Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Da very painful Sana, yoyo kwa yote MUNGU ni mwema siku zote amtangulie,Sina mengi zaidi ya uzuni ulioniingia kwa Kasi ya hajabu moyoni
 
Imagine taifa lingekuwa mikononi mwa huyu puppet ingekuwaje?

Ameamua kurudi kwao Brussels!
Taifa liko chini ya Magufuli na wapwa zake mbona ndiyo maisha yamezidi kuwa mabaya kuliko muda wote tangu tupate uhuru?
 
Silencing the robberers at the very scientific way can be the very best way forward!! If this happen sporadically the silencers will win the game!! The crying of the energyless can be installed indirectly!! The robberers have to suffer from the consequences !!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Huyu Lissu hadhi yake ya sasa ni mkimbizi! Maana yake hawezi akafanya siasa tena, hasa siasa za kuikashifu au kuhusu nchi aliyo kimbia, hiyo ni sheria inayo mhusu mkimbizi yeyote. Hivyo mwisho wa Lissu kisiasa umefika Hatakuwa na uwaja mwingine wa siasa hana.
Huelewi kitu wewe.. Rais wa DRC wa sasa alitokea ukimbizini hadi ikulu, na mifano ya hivo ipo mingi. Au unaongelea sheria ipi?!
 
Endeleeni hivyo hivyo mtakuja vuna mnachopanda very soon.

Wanajaeshi muliingiza mtaani kufanya usafi, halafu bado unaleta diarrhea kutoka kwenye domo lako chafu.
Wananchi wanapoamua kuundoa madarakani utawala wanaoamini ni dharimu hamna jeshi la kuwashinda. Vinginevyo kuweni wakweli kwamba wananchi bado wana imani na serikali mnayopambana kuwachonganisha nayo
 
Anakimbia huku anasema sikimbii, ha ha ha duh.

Kakimbia? Mmeshindwa kumkimbiza? Mbona hamkumkamata?

Waziwazi ameondoka kupitia JKNIA kama alivyokuja. Si mamboleo wala yeyote aliyeleta kokoro.

Waliomsindikiza Lissu kuondoka ni taarifa tosha kwa akina Jiwe na vibaraka wao kuwa wawe macho.

Wewe jidanganye, waulize wenyewe wako kama mapanya mashimoni!
 
Anaondoka nchini kwa aibu kubwa sana huyu na sijui atasema nini kwa waliomtuma. Plan A imefeli na plan B hivyo hivyo, hapa kwa watu wenye uelewa yawapasa kuwa makini maana haiwezekani mtu awatie hamasa ya kufanya virugu harafu yeye akimbie uwanja wa mapambano.
 
..kama ni kweli Tundu Lissu ameondoka, basi serikali imetumia busara.

..serikali ingeamua kumkamata tungetumbukia ktk MGOGORO WA KIDIPLOMASIA na Ujerumani.
Busara gani ndugu yangu? Magufuli angekuwa na uwezo angeamrisha akatwe kichwa na siyo kukamatwa. Hii ngoma ilikuwa ngumu na Magufuli pamoja na udiktekta uchwara wake alikuwa hana namna. Huoni amepelekwa na magari ya ubalozi na alikuwa amefuatana na maafisa wa ubalozi? Hapa diktekta uchwara alikuwa hawezi kufanya fyoko na angemgusa hata unywele wake basi habari yake angeipata!
 
Anaondoka nchini kwa aibu kubwa sana huyu na sijui atasema nini kwa waliomtuma,plan A imefeli na plan B hivyo hivyo ,hapa kwa watu wenye uelewa yawapasa kuwa makini maana haiwezekani mtu awatie hamasa ya kufanya virugu harafu yeye akimbie uwanja wa mapambano
Diktekta uchwara na wapwa zake wataishia mwisho mbaya sana.
 
Hivi chadema wangekua wamechukua majimbo yote kasoro mawili kwenye uchaguzi, halafu CUF na CCM wakapata kitu kimoja kimoja mngesema CCM waachiwe baadhi ya majimbo ili kuweka balance bungeni?

Chadema tafuteni mlipokosea mtengeneze..... manenomaneno, matusi, uasi, ukimbizi hautamsaidia mtanzania yoyote zaidi ya hao viongozi wenu wabinafsi na wanaojifikiria wenyewe.

Chama mlikinajisi wenyewe kwa kumwita mliyemtuhumu fisadi kugombea urais, tena mbaya zaidi mlimkaribisha baada ya chama chake kumwambia hawawezi kumpa nafasi ya kuongoza dola sababu sio muadilifu.

