Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,887
- 7,673
Nafikiri Mutungi ndio kachemka. Hakutakiwa kwenda kwenye media kutoa vitisho. Yeye kama mlezi wa vyama alitakiwa kuwaandikia chadema kuwaeleza mashtaka yao na wao Chadema kujibu mashtaka yao. Tabia ya mambo kama haya kuyapeleka mitandaoni hasa yanayoihusu Chadema Ofisi ya Mutungi imekuwa ikiifanya sana. Kunanbarua fulani ambayo ilizagaa sana mitandaoni iliyotoka kwa Msajili ambayo Chadema kupitia Mnyika waliwahi kulalamika kuwa ilianza kuzagaa hatankabla wao hawajaipokea. Barua nyingine ilikuwa ya hivi karibuni iliyozua malumbano kati ya Msajili na Ado Shaibu kwa niaba ya ACT.Huyo Lissu naye apunguze kiherehere...
Kwa sasa tension ya kisiasa ipo juu sana. Msajili kama mlezi wa vyama atumie njia za kitaalam na za kiuungwana kushughulikia mambo kuliko kuendelea kutumia Media kujifanya anaonya wakati pengine anafanya kazi ya chama fulani cha siasa kwa mgongo wa MSAJILI