Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024, jijini Dar es Salaam
Kiongozi wa kikosi cha mauaji dhidi yangu mwaka 2017 alikuwa Paul Makonda. Aliwaongoza wauwaji walionipigia risasi 36 Dodoma.” - Tundu Lissu
"Shambulio dhidi yangu (shambulio la Tundu Lissu kupigwa risasi) limetokea katikati ya majengo ya serikali wanayokaa Mawaziri, Naibu Spika Tulika akson kwa wakati ule (sasa ni Spika wa Bunge), Waziri Harrison Mwakyembe (aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo), Waziri wa Nishati wa wakati ule yeye alikuwa anakaaa juu na mimi nilikuwa nakaa chini" -Lissu
Pia soma:
- Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka
"Katika majenho ambayo yana ulinzi na yanakaa wakubwa (viongozi wa juu/waandamizi) eneo hilo lilikuwa sio tu lina ulinzi masaa 24 bali lilikuwa vilevile na kamera za CCTV, na kama mtakumbuka baada ya shamhulio hilo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma alikuwa anaitwa 'Mroto' alitangaza kuwa Polisi walikua wamepata ile picha za hiyo CCTV kamera iliyokuwa inatazama ile parking lot ambayo nilikuwa nimeshambuliwa" -Lissu
PIA SOMA
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali