Tundu Lissu apuuza wito wa DCI Kingai, asema hatoenda ofisini kwake

Huyo ana maana Lisu apigwe Tena risasi, hujamwelewa tu mbugila huyo?
 
Naona umepanic bila sababu punguza jazba ninachomaanisha ni hicho hicho ulichoandika sema neno mama limekukasirisha bila sababu.
 
Mengine yoooote uliyoandika hayana maana sana kwangu..

Lakini nina swali moja tu kwako. You say the letter is short and clear, right?

It's very clear kwa jicho na Kwa ufahamu wa mjinga pekee asiyejua sheria na jukumu la kisheria la jeshi la polisi...

Kwa sababu ktk macho ya kisheria as far as day to day legal responsibilities of police force is concerned, basi hiyo ni karatasi ya kufungia vitumbua tu..!!

Na hebu nikumbushe, hiyo barua inataja kosa gani kweli ambalo jamaa anatuhumiwa nalo na kutakuwa kuhojiwa? Kutotumia lugha ya staha kumkosoa Rais? Kwa sheria ipi inayozungumza makosa ya "staha?"
 
Kupitia baadhi ya matamshi yake lissu yapo hadharani anastahili kuhojiwa,zipo KAULI ambazo alizitoa ambazo ni za kufedhehesha,kutweza,kuvunjia heshima viongozi wa kitaifa,zipo za kuhatarisha Amani na umoja na uchochezi pia,asiogopwe hata kidogo!
Sasa ndugu Crocodiletooth, kama wanazo hizo kauli mikononi mwao na wanaona kuna makosa Kwa mujibu wa sheria fulani wanayoijua wao, si waende mahakamani na ushahidi wa matamshi hayo?

Polisi kwenda kufanya nini tena? Kuhojiana? Kwenda kuhojiana nini wakati una evidence tayari mkononi? Au hujui maana na sababu ya mahojiano ukiwa polisi?
 
๐Ÿค“ Kama sio kosa si aende tu awambie walio muita kwamba mlichoniitia sio kosa kisheria na yakaisha ๐Ÿ˜œ kubwekabweka na kiburi mingi yanini sasa.
Mbona wewe na hicho unachokitetea hamna uungwana? Mtaweza kuongoza kweli?

Atatiwa nguvuni, mtapoteza muda nendarudi Mahakamani badala ya kuchanja mbuga kwa wananchi.
 
๐Ÿค“ Kama sio kosa si aende tu awambie walio muita
Ngoja nikupe ufahamu na maarifa ya bure bila kunilipa ada yoyote;

1. Nani anayeamua kuwa kitu au jambo au kauli fulani ni kosa au sio kosa? Polisi au mahakama?

2. Bila shaka polisi "wanafikiri" kuwa TL kafanya kosa. Kama ndivyo, wafuate utaratibu sahihi wa kisheria kuthibitisha fikra zao!!
kwamba mlichoniitia sio kosa kisheria na yakaisha ๐Ÿ˜œ kubwekabweka na kiburi mingi yanini sasa.
Na nani anapaswa kujua hili at first place? Polisi wanaotuhumu au anayetuhumiwa? Bila shaka ni wale wanao - enforce law yaani, polisi..

Na ndugu yangu Tlaatlaah wakishajua, wanapaswa kufanya kinachotakiwa kufanya kisheria ikiwemo kufuata sheria namna ya kumtaka mtu awafuate huko polisi. Ni hivyo tu..!
Mbona wewe na hicho unachokitetea hamna uungwana? Mtaweza kuongoza kweli?
Uungwana ni upi? Kuchekavna kuwa petipeti wanaokiuka na kuvunja sheria au kuwakemea na kuukataa ujinga wao?
Atatiwa nguvuni, mtapoteza muda nendarudi Mahakamani badala ya kuchanja mbuga kwa wananchi.
Yaani atiwe nguvuni kwa hili hili la DP World na mkataba wa kimagungo wa Rais Samia a.k.a nani kama mama?

Bila shaka nawe utakuwa ni empty set upstairs...!!

Kwa heri..๐Ÿšถ๐Ÿšถ๐Ÿšถ๐Ÿšถ
Not now bro!!!!
 
๐Ÿค“๐Ÿ˜œ Sawa nashukuru kwa darasa. nimejifunza from the tone of your words naona hulka ya ubishi wa kuzaliwa na ujuaji usio na tija. Rahisi kuikuza na kuifanya ngumu kuvutia huruma. ๐Ÿšถ๐ŸšถEbana sawa kwaheri pia let's wait and see what will happen
 
Nimeamua nirudi ili tuzungumze...

1. MOSI, kwa kuanzia hebu nikushauri kitu kimoja kuwa, ili kuwa na health conversations, basi nakushuri kabla ya kuandika chochote, uwe unasoma hoja za wenzako kwanza ndo ujibu.

2. PILI, sina hakika kama ulichoandika hapa kinahusiana na nilichokiandika mimi ku - kwoti hoja yako ya awali. Hii inanifanya niamini kuwa wewe huna tabia ya kuwasikiliza au kuwasoma wenzio kwa makini ili kujua logic ya hoja zao kabla ya response yoyote. Mtu mwenye tabia hii siku zote huwa ni mtu mwenye kiburi cha kujiona au kujidhania anajua lakini ukweli ukiwa ni kinyume chake. Mimi siamini kama wewe uko hivi..!!

3. TATU, mimi siogopi kushambuliwa iwe kwa lugha kali au isiyo na staha (ili mradi isiwe matusi)...

Muhimu ni kuwa, nishambulie au nikemee vyovyote upendavyo aidha kwa kiniita mjinga au mpumbavu huku ukiwa unajibu hoja zangu. Nami nitakuthibitishia kuwa mimi si mjinga wala mpumbavu kwa hoja...