Nyie sababu ya tamaa zenu za pesa mkamsafisha bila haya ili mshirikiane nae kufisadi nchi.
Hamkujifunza kwa Lowasa 2015........

Na ilipofika 2020 mkakinajisi tena chama kwa kumuweka mgombea mtetezi wa mataifa ya nje asiyejali maslahi ya wananchi. Eti mgombea wenu akaanza kampeni awe mbwembwe huku akiwatukana watanzania wasomi na wasio wasomi hadi maJaji kuwa hawajui kiingereza, eti mkawadharau police na kuwaambia wamechoka na wana hali mbaya, mgombea wenu akawa mjuaji wa kila kitu akamdharau hadi baba wa taifa Nyerere. Kwa kampeni zake hakuna kilichofanyika Tanzania tangu wazungu waondoke.... analazimisha eti hata kwenye reli hakuna kilichofanyika ila reli imejengwa na mjerumani
Juu ya yote akawaahidi waliomtuma hadi kwenye ilani ya chama chenu kwamba akiingia ikulu ataweka madini kama dhamana kwao ili wampe pesa.

Kampeni mwanzo mwisho mgombea wenu alikua akituringishia nguvu ya wazungu, akijidai wakili wake anafuatilia kitu. Watanzania walijiuliza hivi tukimpa kura atatuongoza yeye au atatuongoza kwa amri ya hao mabwana aliowaahidi kuweka mali zetu rehani kwao?

Hivi kweli hadi Karne hii bado kuna wasomi wa Tanzania tunatumia elimu tuliyo nayo kuweka rehani nchi yetu kwa wazungu badala ya kutumia ujuzi na elimu yetu kuvuna rasilimali zetu kwa faida? Tundu amelifedhehesha sana taifa

Hivi mlifikiri watanzania ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama huyo kuwa rais wa nchi?
Wafuasi wa Tundu ambao ni wachache sana wana mienendo kama ya Tundu.
Tuliwashauri mapema mkawe mawakala ili mkasimamie haki mnayoiimba hapa jf hamkuskia, tena badala yake chama chenj kikatafuta ambao hadi leo hakijawalipa posho zao.

Matokeo yake kila siku mnarudi hapa kulalamika kwamba mmeibiwa kura, hivi hamjisikii aibu kila uchaguzi mnalalamikia tatizo lilelile kama sababu ya kushindwa? Hamuoni kama nyie ni chama kisichoweza kutatua matatizo ya chama wala ya wananchi?

Haya sasa wananchi wamewakataa kwenye kura, wamewakataa kwenye maandamano, wamewakataa kwenye kuigomea serikali....... na hii inaonyesha chama chenu sio cha wananchi bali ni cha viongozi ndio maana mmebaki wenyewe mkihangaika.
Ingekua wananchi wanawapenda kungekua na maandamano yasiyozuilika kama maji ya jangwani kipindi cha mafuriko ila wananchi wana raha na amani tele, hata wale mliowaandaa kwa malipo sasa wanajuta na hawawezi rudia

Kwa tamaa zenu 2015 mliua kile chama tulichokipenda, Ile chadema ya wananchi, chadema iliyokua tumaini la wanyonge, chadema ya Mzee Ndesamburo na Dr Sla na wale viongozi wengine makini. Laana itawaandama kama hamtawaambia wananchi mliwakosea ili muanze upya

Maisha sio rahisi kwa mtanzania yoyote hata kwa Rais, huu ni muda wa kujenga uchumi wetu tuliouharibu na huduma za kijamii kwa maslahi yetu wote. Acheni kulalamika sasa

Tundu asafiri salama, tunamshukuru kwa kushiriki

Mods msidelete
Andika kifupi tu mama D.

Andiko refu namna hii wakati yale mabegi meusi yaliwasaidia kubebea kura zenu mlizotiki kwa wagombea wenu sio poa.

Nyie hamkushinda, mlipora.
 
