Valuhwanoswela
JF-Expert Member
- Jun 27, 2019
- 1,229
- 1,125
Kenya na Zimbabwe ni mifano miwili ya nchi zinazonufaika sana kwa kujua lugha fasaha ya watu wengine tofauti na Tanzania iliyotelekeza lugha za kigeni na kubaki na Kiswahili cha mtaani (Creole) na Kisukuma. Kenya wanajua Kingereza kizuri na Kiswahili kizuri ndo maana walimu wengi wanaofundisha Kiswahili kote ulumwengu I wanatoka Kenya.Mgombea Uraisi wa chama fulani alisema kuwa watanzania hawajui kingereza, hasa wanatia aibu wanapokuwa huko ughaibuni. kisha nikajiuliza; je! kiswahili chetu hiki, watanzania wote wanakifahamu kwa usanifu na usadifu wake?
kitu ambacho naamini sio kweli, yawezekana mwenyewe nikawa miongoni mwa wahanga hao. Sasa yanini kulilia kujua kingereza kwa ufasaha wakati kiswahili chenyewe tunamakosa mengi kwenye kukizungumza na kuandika. siku zote ukitaka kuwatambua wengine anza kujitambua mwenyewe. jambo jingine la kufurahisha hapa, sijawahi kusikia wazungu wakichekana ati wanaaibisha mataifa yao kwa kuongea kiswahili kibovu, mbali zaidi wengine wanakuja huku hata kingereza chenyewe hawajui, na wanafundishwa na wabongo hiyo broken.
Me nadhani wanaotucheka kwa kuongea kingereza kibovu hapa nchini na ughaibuni si wazungu bali ni sisi wenyewe. Je! kuna ulazima sana siye kujua Kingereza ili tufike Nchi ya ahadi?, Mataifa kama Uganda, Zimbabwe, Kenya n.k ambayo yasemekana yanawazungumzaji wazuri wa kingereza Wamefika Kanani?
(Nchi ya Ahadi).
Mi nadhani kheri yule mwenye Maarifa, busara na hekima, na hajui kingereza. kuliko ajuaye kingereza na akakosa vitu vitatu. kikubwa Elimu iboreshwe watu wapate Maarifa yanayoenda na wakati, na si lazima wote tujue kingereza ndio maana kuna watu wanasomea utafsri wa lugha, na Maranyingi mataifa ya Asia ya mbali wanatumia sana lugha zao hata wakiwa nje ya Nchi zao na wakalimani huhusika sana kwenye masuala yanayohusu lugha tofauti na yao.
Je! Mataifa hayo hayajapiga hatua ya kimaendeleo? Kwahiyo hili suala la kutojua kingereza Mheshimiwa aliliongelea kwa upande mmoja wa sarafu. mihemko( emotions) inatupofusha kutazama mambo yaliyo mbali zaidi.
Hata watangazaji wa Kiswahili wa Radio na Tv za Media mashughuri duniani kama vile BBC, VOA, DW, nk ni Wakenya wakiipiku TBC iliyokuwa inaongoza kutoa wafanyakazi kwenye Media hizo hata kuanzishwa kwao kulifanywa na wanafunzi wetu waliokuwa wanasoma huko zama hizo. Wajerumani hawazai Tena kwa hiyo wanapungukiwa sana Nguvukazi kwenye Viwanda vyao na kwingineko kwa hiyo
sasa wanapata toka India ambao wana elimu nzuri. Zimbabwee ni nchi mojawapo ya Afrika yenye elimu nzuri inayotambulika kimataifa ndo maana ndiyo nchi pekee inayopeleka Wauguzi (Nurses) wengi Ulaya kwa sababu Wasichana wa huko hawataki kazi kama hizo za kuvaa sare kazini. Pesa wanazorudisha nyumbani kwa ndugu zilisaidia sana kulipa mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kwa Dollar za Marekani uchumi ilipokuwa mbaya.
Nchi za Kusini mwa Afrika baada ya kupata Uhuru wao, wafanyakazi wengi Serikalini, vyuoni, hospitalini nk walikuwa Watanzania kwa sababu walikuwa wanajua Kingereza na wasomi wazuri lakini sasa hivi kama wapo ni mabaki tu maana wa sasa hawaajiriki. Kiswahili kizuri Tanzania kimebaki Zanzibar tu lakini elimu yao ni ileile kama ya Bara. Huwezi kumfundisha mtu lughà yako kama hujui lughà yake.