Tundu Lissu apendekezwa kuwania tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2026

Tundu Lissu apendekezwa kuwania tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2026

Kwanini hujampigia Netanyahu yule shetani kaua Wapalestina?
Swali la kinyonge sana hili. Yaani wandengereko wenzetu wameuawa hapa Tanzania tuwe hatuna habari nao ila wapalestina ambao hatuna hata nasaba nao ndiyo tuwape kipaumbele? KWA NINI?

Wema huanzia nyumbani.
 
Kwanini ni TUZO YA AMANI badala ya TUZO YA HAKI? Nyie mnasema ni wapigania haki sio amani?
Hiyo tuzo inaitwa ni ya Amani lakini hupewa wale tu wanaopigania haki kwa lengo la kuleta amani.

Tatizo CCM huwa hawajui tofauti kati ya Utulivu na Amani. Hata majambazi wakiingia nyumbani kwa mtu kupora hulazimisha utulivu uwepo. Utasikia wakisema "tulia".
 
Shida ni kuamini wapigania amani ni ccm pekee na wapigania haki ni chadema pekee. Hakuna asiyetaka kuona haki inatendeka ila sio kwa gharama ya amani. Hakuna popote duniani ambapo madai ya haki yaliyoambatana na vurugu yaliletq amani. Nadhani hapo ndipo tunapopishana na nyie wadai haki wa JF na TEC etc
 
Kwanza kwa nini kuwe na amani halafu Haki ikosekane? Yaani amani iliyopo inaletwa na nini nje ya Haki?

Nyie CCM mnachanganya kati ya Utulivu na Amani.
 
Kwanza kwa nini kuwe na amani halafu Haki ikosekane? Yaani amani iliyopo inaletwa na nini nje ya Haki?

Nyie CCM mnachanganya kati ya Utulivu na Amani.
Nyie ndio mnachanganya. Sio kila haki inafaidisha watu wote kwa nyakati zote uwepo wa amani unanufaisha watu wote kwa wakati wote. Mfano, madai ya haki kwa harakati za tarehe 29 Oct kudai mambo mliyoyaona muhimu yaliondoa amani kwa wengine ambao hatukuona umuhimu kwa mambo hayo. Madai ya haki ya kuzuia uchaguzi trh 29 kwa sababu mlizoona zinafaa yaliondoa haki kwa wengine ambao hawakuona shida katika uchaguzi ule na pia yalileta vurugu ambazo ziliondoa haki kwa watu wengine ya kula, kutibiwa na nk.

Amani ingekuwa na sifa ya kuchagua, wala shida isingekuwepo. Kwamba, unaweza kuchoma moto mwendokasi huku wengine wakiendelea kupata haki yao ya kusafiri na usafiri huo na wengine kuwa na amani. Bahati mbaya hilo haliwezekani.

Sisi wapenda amani sio kwamba hatutaki wadai haki mdai haki zenu, ila tunataka mfanye hivyo bila kuathiri haki za wengine na kutoondoa amani wengine ambao si sehemu ya wanaodai. Ndio maana tunasisitiza kaeni chini jadilianeni namna ya kugawana hiyo keki huku sisi mkituacha na amani yetu. Ila mnapoamini kwamba lazima mchafue amani wakati w kudai haki zenu, hapo hatutakuja kuelewana abadan.
 
Ila mnapoamini kwamba lazima mchafue amani wakati w kudai haki zenu, hapo hatutakuja kuelewana abadan.
Kwanza hakuna "anayeamini" kuwa haiwezekani kudai haki bila kuchafua amani. Amani haiwezi kuwepo kama hakuna haki.

Unazungumzia haki ya mtu kupanda mwendokasi, haki ambayo imetajwa kwenye Katiba HAKI ya kuishi huitaji!

Mtu kuandamana si kuvuruga utulivu maana mbona maandamano ya kupongeza viongozi huwa watu hawapigwi risasi?
 
Mtu kuandamana si kuvuruga utulivu maana mbona maandamano ya kupongeza viongozi huwa watu hawapigwi risasi?
Unataka kuniambia nchi hii hakujawahi kuwa na maandamano yasiyo ya kupongeza serikali? Tukiwauliza iwapo yale ya tarehe 29 ni maandamano au vurugu au ni maandamano ya amani, mnakosa majibu. Kwanini mfanye maandamano yasiyo na uratibu ulio wazi. Maandamano ni ujumbe kwa mlengwa, nyie maandamano yenu yako vipi?

Maandamano yasiyo na ukomo ya kuondoa serikali yanakuwaje ya amani? Allen, mbona ulikuwa na ubongo mzuri tu huko nyuma, nowdays umepatwa na nini?
 
Maandamano yasiyo na ukomo ya kuondoa serikali yanakuwaje ya amani? Allen, mbona ulikuwa na ubongo mzuri tu huko nyuma, nowdays umepatwa na nini?
Najua wewe na wengine mnafanya juhudi za kuhalalisha mauaji yaliyofanywa tarehe 29Oktoba. Lakini ule ulikuwa ni unyama usiomithilika.

Kuna mtu ametetea mauaji ya 29Oktoba halafu ghafla anaanza kuwashutumu waisraeli kwa mauaji ya wapalestina Gaza.

Nikamuuliza mbona Gaza anataja idadi ya watu wanaouawa na siyo maghorofa yanayobomolewa wakati Tanzania anataja mabasi ya mwendokasi na vituo vya mafuta vilivyochomwa moto bila ya kutaja idadi ya watu waliouawa 29Oktoba?

Hakuna jambo lolote lile linalozidi thamani ya uhai wa binadamu.
 
Najua wewe na wengine mnafanya juhudi za kuhalalisha mauaji yaliyofanywa tarehe 29Oktoba
Siyo juhudi ya kuhalalisha, uhalisia. Wafanya vurugu walikuwa na lengo baya kabisa kwa nchi na hivyo nguvu iliyotumika ni sahihi na sawa na nguvu waliotumia wafanya vurugu, kwa kivuli cha maandamano. Jambo pekee la ku regret ni waliokufa bila kuhusika na vurugu kufuatia vurugu zile. Na huo ndio msingi wa maoni yetu ya kukataa vurugu kama njia ya kudai haki kwasababu njia hiyo inaweza kuwaathiri wasiohusika kama ilivyotokea.
 
Nilishawai leta Uzi mmoja kuwa Kwa washindi wa tuzo ya amani ya Nobel wengi walipitia mazito Kama alivyopitia Lissu.

Sasa potential candidates wa tuzo ya Nobel Kwa 2026, Jina la Lissu linatajwa kupendekezwa.

Believe me Kwa yaliyomkuta Lissu, yeye ndo atashinda iyo tuzo 2026. Anae bisha tukutane mwakani.

Aione
Samia
Nassoro KatugaView attachment 3521651
Tuzo ya haki tutampa Bi Msumi. Happy?
Kaisha pata tiyari, hakuna wa kuzuia
 
Back
Top Bottom