Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar.9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini. Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar.10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.! #Mwamba #AkiliKubwa #NiYeYe