Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Da very painful Sana, yoyo kwa yote MUNGU ni mwema siku zote amtangulie,Sina mengi zaidi ya uzuni ulioniingia kwa Kasi ya hajabu moyoni
 
Imagine taifa lingekuwa mikononi mwa huyu puppet ingekuwaje?

Ameamua kurudi kwao Brussels!
Taifa liko chini ya Magufuli na wapwa zake mbona ndiyo maisha yamezidi kuwa mabaya kuliko muda wote tangu tupate uhuru?
 
Silencing the robberers at the very scientific way can be the very best way forward!! If this happen sporadically the silencers will win the game!! The crying of the energyless can be installed indirectly!! The robberers have to suffer from the consequences !!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Huelewi kitu wewe.. Rais wa DRC wa sasa alitokea ukimbizini hadi ikulu, na mifano ya hivo ipo mingi. Au unaongelea sheria ipi?!
 
Endeleeni hivyo hivyo mtakuja vuna mnachopanda very soon.

Wanajaeshi muliingiza mtaani kufanya usafi, halafu bado unaleta diarrhea kutoka kwenye domo lako chafu.
Wananchi wanapoamua kuundoa madarakani utawala wanaoamini ni dharimu hamna jeshi la kuwashinda. Vinginevyo kuweni wakweli kwamba wananchi bado wana imani na serikali mnayopambana kuwachonganisha nayo
 
Anakimbia huku anasema sikimbii, ha ha ha duh.

Kakimbia? Mmeshindwa kumkimbiza? Mbona hamkumkamata?

Waziwazi ameondoka kupitia JKNIA kama alivyokuja. Si mamboleo wala yeyote aliyeleta kokoro.

Waliomsindikiza Lissu kuondoka ni taarifa tosha kwa akina Jiwe na vibaraka wao kuwa wawe macho.

Wewe jidanganye, waulize wenyewe wako kama mapanya mashimoni!
 
Anaondoka nchini kwa aibu kubwa sana huyu na sijui atasema nini kwa waliomtuma. Plan A imefeli na plan B hivyo hivyo, hapa kwa watu wenye uelewa yawapasa kuwa makini maana haiwezekani mtu awatie hamasa ya kufanya virugu harafu yeye akimbie uwanja wa mapambano.
 
..kama ni kweli Tundu Lissu ameondoka, basi serikali imetumia busara.

..serikali ingeamua kumkamata tungetumbukia ktk MGOGORO WA KIDIPLOMASIA na Ujerumani.
Busara gani ndugu yangu? Magufuli angekuwa na uwezo angeamrisha akatwe kichwa na siyo kukamatwa. Hii ngoma ilikuwa ngumu na Magufuli pamoja na udiktekta uchwara wake alikuwa hana namna. Huoni amepelekwa na magari ya ubalozi na alikuwa amefuatana na maafisa wa ubalozi? Hapa diktekta uchwara alikuwa hawezi kufanya fyoko na angemgusa hata unywele wake basi habari yake angeipata!
 
Diktekta uchwara na wapwa zake wataishia mwisho mbaya sana.
 
Andika kifupi tu mama D.

Andiko refu namna hii wakati yale mabegi meusi yaliwasaidia kubebea kura zenu mlizotiki kwa wagombea wenu sio poa.

Nyie hamkushinda, mlipora.
 
Tumemnyoosha alifikiri sisi ni wasaliti kama yeye! Eti nikishindwa nitawaingiza barabarani as if sisi watz ni watoto wake! Aende kwa mabwana zake!
Haya maneno yanapandisha chuki badala ya kuponya makovu.. kuna nchi mpaka Leo hii watu hawana Amani iwe ni waanzilishi wa dhuluma ama wahanga wa dhuluma. Huwezi kuwa powerful forever nawaapia huwezi. Ukijua hili basi utafikili a kesho ya vizazi vyako. Lakini ukiwa punguani basi utakua na fikra zakipunguani zaidi!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo hao unaowapa mawaidha na maoni hawana upeo wa fikra, wala hawana elimu au exposure. Mtu anayeona kutokwenda nje ndio uzalendo atajuaje diplomasia? Yeye basi aona Tanzania ina utajiri wote na wala haimhitaji yeyote- ingawaje katika kipindi cha miaka minne tu amekwishakopa Zaidi ya dola Bilioni 9 (Kikwete na ubadhirifu wake wote alikopa dola bilioni 7 tu katika kipindi cha miaka 10). Halafu anawaambia reli inajengwa kwa pesa za wauza pilipili manga! Kweli, hiyo reli imeishafika Morogoro? Si ilikuwa iwe imefika mwaka uliopita? Hata haizungumziwi tena!
 
Kuhusu kutafuta hifadhi kwa viongozi wa upinzani katika mataifa yanayoheshimu uhuru na haki ya kuishi.

Na Mwl, John Pambalu

Mwaka 2015 baada ya uchaguzi uliompa ushindi Mhe. Magufuli. Aliyekuwa Mkt wa Chadema mkoa wa Geita na mgombea ubunge Jimbo la Busanda marehemu Alphonce Mawazo. Alipokea taarifa za vitisho juu ya uhai wake, hakuamua kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini, siku chache baadaye aliuawa kikatili mchana kweupe mita chache kutoka kituo cha polisi huku jimboni Busanda mkoani Geita.

Kiongozi mwingine wa Chadema na mkosoaji wa serikali ya awamu ya tano Ben Saanane alipokea taarifa za kutishia uhai wake. Hakuona sababu za kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini. Siku chache baadaye alipotea na mpaka leo hakuna anayejua yuko wapi Ben Saanane.

Mwaka 2017 Mhe. Tundu Lissu alipokea vitisho juu ya uhai wake. Yeye alijaliwa kujua mpaka namba za gari za waliokuwa wakimfatilia. Lissu hakuona umuhimu wa kutafuta hifadhi. Siku chache baadaye alishambuliwa kwa risasi za moto kwenye nyumba za serikali zenye ulinzi full-time. Mpaka leo hata hao wanaodai nchi iko swali hawajawahi kusema ni wakina nani walimshambulia Lissu.

Nataka kusema nini?.

Wapinzani wanaotishiwa uhai wao kuamua kuondoka nchini kutafuta hifadhi ni hekima ya kimungu. Yusuph alimkimbiza Bethlehem mtoto Yesu kukwepa tishio la kupoteza uhai wa mtoto Yesu baada ya mfalme Herode kutangaza watoto wote wa kiume wauawe.

Mhe. Lissu na Lema ambao wameondoka nchini kutafuta hifadhi nje ya nchini wanastahili pongezi hata Yesu alipelekwa uhamishoni ili abaki salama.

Wasalaam
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa
 
Inauma sana ila Dunia kigeugeu hii

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…