Tundu Lissu aondoka nchini kuelekea Ubelgiji. Asema anakwenda uwanja mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu

Sasa tujiandae kwa spana....naona ataenda taasisi za kimataifa plus mabunge yenye nguvu duniani kueleza kilichotokea wakati wa uchaguzi...
 
Andika kifupi tu mama D.

Andika refu namna hii wakati yale mabegi meusi yaliwasaidia kubebea kura zenu mlizotiki kwa wagombea wenu sio poa.

Nyie hamkushinda, mlipora.

Mungu atupe uhai denooJ kuna siku utajuta kuwafahamu hao mabwana na utarudi kuisoma hiyo ndefu
 
Tatizo hao unaowapa mawaidha na maoni hawana upeo wa fikra, wala hawana elimu au exposure. Mtu anayeona kutokwenda nje ndio uzalendo atajuaje diplomasia? Yeye basi aona Tanzania ina utajiri wote na wala haimhitaji yeyote- ingawaje katika kipindi cha miaka minne tu amekwishakopa Zaidi ya dola Bilioni 9 (Kikwete na ubadhirifu wake wote alikopa dola bilioni 7 tu katika kipindi cha miaka 10). Halafu anawaambia reli inajengwa kwa pesa za wauza pilipili manga! Kweli, hiyo reli imeishafika Morogoro? Si ilikuwa iwe imefika mwaka uliopita? Hata haizungumziwi tena!
Mtandao wa Jamii forum unasomwa na watu wengi na viongozi wengi hata Rais pia. Nahisi hawajachelewa kufanya hili tunalojadili.

Wapigania Uhuru wa SA wengine walikimbilia Tanzania hapo Morogoro walipopikwa walirejea kwao.

Ukiona watu wanaanza kukimbia nchi yao namna hii sio ishara njema.

Hivi unadhani walio ondoka kimya kimya kwenda huko wangapi Mimi na wewe hatujui. Sasa ili kuzima haya

1. Rais awatumie hawa
A) viongozi wa dini wanaoungwa mkono na vyama vya upinzani awakutanishe pamoja na hivyo vyama
2. Mabalozi wanaochangia maendeleo kwa asilimia kubwa nchini
4. Walio shiriki uchaguzi katika ngazi ya urais ili wazungumze. Otherwise kukimbia nchi sio ishara njema kabisa
 
Uzuri alishatuaga, kuwa baada ya uchaguzi ataondoka. Alichokosa ni nauli tu imebidi ajidai mkimbizi.
 
Haya ndiyo tunaita mawazo ya ki-nyani nyani. Udikteta na uongozi mbovu wa Magufuli na wapwa zake unaathiri watanzania wote. Mabadiliko yakitokea na kwa faida ya watanzania wote na tukiendelea na huu uongozi mbovu ni hasara ya watanzania. Ni jukumu la watu wote kuipigania nchi yetu. Kama wewe unaona kuna wenye wajibu zaidi basi utabaki na upumbavu wako huku ufukara ukindelea kukutafuna unless uwe kwenye inner circle ya Magufuli na wapwa zake.
Matatizo yako hayawezi kuwa matatizo ya watanzania wengi.

Kuanzia leo fahamu, mabadiliko huwa hayazuiliki ila kama hapa yamezuilika mjue mnakosoro kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora amefanikiwa kuokoa roho yake.

Mapambano yanaendelea from whichever angle.
Mkuu niliwai sema hum LISSU anaakili nyingi wtu wako kaondoka, kuondoka sio shida shida nini kitafuata. Vita ni akili hata wakati tunamtwanga idd amin hatukua na jeshi kubwa, wala zana kubwa kuliko idd amini,ila akili kubwa ya viongozi kwa kipindi hicho chini ya mwalim tulimnyoosha na jeuri yake yote.

Viongozi wa kisiasa kuondoka kwa Sasa sio afya kwa nchi
 
Maandamano yasiyo na kikomo yameishia wapi ?Bora hata msingetaja maandamano.Wapinzani huwa mnakurupuka na kusema vitu ambayo hamuwezi timiza. Grow up.
You cannot demonstrate in the face of a brutal police force. You cannot demonstrate in the face of a regime which brooks no democratic opposition. Grow up.
 
Pasi shaka yoyote, hizi kesi ndio imebaki turufu yao kuu ya kummaliza Tundu Lissu, kumbe yeye alishauona mchezo kungali mapema kabisa.

..Lissu katumia akili sana.

..angekubali kwenda mahakamani angefungwa na most likely angefia gerezani.
 
Sheria za Kimataifa ziko wazi kuhusu Ubalozi na hii ni Dunia nzima, nchi ya Ujerumani haiwezi kuzivunja hata siku moja sababu ya huyo kichaa wenu, isitoshe hata kama angekwenda Ubalozi wa Komoro asingeshikwa pia, ...

..kwanini hakushikwa uwanja wa ndege wakati ana kesi mahakamani?

..tukubali kwamba serikali imesalimu amri kwa kumuacha aondoke wakati ikimhitaji akajibu mashtaka ya uchochezi.
 
sikimbii mapambano, ila nakwenda uwanja mwingine mpya wa kudai haki, demokrasia na utu wetu kwa nchi yetu.
Wewe harakati unaenda kufanyia nje ya nchi, makamanda wako bongo harakati wanafanyia kwenye thread za Jf! Sioni hii mission yenu ikifanikiwa maana wote mnaogopa kuingia field. All battles are won with boots on ground, zaidi ya hapo ni mbio za sakafuni tu.
 
..kwanini hakushikwa uwanja wa ndege wakati ana kesi mahakamani?

..tukubali kwamba serikali imesalimu amri kwa kumuacha aondoke wakati ikimhitaji akajibu mashtaka ya uchochezi.
Sasa mustakabali wa CHADEMA ukoje?

It seems to me they’ve resigned to fate.
 
Hivi chadema wangekua wamechukua majimbo yote kasoro mawili kwenye uchaguzi, halafu CUF na CCM wakapata kitu kimoja kimoja mngesema CCM waachiwe baadhi ya majimbo ili kuweka balance bungeni?

Chadema tafuteni mlipokosea mtengeneze..... manenomaneno, matusi, uasi, ukimbizi hautamsaidia mtanzania yoyote zaidi ya hao viongozi wenu wabinafsi na wanaojifikiria wenyewe.

Chama mlikinajisi wenyewe kwa kumwita mliyemtuhumu fisadi kugombea urais, tena mbaya zaidi mlimkaribisha baada ya chama chake kumwambia hawawezi kumpa nafasi ya kuongoza dola sababu sio muadilifu.

Nyie sababu ya tamaa zenu za pesa mkamsafisha bila haya ili mshirikiane nae kufisadi nchi.
Hamkujifunza kwa Lowasa 2015........

Na ilipofika 2020 mkakinajisi tena chama kwa kumuweka mgombea mtetezi wa mataifa ya nje asiyejali maslahi ya wananchi. Eti mgombea wenu akaanza kampeni awe mbwembwe huku akiwatukana watanzania wasomi na wasio wasomi hadi maJaji kuwa hawajui kiingereza, eti mkawadharau police na kuwaambia wamechoka na wana hali mbaya, mgombea wenu akawa mjuaji wa kila kitu akamdharau hadi baba wa taifa Nyerere. Kwa kampeni zake hakuna kilichofanyika Tanzania tangu wazungu waondoke.... analazimisha eti hata kwenye reli hakuna kilichofanyika ila reli imejengwa na mjerumani
Juu ya yote akawaahidi waliomtuma hadi kwenye ilani ya chama chenu kwamba akiingia ikulu ataweka madini kama dhamana kwao ili wampe pesa.

Kampeni mwanzo mwisho mgombea wenu alikua akituringishia nguvu ya wazungu, akijidai wakili wake anafuatilia kitu. Watanzania walijiuliza hivi tukimpa kura atatuongoza yeye au atatuongoza kwa amri ya hao mabwana aliowaahidi kuweka mali zetu rehani kwao?

Hivi kweli hadi Karne hii bado kuna wasomi wa Tanzania tunatumia elimu tuliyo nayo kuweka rehani nchi yetu kwa wazungu badala ya kutumia ujuzi na elimu yetu kuvuna rasilimali zetu kwa faida? Tundu amelifedhehesha sana taifa

Hivi mlifikiri watanzania ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama huyo kuwa rais wa nchi?
Wafuasi wa Tundu ambao ni wachache sana wana mienendo kama ya Tundu.
Tuliwashauri mapema mkawe mawakala ili mkasimamie haki mnayoiimba hapa jf hamkuskia, tena badala yake chama chenj kikatafuta ambao hadi leo hakijawalipa posho zao.

Matokeo yake kila siku mnarudi hapa kulalamika kwamba mmeibiwa kura, hivi hamjisikii aibu kila uchaguzi mnalalamikia tatizo lilelile kama sababu ya kushindwa? Hamuoni kama nyie ni chama kisichoweza kutatua matatizo ya chama wala ya wananchi?

Haya sasa wananchi wamewakataa kwenye kura, wamewakataa kwenye maandamano, wamewakataa kwenye kuigomea serikali....... na hii inaonyesha chama chenu sio cha wananchi bali ni cha viongozi ndio maana mmebaki wenyewe mkihangaika.
Ingekua wananchi wanawapenda kungekua na maandamano yasiyozuilika kama maji ya jangwani kipindi cha mafuriko ila wananchi wana raha na amani tele, hata wale mliowaandaa kwa malipo sasa wanajuta na hawawezi rudia

Kwa tamaa zenu 2015 mliua kile chama tulichokipenda, Ile chadema ya wananchi, chadema iliyokua tumaini la wanyonge, chadema ya Mzee Ndesamburo na Dr Sla na wale viongozi wengine makini. Laana itawaandama kama hamtawaambia wananchi mliwakosea ili muanze upya

Maisha sio rahisi kwa mtanzania yoyote hata kwa Rais, huu ni muda wa kujenga uchumi wetu tuliouharibu na huduma za kijamii kwa maslahi yetu wote. Acheni kulalamika sasa

Tundu asafiri salama, tunamshukuru kwa kushiriki

Mods msidelete
mimi mama d nilikua mwanaharakat wa kupenda kusikia kipind kile cha slaa kampen zilikua kal sana tangu kusikia ishu za kusapot ushoga bad nilichukia sana .na kuwekwa lehani madini hapo ndio walinitibua.nawapongeza waheshimwa walioshinda majimbon kwa kishindo safar hii maji kila kona mpaka yamwagike
 
Duh, bandiko refu lisilo na mantiki, Issue hapa sio matokeo bali ni huku kutishana

Unakumbuka kauli ya Heri James? "Hatutatumia risasi, saivi ni sindano tu" Ilimlenga nani?
 
Back
Top Bottom