Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Mkuu watanzania linapokuja suala la kitaifa huwa wako makini mno!

Aliyemuharibia Lissu ni Amsterdam.

Watz wako makini sana huwezi kuwapelekesha
 
Mkuu watanzania linapokuja suala la kitaifa huwa wako makini mno,!

Aliye muharibia Lisu ni Amsterdam.

Watz wako makini sana huwezi kuwapelekesha

Sikuandika watanzania hawako makini kwa mambo ya kitaifa.
Umakini unaendana na uwezo wa kufikiri.
Nataka tuboreshe zaidi kwa watu wetu.
 
Hii inaitwa political tourism. Unaenda nchi fulani unagombea Urais, uchaguzi ukiisha unapanda ndege unaenda kuendelea na maisha yako.

Wale waliomuamini wote anawaona mabwege.
Ilitabiriwa

 
Acha kuingiza watu barabarani ila hata kuita mkutano wa hadhara kuwaaga makamanda ameshindwa
Mkuu unaishi mwezini, taratibu hapa ni uchaguzi ukiisha hakuna mikutano ya hadhara, hakuna kufanya siasa labda kwenye jimbo lako kama umefanikiwa kuupata ubunge.

Vinginevyo ni mpaka baada ya miaka mitano.
 
Leo ni siku muhimu sana kwa Taifa letu. Tusije kusahau wahenga walisema fimbo ya mbali huwa haiui nyoka na mkataa kwao mtumwa. Haya mambo mawili yanakuja mbele ya safari. Tuyape muda tu.

Ningeweza kushauri, ningeomba kesi zote za TL zifutwe. Halafu aendelee kuongoza kutoka huko alikokwenda maana hawa anaofikiria ni wenzake ni wafanya biashara. Watakuja kimya kimya kuomba kupewa fursa.

Tanzania yetu hii ni lulu, wameliona hilo kupitia uchaguzi ambao waliamini lazima ungeambatana na fujo. Sasa limewashuka wanahangaika na story za kupikwa
 
Kama tungekuwa na viongozi wenye akili wangejitahidi kuhakikisha hawa viongozi wa upinzani wanabaki nchini.

Sasa ushindani kati ya Jiwe na Wapinzani unaenda kwenye ngazi ya kimataifa, ambako kwa kipimo chochote kile, Jiwe ni dhaifu sana.
HAKUNA mwenye shida nao, hata viongozi wa saccos hawana shida nao.
Mbowe yuko usingizini.
 
Mkuu hii hama Hama ya viongozi hasa wa upinzani sio afya kwa taifa ,so vyema shauri itakua nzuri zaidi mkuu ,

Kama waliweza kuwa salama hadi kampeni zikaisha na ilipotokea wameshindwa ndio wakaamua kuhama hakuna anayeweza kuwazuia

Hawahawa hata wakati wa corona walikaa bunge hadi posho zilipoingia ndio wakajipeleka quarantine
 
Alisema tiketi yake ni 8/12/2020
Imekuwaje Tena?
Huyu mwamba muongo Sana!
 
Haikuwa siri boss.
Hivi hawa watu wanadhani kila mtu ni mjinga kama wao? Uhuni uliofanywa kwenye huu uchaguzi kuna mtu ambaye hakuuona? Ukiondoa wote walioteuliwa na Magufuli na kundi lake kwenye nafasi za ubunge hakuna mtu mwingine, hata awe mwana CCM aliyefurahia. Wananchi, wakiwemo wana CCM wamepelekewa mtu aliyempendekeza Magufuli and co ili awe mbunge wao wapende au wasipende.
 
Nenda eenh Lissu kawaambie hapa ni Bongo hatugombanishwi kwa tofauti za vyama vyetu, dini zetu(makanisa yanachangia ili misikiti ijengwe), n.k
Yote kwa yote tumekusamehe maana tunajua hukuwa wewe. Enenda zako eeh Tundu na usitende dhambi tena.
 
Mkuu unaishi mwezini,taratibu hapa ni uchaguzi ukiisha hakuna mikutano ya hadhara,hakuna kufanya siasa labda kwenye jimbo lako kama umefanikiwa kuupata ubunge.
Vinginevyo ni mpaka baada ya miaka mitano.
Hii sheria mwaka huu itabadilishwa. Wabunge wa CCM na CCM wataruhusiwa kufanya mikutano ya siasa kila mahali kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…