Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amuunga mkono Maalim Seif Urais Zanzibar

Mbona unapagawa. Asante kwa kutambua kuwa 2021 - 2015 Zanzibar ACT Bara Chadema.

Usisahau kudondosha kura yako.👏👏
Hajui hoja kuu za Chadema na ACT ni katiba ya warioba ambapo inasema kutakuwa na serikali 3. Mpuuzi huyu achana nae
 
Mgombea Urais wa Tanzania Bara kupitia CHADEMA akiwa kwenye kampeni Zanzibar amesema Maalim Seif wa ACT-Wazalendo ndio sauti ya wazanzibari kwa miaka 35, hajawahi kubadilisha msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar, kuna kila sababu ya kuungwa mkono kwa msimamo wake

Amesema kuwa, "Kumuunga Maalim Seif mkono na ACT sio kuwasaliti watu wetu, ni kutambua ukweli ulioko wazi kwa kila mtu kwamba, hawa ni chama kinachoweza kuiondoa CCM madarakani"

Kwa hiyo mgombea wa Chadema Zanzibar atajitoa....
 
Ni fedheha kubwa kwa kiongozi anayetaka kuwa Mkuu wa nchi hoja yake kubwa ati ni kuiondoa CCM madarakani. INAFIKIRISHA.
Sasa kuna hoja kubwa kwenye uchaguzi huu zaidi ya hii??? Hakuna katiba mpya ya warioba bila CCM kutoka madarakani??? Hakuna uhuru wa Zanzibar bila CCM kutoka madarakani, Hakuna Uhuru, haki na maendeleo bila CCM kutoka madarakani!!!

Mnalo mwaka huu mataga 😂😂😀
 
Firauna aliondoka misri na yy alikua na jeshi Kali kushinda majeshi yote jee Huyu mungu wa chato asiondoke kwa sababu gani

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Hujanielewa. Hoja yangu si kumtetea kiongozi kwani hata huyo ataondoka na vyama vitabaki.

Hoja yangu, nini ataifanyia Tanzania baada ya kupewa ridhaa na siyo kunwondoa kiongozi au Chama. Kama nia ni kuiondoa CCM hata mapinduzi ni njia pia.
 
Sasa kuna hoja kubwa kwenye uchaguzi huu zaidi ya hii??? Hakuna katiba mpya ya warioba bila CCM kutoka madarakani??? Hakuna uhuru wa Zanzibar bila CCM kutoka madarakani, Hakuna Uhuru, haki na maendeleo bila CCM kutoka madarakani!!!

Mnalo mwaka huu mataga [emoji23][emoji23][emoji3]
Nimemjibu mwenye hoja kama yako. Kunakuwa na Chaguzi ili kuweka utawala wenye Sera/Mikakati mbadala si kwa lengo la kuondoana madarakani.
 
Mgombea Urais wa Tanzania Bara kupitia CHADEMA akiwa kwenye kampeni Zanzibar amesema Maalim Seif wa ACT-Wazalendo ndio sauti ya wazanzibari kwa miaka 35, hajawahi kubadilisha msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar, kuna kila sababu ya kuungwa mkono kwa msimamo wake.
Huu ni ulaghai wa kisiasa tu. Hili hata mtoto wa chekechea analijua kwamba Chadema Zanzibar hawana ushawishi wowote ule. Hawawezi kupata kura hata asilimia 1, kwahiyo suala la wao kumuunga mkono Maalim Seif hawapotezi chochote kile. Ni tofauti sana na ACT huku Bara, kuna maeneo wanakubalika, hivyo kumuunga mkono Lissu bila mkakati wowote ni kama wao watapoteza zaidi.

Tuliona 2015, Chadema walivyowatapeli UKAWA kwenye suala la urais na kuachiana majimbo. Mwisho wa siku wao ndiyo waliopata kura nyingi za urais na majimbo mengi na hivyo kupata ruzuku zaidi kuliko Vyama vingine vya Upinzani. Bahati nzuri, huu utapeli wanaotaka kuufanya Chadema Zitto anaujua. Ndio maana mpaka leo imeshindikana kuungana kwasabbu CDM wanataka kunufaika zaidi ili waimarishe SACCOS yao.
 
Nimemjibu mwenye hoja kama yako. Kunakuwa na Chaguzi ili kuweka utawala wenye Sera/Mikakati mbadala si kwa lengo la kuondoana madarakani.
Huwezi kuweka sera zako bila kipaumbele za kwanza cha kumtoa mpinzani wako mwenye ufedhuli mwingi kutumia
 
Huu ni ulaghai wa kisiasa tu. Hili hata mtoto wa chekechea analijua kwamba Chadema Zanzibar hawana ushawishi wowote ule. Hawawezi kupata kura hata asilimia 1, kwahiyo suala la wao kumuunga mkono Maalim Seif hawapotezi chochote kile. Ni tofauti sana na ACT huku Bara, kuna maeneo wanakubalika, hivyo kumuunga mkono Lissu bila mkakati wowote ni kama wao watapoteza zaidi...
Kajipange upya mwana Ccm. Lissu kawashika vibaya na pabaya sana mwaka huu. Na ukweli ni kwamba hamna namna kwake
 
Ndio mana ninaamini uchaguzi huu ni mwepesi sana. Yule mgombea wa Chadema urais wa zanzibar mtamwambia nini?
Kama mliyajua hayo kwanini mliacha mchakato uendelee?

Tusubiri mgombea wa Chadema atakaposema wanaChadema Zanzibar wampigie membe kura za ndiyo.
Chadema wana ushawishi gani Zanzibar? Huu ni utapeli tu wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom