Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Inaelekea umeweka pamba masikioni. Amezungumzia Tume Huru, mahusiano na nchi za nje, Katiba mpya itakayompa Uhuru na Haki zaidi mwananchi, kusuka upya mifuko ya pensheni na kuhakikisha pensheni inalipwa pale mtu anapostaafu na sio kusubiri hadi atimize miaka 60, vitambulisho vya ujasiriamali, kuheshimu haki za wafanyabiashara n.k. Labda kwa vile amejikita zaidi katika kurekebisha ( anavyoona yeye) mifumo yetu ya utawala na uongozi na sio kwenye mali ndio maana unaona hajasema kitu.
Amandla...