Tumemnyoosha alifikiri sisi ni wasaliti kama yeye! Eti nikishindwa nitawaingiza barabarani as if sisi watz ni watoto wake! Aende kwa mabwana zake!
Haya maneno yanapandisha chuki badala ya kuponya makovu.. kuna nchi mpaka Leo hii watu hawana Amani iwe ni waanzilishi wa dhuluma ama wahanga wa dhuluma. Huwezi kuwa powerful forever nawaapia huwezi. Ukijua hili basi utafikili a kesho ya vizazi vyako. Lakini ukiwa punguani basi utakua na fikra zakipunguani zaidi!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Hii ina hatari yake. Kumbukeni alipokuwa tunduma yule police alimwambiaje kaka usikitafutie matatizo na police naona alimwelewa akamwacha.
Jamaa amekusanya evidence nyingi sana Mimi nionavyo huyu anakwenda kukinukisha .
Nilidhani serikali ilipaswa hata kumuita balozi aliyemhifadhi aende nae kuwe na mazungumzo ya ana kwa ana na Rais ili Ku resolve hii kitu kuliko kumwachia hivi.
Kumbuka
Issue ya chato akagoma kuondoka
Kumbukeni alivukaje kwenda kisiwa cha ukerewe
Kumbukeni nyamongo
Matukio yote hayo yeye hajajibizana nayo ila anawasiliana na Mwanasheria wake.
Binafsi huyu hakupaswa kuondoka.

Kwa sasa nashauri
Viongozi wana diplomacy wa ccm Nguli pamoja na Rais wetu wawaite viongozi wa chadema wakae nao wazungumze mambo yataisha kabisa .
Ila mkataapo haya yataleta kushusha heshima ya Tanzania ilijengwa katika ulimwengu.
Pili vikwanzo vitaanza kuibuka
Tatu uchumi utaporomoka

Maoni tu haya
Tatizo hao unaowapa mawaidha na maoni hawana upeo wa fikra, wala hawana elimu au exposure. Mtu anayeona kutokwenda nje ndio uzalendo atajuaje diplomasia? Yeye basi aona Tanzania ina utajiri wote na wala haimhitaji yeyote- ingawaje katika kipindi cha miaka minne tu amekwishakopa Zaidi ya dola Bilioni 9 (Kikwete na ubadhirifu wake wote alikopa dola bilioni 7 tu katika kipindi cha miaka 10). Halafu anawaambia reli inajengwa kwa pesa za wauza pilipili manga! Kweli, hiyo reli imeishafika Morogoro? Si ilikuwa iwe imefika mwaka uliopita? Hata haizungumziwi tena!
 
Kuhusu kutafuta hifadhi kwa viongozi wa upinzani katika mataifa yanayoheshimu uhuru na haki ya kuishi.

Na Mwl, John Pambalu

Mwaka 2015 baada ya uchaguzi uliompa ushindi Mhe. Magufuli. Aliyekuwa Mkt wa Chadema mkoa wa Geita na mgombea ubunge Jimbo la Busanda marehemu Alphonce Mawazo. Alipokea taarifa za vitisho juu ya uhai wake, hakuamua kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini, siku chache baadaye aliuawa kikatili mchana kweupe mita chache kutoka kituo cha polisi huku jimboni Busanda mkoani Geita.

Kiongozi mwingine wa Chadema na mkosoaji wa serikali ya awamu ya tano Ben Saanane alipokea taarifa za kutishia uhai wake. Hakuona sababu za kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini. Siku chache baadaye alipotea na mpaka leo hakuna anayejua yuko wapi Ben Saanane.

Mwaka 2017 Mhe. Tundu Lissu alipokea vitisho juu ya uhai wake. Yeye alijaliwa kujua mpaka namba za gari za waliokuwa wakimfatilia. Lissu hakuona umuhimu wa kutafuta hifadhi. Siku chache baadaye alishambuliwa kwa risasi za moto kwenye nyumba za serikali zenye ulinzi full-time. Mpaka leo hata hao wanaodai nchi iko swali hawajawahi kusema ni wakina nani walimshambulia Lissu.

Nataka kusema nini?.

Wapinzani wanaotishiwa uhai wao kuamua kuondoka nchini kutafuta hifadhi ni hekima ya kimungu. Yusuph alimkimbiza Bethlehem mtoto Yesu kukwepa tishio la kupoteza uhai wa mtoto Yesu baada ya mfalme Herode kutangaza watoto wote wa kiume wauawe.

Mhe. Lissu na Lema ambao wameondoka nchini kutafuta hifadhi nje ya nchini wanastahili pongezi hata Yesu alipelekwa uhamishoni ili abaki salama.

Wasalaam
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa
 
Walipotea sehemu ndogo sana, kama wangemuwahi Lissu kabla hajafika ubalozi wa ujerumani that day, walikuwa wammalize, but the moment Lissu ameshafika mbele ya ubalozi, na balozi akawa ameshajua uwepo wake nje, hapo kila kitu kikawaharibikia.

Ndio maana walivyojaribu kumchukua kwa gari za polisi, na maafisa wa ubalozi wa ujerumani wakawa wanawafuatilia kwa nyuma, mpaka hapo wasingempata Lissu tena.
Inauma sana ila Dunia kigeugeu hii

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom