
 
evidence, evidence, evidence...... anatoa revelations tu bila ushahidi.. kama akina Mbowe wangelikuwa kama yeye, wangelibwatuka tu na kumvika uongo kama anavyofanya yeye........

Fine sasa anashindwa nini kumuondoa Samia madarakani, kinamzuia nini ambacho atakipata kwenye uenyekiti?
Hizi pumba zako hazihitaji majibu, endelea na ujinga wako.
Inamaana hujui nguvu ya mwenyekiti juu ya mjadala au maamuzi ya kikao chochote anachokiongoza?
Au hujawahi kuhudhiria kikao chochote?
 
Lisu anajua anachofanya! Lisu ni mropokaji ila anaropoka vitu ambavyo ni sahihi yaani hana uwezo wa kutunza siri li friji lake haligandishi. Anachosema sasa ndo ukweli wenyewe kwamba mauaji ya wanachadema yanafadhiliwa na mamlaka ya juu ndani ya Chadema yenyewe.

Kuna wanachadema wamepotea wengine hawakuwa hata na athari zozote kwa serikali hata wananchi wengi wamewajua baada ya kutangazwa kuwa wamepotea au wamekua akiwemo huyo babu Kibao.

Hao watu watakuwa walionekana threat kwa mtu au kundi flan ndani ya CHADEMA na kundi hilo likaamua kuwaondoa kikatili wakijua atakayesingiziwa ni serikali/usalama/polisi ila sasa ukweli unaanza kuonekana.

Yaani CHADEMA inaua Chadema
Acha ujinga, serikali inavyo vyombo vyake vya kubaini wahusika wa mauaji kama ingekuwa ina nia ya kuwapata.
Serikali inahusika moja kwa moja na inaweza kuwa inafanya kwa ushirikiano na huyu anayetajwa
 
Aiseee!

Ipo shida kubwa CHADEMA, naomba isiwe hivi ninavyofikiri.

Lakini, siasa za Tanzania ni hatari mno. Kama mtu anajijua hayuko tayari kuagana na nyonga ni vyema asijihusishe kabisa.

Chadema ni CCM B. Kama vilivyo vyama vingine kadhaa vya siasa.
Na toka vyama vingi imekuwa hivyo. Ni wale wale na agenda zao zile zile, wanawazingua wananchi tu
 
Wanaotekwa, Wanaouliwa Na wanaofanyiwa mambo ya Kinyama wote wanafanyiwa na Vyama vyao Ila Kisingizio mama samia na Serikali yake au Kisingizio Magu na Serikali yak..
Huu Ni ushahidi Kamili kwamba Chama Changu cha CCM Hakihusiki na Yote yanayotajwa Eeh Mungu nisamehe kwa Kuchukia Chama changu ns Kutamani Uongozi ubadilike..

Pia Lucas Mwashambwa Nisamehe Mdogo wangu Ukweli sasa Unaanza kidogo kidogo kufahamika
Kuwa Serikali haihusiki
Sasa kama hawahusiki kwa nini wasiruhusu uchunguzi huru?
Wanaogopa nini?
 
You've missed the point.

Uhusika wa wapinzani ni tuhuma za kushirikiana na system/dola/CCM/serikali kuteka, kutesa na kuua. Dola ndio wenye vyombo na mfumo wa utekelezaji. Kisha kuzuia uchunguzi na kupoteza ushahidi. Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kufanya utekaji na mauaji nchi hii kikabaki salama mbele ya serikali na vyombo vya dola.
Upo sahihi 100%
 
Kumbe ndiyo maana kuna watu, hata humu JF wamevimba midomo, macho, masikio hadi pua; na vidole kujipinda kwa kubonyeza 'keyboard' wakimlaumu Tundu Lissu kwa wanaouita wao "uropokaji".

Kumbe wanajua mabomu aliyo nayo Tundu Lissu na wanayo hofu kubwa kuwa atayalipua!

Uovu wa aina hii nao uwe ni sehemu ya kuwekeana siri viongozi?

Hovyo kabisa.
Mungu amlinde Lissu, kuna mengi nyuma ya pazia
 
Back
Top Bottom