Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aongea na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Sept 9, 2020, ataenda Mahakamani kwenye kesi zake Kampeni zikiisha

Shida ya lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Walizoea siasa za personal attacks enzi za Kikwete sasa watanzania wamekomaa politically wanataka sera sio umbeya wa kuongelea mtu

Halafu ona anaongea vitu Ushahidi hana anasema Magufuli anataka kuongeza miaka 10!!! HIVI kweli kuna chombo chochote cha habari anategemea kiandike huo ujinga?

Hawaandikwi wala kutangazwa sababu ya matamshi yao wenyewe yako chini ya kiwango na kinyume cha sheria
 
Maneno ya Lisu ni magumu na mazito mno kuyasikiliza!!Yanatia uchungu sana!!!!NAWAAHIDI MIMI NA FAMILIA YANGU NITAMPIGIA KURA!!!LAKINI BARABARANI SITOINGIA !!KAZI KWAKE KULINDA ASIIBIWE!!!!NAWASHAURI ASHIRIKIANE NA DIASPORA WAUNDE JESHI LA MSITUNI ILI WAJE NA OPERATION "OKOA DEMOKRASIA YETU" WAPAMBANE ILI WATANGAZWE WASHINDI!!!!!
 
Lissu hawezi kuchambua au kueleza mambo pasina kulaumu au kumshambulia mtu,hivyo ndivyo alivyo na uzuri au ubaya kuna watu wanapenda hiyo hali ya kusikia malalamiko muda wote kuliko kusikia ni nini kifanyike.
Utakuwa kiziwi, au una akili ndogo wewe ndie huwezi kuchambua mambo.
 
Hyo picha mbona ni logical? Ina maana kwamba something is better than nothing, hta umasikini hauondoki siku moja ila ni process ya jitihada ndogo ndogo zinazaa matunda baadae.
Hayo mashimo ya mashoka kwenye huo mti yatatoa starting point kwa wanamageuzi wa baadae kuiondosha CCM.

Sijaona cha kuchekesha hapo unless mlidhani kuitoa CCM ni tukio na sio process iliyoanza 1995!!
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Better late than never , kama na wewe unakiri hadharani kwamba Magufuli hafai basi kampeni zetu zimefanikiwa sana ! ondoa shaka kuhusu atakachofanya Lissu , huyu ataondoa utumwa na utekaji , ataleta uhuru kamili na kuhakikisha haki kwa kila mtu
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Kuna tofaut kubwa sana kati ya "Wewe kutosikiliza au kufuatilia hotuba zake, wewe kutokujua chochote kuhusu ilani ya chadema" vs Kilichopo kwenye ilani na sera anazonadi

wewe kutokua na taarifa haimaanishi kwamba hafanyi, usichanganye hayo mambo mawili, utachekwa
 
Hivi watu wameshasahau kama tulikuwa tuna mgombea kama huyu ambaye ni dr slaa kazi ya upinzani ni kukosoa siku zote kwanini utawala huu mturudishe mfumo wa chama kimoja kwamba kila anaekosoa sio mzalendo
 
Acha ujinga, kwa hiyo anayotaka kutuambia atafanya nini yameisha? Kwani akisema kila siku atatufanyia nini shida iko wapi?
Huyu anaanza kupotea, arudishwe kwa nguvu kwenye mstari
Usimpangie cha kusema kila wakati!Leo anasema haya,kesho kasikikize atasema yapi!
Acheni ufala!Haya anayozungumza ni ya msingi sana!Safari hii kama ni kushindwa tushindwe kihalali else tutadai haki yetu kwa namna yoyote ile!
 
Tayari Tundu Lissu jamani ameshakata tamaa yaani ana declaire kushindwa mapema hivi au hela ya kampeni imeshakata ? Na dj yupo kimya wala hahangaiki nae tena du jamani wajanja wamemtosa bora angekuwa yuledogo sasa hivi tungekuwa tunashuhudia kampenimotomoto
 
Shida ya Lissu hasemi yeye kama yeye atafanya mambo gani makubwa, tushajua magu hafai. Sasa yeye aache kila siku kumzungumzia magu badala yake aseme yeye kama yeye atafanya yapi
Na kutofaa kwa Magufuli hakumpi yeye nafasi ya kuwa rais maana wapiga kura tunaweza pia kuwa tunamuona kuwa hatufai!
 
Back
Top Bottom