Tundu Lissu Anakumbusha Uchaguzi wa Urais wa TAA Kati ya Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TUNDU LISSU AKUMBUSHA UCHAGUZI WA PRESIDENT WA TAA KATI YA ABDULWAHID SYKES NA JULIUS NYERERE 1953

Kila uchao tunakumbushana na kuazima ukurasa kusoma kutoka historia ambayo ilifutika.

Leo usiku katika kipindi cha ITV Dak. 45 Tundu Lissu akihojiwa na Mtangazaji Farhia Middle katika kujadili demokrasia alisema kuwa mara ya mwisho nafasi ya urais kugombewa katika TANU ilikuwa 1954 Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere walipogombea urais wa TAA.

Lissu amekosea mwaka.
Uchaguzi ule ulikuwa mwaka wa 1953.


View: https://youtu.be/KH2tQw7TYec
 
Abdulwahid Sykes alishindwa vibaya na huo ndio ukawa mwisho wake wa siasa za Kariakoo.
 
Uzuri tumejua, kumbe hakumuachia Nyerere bali alishindwa vibaya sana
 
Hajasema hivyo kasema uenyekiti akimanisha kwa sasa.. na kukumbishia nyuma 1954 neno rais halijatajwa
 
Uzuri tumejua, kumbe hakumuachia Nyerere bali alishindwa vibaya sana
Naby...
Kitabu cha Judith Listowel ndicho kilichoeleza kuwa Abdul Sykes na Nyerere waligombea nafasi ya urais wa TAA mwaka wa 1953.

Judith Listowel ndiye anaeeleza uchaguzi huu na ndiyo aliyesema kuwa Nyerere alipata ushindi mdogo.

Angalia kitabu chake, ''The Making of Tanganyika,'' (1965) uk. 221:
''Nyerere was elected by a small margin...''


 
Ushindi ni ushindi mraaa,,,kikubwa hakuachiwa kama stori zako za kwenye kahawa unazotakaga tuamini
 
Hapana. Huo ulikuwa ni mpango maalum uliosukwa na Waislam.

Hiyo kura ingefanywa inavyotakiwa, nyerere, wakuja, angeshindwa vibaya sana na mtoto wa mjini na mwenyeji wake Abdul Sykes.

Mipango mingi ingeharibika.
Sababu za kufanya hivyo zipo nyingi, sikiliza video hiyo juu hapo na msome Alama Mohamed Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…