Lakini ku - attack personality ya mtu bila kujibu hoja yake mtu huyo, bila shaka nadhani huo afanyao mtu huyo itakuwa ni ujinga 100%..

MWISHO lakini si kwa umuhimu: Tuendelee na mjadala.

Na swali ni hili; Je, unadhani wito wa barua kumtaka TL kwenda kwa DCI Kingai kisheria uko sahihi?

Tukipata jibu hili ndo tutajua nani si muungwana na nani ni mbishi tu wa kuzaliwa..
 
UKIITWA POLISI NENDA MARA MOJA,ASIPOENDA INAGEUKA FADHAA KWA JESHI LETU,TUTII SHERIA NA WITO BILA SHURUTI.
 
With all due respectโ€ฆ tusipeane moyo wa keybord

Hakuna individual aiyeshindana na dola akashinda

life could be simpler if mh angeitikia wito
 
๐Ÿค“ Gentleman!! "Uzima Tele"
Naona una kitu tena kikubwa mno, actually una fikra pevu mno. I like that.
Lets not waste time kwa vitu ambavyo vinatuchelewesha sisi wenyewe Thank you commander, itikieni wito wa police kwa wema with positive mindsets mambo yaishe,
tusipoteze muda mwingi kufanya jamb lionekane kububwaaa, wakat kundi kubwa la waTz wanahitaji fikra mbadala za kimageuzi.
tunawachelewesha sana wa TZ kwa Ubinafsi na Ubishi usio na tija. Tunataka tu tuonekane na kusikika na hatimae kuhurumiwa
 
Kingai alishakana kuwa sio yeye bali ni Mzanzibari Masauni!!!
 
๐Ÿค“ Gentleman!! "Uzima Tele"
Naona una kitu tena kikubwa mno, actually una fikra pevu mno. I like that.
Thanx for the compliment..
Lets not waste time kwa vitu ambavyo vinatuchelewesha sisi wenyewe
Nyie kina nani na ni vitu gani hivyo vinavyo wachelewesha?

Sikiliza ndugu Tlaatlaah, kuwa, kufanya mambo kinyume cha utaratibu na sheria tulizoziweka sisi wenyewe ili kuwezesha smoothness ya kuendesha maisha yetu kwa wajibu na haki,HUKO NDIKO KUHARIBU NA KUCHELEWESHA MAMBO TUYATAKAYO..!

It's very simple like this๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰, tell the police to re - write their call letter for Mr TL kwa kufuata kuzingatia sheria. Ni hilo tu
Thank you commander, itikieni wito wa police kwa wema with positive mindsets mambo yaishe,
Rudia kunisoma tena hapoโ˜๏ธโ˜๏ธโ˜๏ธโ˜๏ธjuu...

Just to remind you, kwamba, things don't go like that. Wito wa polisi huwa ni document ya kisheria. Ikikiuka sheria, hiyo ni ya kupuuzwa tu..!!

Na kumbuka hili: Mjinga akikushurikisha jambo lake la kijinga nawe ukakubali kushiriki, nawe automatic unakuwa mjinga pia..!
tusipoteze muda mwingi kufanya jamb lionekane kububwaaa, wakat kundi kubwa la waTz wanahitaji fikra mbadala za kimageuzi.
Ni jambo kubwa kwako wewe Tlaatlaah..!!

Kwa Tundu Lissu na kwangu mimi that's completely nothing bali ni hila zilezile za miaka yote za baadhi ya viongozi wa serikali dhidi ya wakosoaji wa sera, mipango na matendo ya watawala wajinga na wapumbavu wa nchi hii kwa kulitumia jeshi la polisi ama baadhi ya maofisa wa jeshi hilo akiwemo DCI Ramadhani Kingai na IGP Cammilius Wambura...

Unfortunately kwao ni kuwa ama ni wajinga wa sheria au wanafanya makusudi kukiuka sheria ktk utendaji wao wa kila siku only to impress their gold digger masters..!

Hawa wakiukao sheria kiuhalisia ndio wanaochelewesha shughuli za maendeleo zisiende mbele kwa haraka na kamwe sio kina Tundu Lissu wanaopigia kelele uvunjivu wa sheria..!
tunawachelewesha sana wa TZ kwa Ubinafsi na Ubishi usio na tija. Tunataka tu tuonekane na kusikika na hatimae kuhurumiwa
Kwa hoja ya "tunachelewesha sana waTZ", nimetoa maelezo yake Kwa kirefu hapo โ˜๏ธโ˜๏ธโ˜๏ธโ˜๏ธjuu.

Na wewe nikushauri jambo moja, kuwa chunguza kabla ya kukubaliana na jambo liwe linatoka Kwa waserikali au Kwa Tundu Lissu au kwangu mimi. Na ukiona haliko sawa, likatae hapohapo au mwambie atakaye hivyo arekebishe..

Kwa ninavyoyasoma mawazo yako wewe, inaonekana una - argue hoja zako si kwa kutafuta maarifa yako mwenyewe bali kwa kuwa "unasikia tu" au "unaamini viongozi wa serikali kwa kuwa wamesema" bila kusumbua akili yako kutaka kujiridhisha kama kilichosemwa Kiko sahihi au la...

Na kwa kumalizia tu nikuulize swali hili, kwamba, hivi kwa kadiri ya ufahamu wako wewe Tlaatlaah unadhani Tundu Lissu miongoni mwa wanasheria bora kabisa Tanzania na pengine duniani anaweza kugomea wito wa polisi iwapo hauna kasoro yoyote kisheria?
 
๐Ÿค“๐Ÿค๐Ÿ™Œ๐Ÿค
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