Tundu Lissu arejea Nchini asema ripoti ya CAG ufisadi ni uleule, mambo ni yaleyale

Tundu Lissu arejea Nchini asema ripoti ya CAG ufisadi ni uleule, mambo ni yaleyale

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648

Mwandishi: Ripoti ya CAG imetoka na majibu ya Rais ni kwamba waliofanya madudu wampishe. Unadhani hiyo ni kauli ya kitendaji au ya kimamlaka?

Lissu: Kwanza wizi na ufisadi ni ule ule wa miaka yote, kama haujaongezeka, ninachosoma ni kwamba umeongezeka. Wizi ni ule ule, wa watu wale wale, wa chama kile kile, mambo yale yale, ahadi zile zile. Kwahiyo kusema ampishe, nani ndie mwajiri mkuu wa nchi hii? Nani anawapa hizo kazi, nani mwenye mamlaka ya kuwaondoa? Ni mambo yale yale!
 
Ajabu, mtendaji mkuu au bosi wa serikali anawaomba wezi wa mali ya umma wampishe, huu udhaifu ni zaidi ya ule wa enzi za JK.

Hapa ndipo penye kiini cha matatizo yetu, wala tusidanganyane na story za mifumo, na kama huyu dhaifu+ ataendelea kutuongoza mpaka 2030, mbwa mwitu watatutafuna mpaka mifupa.
 
Nakumbuka Kangi Lugola aliambiwa na Hayati Magufuli 'sikutegemea kukuona hapa ...' na masaa machache kila mtu anajua kilichotokea.

Kauli ya Mhe.Rais ni ya kimamlaka kwa sababu uwezo wa kuwaondoa anao na kuombwa kupisha ni kutambua uwajibikaji
 
No siwezi kumuuliza swali hilo kwasababu sio swali. Kuna type ya maswali very specific to Lissu, nikifanikiwa kupata appointment nitaileta humu JF.
P
Lakini hata yeye huwa anatoa maneno makali sana

Kweli unachagua maswali ya kumhoji na ninaheshimu kazi yako
Dunia hii ya leo ipo wazi sana kwa kila jambo
Kila la kheri tunasubiri hiyo interview
 
Back
Top Bottom