Tundu Lissu apata passport mpya, amshukuru Rais Samia, kurudi Nchini

Tundu Lissu apata passport mpya, amshukuru Rais Samia, kurudi Nchini

Mh.Rais wangu SSH ,kipenzi cha watanzania.....

Kila uchao anaendelea tu kutuwekea rekodi......

Rais SSH ni mbobezi wa siasa na diplomasia......

#Siempre SSH 🙏
#Siempre JMT🙏
🌹🌹❤️❤️❤️♥️♥️💯🌷🍾🍾🔥🔥💅
 
Hazimtoshi yule, usishangae akaja na kuanza kumtukana tena.
SSH alienda kumsalimia lisu alipokuwa anatibiwa nairobi, lakini baada ya kuapishwa kuwa rais, lisu huyo huyo ndiye alikuwa wa kwanza kumbambikia majina ya kijinga, mara Magufuli wa kike, mara dikteta mwanamke!
Jamaa ni chizi mr #dishlimetilt
Kwenda kumsalimia sio sharti ya kuanza kuiga udikteta qa Magufuli.

Alhamdullilah Samia ameachana na udikiteta wa mwenda zake. Anawaumbua wafuasi wa siasa chafu nyie.

Hapo ulipo umefura kwa kinyongo.
 
Maana yake baadhi ya mapendekezo aliyotoa Lissu kwa Samia walipokutana Belgium yameanza kufanyiwa kazi.

- Mbowe kaachiwa bila masharti.

- Passport.

Then.

- Kuruhusu mikutano ya siasa bila kanuni mpya, sheria ipo ifuatwe.

- Katiba Mpya.
CCM hawataki kusikia hiyo....!!
 
Maana yake baadhi ya mapendekezo aliyotoa Lissu kwa Samia walipokutana Belgium yameanza kufanyiwa kazi.

- Mbowe kaachiwa bila masharti.

- Passport.

Then.

- Kuruhusu mikutano ya siasa bila kanuni mpya, sheria ipo ifuatwe.

- Katiba Mpya.
Ni kazi nzuri Mh Rais anafanya
 
Tundu Lissu amepewa passport mpya na Serikali ya Tanzania baada ya ile ya awali kupotea kwa kuibwa kule Ujerumani.

Lissu amekabidhiwa passport yake leo na balozi wetu.

Lissu amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo Watanzania wote tumuunge mkono ili tujenge Tanzania mpya yenye Upendo na Umoja.

Tundu Lissu amemshukuru sana Rais Samia.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Eti kuna watu wamechukizwa na hii taarifa. Jomba kama wewe ni mmojawapo jitafakari... Utakuwa una hulka za uchawi na uzandiki!!
 
Tundu Lissu amepewa passport mpya na Serikali ya Tanzania baada ya ile ya awali kupotea kwa kuibwa kule Ujerumani.

Lissu amekabidhiwa passport yake leo na balozi wetu.

Lissu amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo Watanzania wote tumuunge mkono ili tujenge Tanzania mpya yenye Upendo na Umoja.

Tundu Lissu amemshukuru sana Rais Samia.

Source: Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Mataga watanuna. Walitegemea Samia angeendeleza kikosi cha polisi cha kumuua Lissu na Mbowe . Kilocho asisiwa na Muuaji Magufuli
 
Back
Top Bottom