Uchaguzi 2020 Tundu Lissu anajitutumua kuitumia Corona kisiasa lakini wapi!

Najua kazungumzia na mengine. Nimeyasikia.

Kilichonigusa zaidi ni Corona na ndicho nilichoamua kukizungumzia.

Mimi siyo kamanda nisiyeelewa mambo mepesi.
 
Mimi uncle wangu juzi kafariki singida kwa Corona yaani anazikwa juma nne. Wajinga wachache wanasababisha ndugu zetu kufa kwa ushabiki wa Siasa. Ngoja upoteze mtu ndiyo utajua Corona ipo
We jamaa una fiksi sana.

Anko wako kafariki juzi....Ijumaa, siyo? Halafu anazikwa keshokutwa Jumanne?

Hahahahaaaa.
 
Lissu yupo kwenye ziara ya kuona maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo alikuwa amelala, wenzie wanapiga kazi.
Yeye sio urais tu hatopata bali hata ubunge kule alikozaliwa hawezi kupata.
 
Nimepata kukitazama kipande cha video ambacho ameongea kuhusu hilo na ni dhahiri kuwa wewe haujapata kuielewa hoja iliyomo.

Corona si hoja hapo isitoshe corona ni suala la juzi tu hapa katika yale yaliyomo katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya tano.

Hoja iliyoko hapo ni kauli za Rais katika masuala mbalimbali ya kitaifa. Ndio maana amezungumzia pia suala la majanga ya kiasili kama tetemeko la ardhi n.k.

Hoja si corona wala natural disasters alizozisema bali hoja ni kauli za kiongozi kwa wananchi pale ambapo majanga hayo yanatokea.
 
Unaweza kutumia dawa ya kuharisha wakati hujahalisha?
Utavaa barakoa wakatu hakuna ugonjwa?
 

Uko sahihi, mleta mada kaichukua kauli ya Lissu out of context!

Theme pana ya Lissu haikuwa jinsi Magufuli alivyopambana na Korona, bali inahusu kauli zisizo na staha kwenye utendaji wake!

Kitendo cha jiwe kuifananisha Barakoa na titi la mtu lililokatwa ni sexism, si kauli ya staha na haimfai kiongozi wa nchi!.
 
Kamkosoa Magufuli kwa kuwaambia watu wasivae barakoa, ‘kwanza zinafanana na sidiria za wanawake’.

Sijui ni lini na wapi Rais alisema hivyo. Mnaojua mtanifahamisha.
Kama hukumsikia bora ukae kimya! Tafuta clips alipokuwa anafungua majengo kule Dodoma mwezi uliopita.
 
Mimi uncle wangu juzi kafariki singida kwa Corona yaani anazikwa juma nne. Wajinga wachache wanasababisha ndugu zetu kufa kwa ushabiki wa Siasa. Ngoja upoteze mtu ndiyo utajua Corona ipo
Pole sana mkuu ila kama unatudanganya hapa kwa manufaa ya kushinda mjadala basi ulaaniwe
 
Tundu Lisu akiwa kwenye jukwaa la Sera za CHADEMA apambanue na kupambana na sera za CCM, akipambana na Magufuli, hatamkwepesha ikulu, kwa kuwa CHADEMA isipoiweza CCM, ndio hivo Tena!
Kampeni hazijaanza hivyo siyo wakati wa kumwaga Sera huu!
 
Tundu ndiye mgombea mbovu toka Chadema ianzishwe
 
Hiyo clip nimeisikiliza sana na kuielewa sana na mimi actually ndo wa kwanza kuileta na kuianzishia mada hapa JF.
(Mada inayohusu ziara ya Lissu Muheza Tanga ipo hapa kwenye jukwaa la siasa)
Lissu hajadai kuwa Magufuli aliilinganisha barakoa na titi, kama ulivyodai wewe.

Unabisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…